Hakuna tafsiri nzuri zaidi ya hii kuhusu hali inayomkabiri Samia wakati huu na kufanya maamuzi ya ajabu ajabu hivi.Ni pale mtu anapoamua kumtafuta jambazi mkuu awe mlinzi wake akijua kuwa hakuna jambazi atakayemtishia kwa sababu yeye ameshikamana na jambazi mahiri zaidi kwenye ujambazi. Ni sawa na ule msemo kuwa mpe mchawi akulelee mwanao kwa kuamini hakuna mchawi atakayemnyemelea.
Samia inaonekana amekuwa na tamaa ya uongozi kiasi cha kuwa tayari kufanya chochote alimradi kama itamsaidia kuulinda Urais.
Tokea ule mkasa wa DP World, huyu mwana mama kapoteza hata kile kidogo alichokuwa anakitegemea kuwa kitamsaidia kuendelea kushika madaraka. Sasa amebaki kutapatapa kama mfa maji.