Sasa kama taasisi zote zimekuwa compromised hivyo kipi kinakufanya uamini jeshi nalo halijawa compromised?Ukweli ni kwamba Taasisi zote na mifumo yote nchi hii imekuwa compromised vibaya sana. Elewa neno vibaya sana.
Nchi hii sasahivi watumishi na mifumo inaiabudu CCM kuliko Katiba na Taifa.
Si Mahakama, Si Tume ya Uchaguzi, si TISS, si Polisi, si TAKUKURU, si Uhamiaji si Magereza si DPP si Mwanasheria Mkuu si Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora si Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Hakuna namna nchi hii inaweza kujengwa vizuri sasa bila kufanyiwa overhaul.
Na njia pekee iliyopo ya kufanya overhaul na kuanza kujenga mifumo na Taasisi upya inayoweza kufanikiwa lazima ilihusishe Jeshi.
Nchi hii imeoza
Jeshi lina afadhali kuliko hao wapuuzi wengine.Sasa kama taasisi zote zimekuwa compromised hivyo kipi kinakufanya uamini jeshi nalo halijawa compromised?
Unaweza kui compromise jamii nzima halafu jeshi likasimama bila kuwa compromised?
Hao wanajeshi wanaishi katika kisiwa gani ambacho hakifikiwi na Watanzania wengine wote waliokuwa compromised?
Hilo jeshi lishakuw acompromised na chama na siasa siku nyingi sana tangu uasi wa 1964. Nyerere alisema never again shall we face this shameful predicament.Jeshi lina afadhali kuliko hao wapuuzi wengine.
Jeshi shida ipo kwa wakubwa wachache sana ambao wanaweza kuwa contained na wenzao humo humo sio kama hawa wajinga na washenzi TISS, Polisi, TAKUKURU, Mahakama na wengineo.
HapanaHilo jeshi lishakuw acompromised na chama na siasa siku nyingi sana tangu uasi wa 1964. Nyerere alisema never again shall we face this shameful predicament.
Akahakikisha jeshi linakuwa politicized sana.
Hakuna lolote linaloweza kutokea kutoka jeshini.
Hususan kama wananchi wenyewe hawajafanya kazi yao.
Yaani hali ni mbaya, Watumishi wa umma wamegeuka misukule ya CCM,. wanasubiriwa tarehe 29 ambaye hatatiki kitakachomkuta atasimuliaUpumbavu unaoendelea kwenye Taasisi za Umma umefikia kiwango cha kutisha hakika.
Watumishi wa Umma, badala ya kujikita kulitumikia Taifa ili Wananchi wawe na maendeleo sasahivi wamegeuka kuwa vijakazi na watumwa wa CCM. Kuwahudumia CCM badala ya kulihudumia Taifa.
Vitendo vilivyofanywa na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kulipa watu kuandamana eti kumuunga mkono Samia na CCM ni ishara kubwa sana kuwa Taasisi za Umma nchini zimeshajifia na sasa zinafanya kazi kwa ajili ya CCM na sio Taifa tena.
Kwa hatua tuliyofikia Tanzania, ni dhahili kuwa Taasisi zote zimekuwa compromised na ujinga wa kisiasa ( Political Stupidity) na dawa pekee kulikomboa Taifa ni Jeshi kuchukua hii nchi na kuanza kuisuka na kuijenga upya.
View attachment 3490218View attachment 3490219
Updates
Uthibitisho mwingine wa namna Taasisi za hili Taifa zilivyojifia ni namna walivyomfanyia John Heche wakati anaenda Msibani jana ba hili tamko walilolitoa jana Uhamiaji wa Tanzania
Kwa akili za kawaida tu kila mwananchi ameona kilichotokea jana na nguvu ya Umma ilivyotumika kumuingiza Heche Kenya alafu hawa wapumbavu Uhamiaji kwa ajili ya kutumika kisiasa tu wamekuja na tamko hili la kipuuzi.
View attachment 3490570
Kutegemea jeshi lilete demokrasia, haki na uhuru ni contradiction.
Jeshi linatawala kijeshi na halina guarantee yoyote ya kuheshimu demokrasia, haki wala uhuru wa watu.
In fact jeshi likipindua nchi kitu cha kwanza lina suspend katiba na kutangaza a military council, martial law, curfews and rule by military decrees.
Watanzania wanaotajataja sana jeshi lichukue nchi wengi wana tabia hizi.
1. Wako desperate. Desperate people do desperate things. Mfa maji haishi kutapatapa. Mtu anayezama hata akiona unywele ataushika ili asizame.
2. Wavivu. Watu wavivu wanapenda kuwapangia wengine wafanye kazi wanayotakiwa kufanya wao. Badala ya wao kufanya wajibu wao kuitoa serikali wanayoona dhalimu madarakani, wanalisukumia wajibu huo jeshi.
3. Wanapenda shortcuts. Badala ya kufanya kazi kubwa na nzito ya kuelimisha jamii ili jamii ijue uhuru ni nini, ifanye mabadiliko ya kimsingi ya kijamii, wanakimbilia shortcut ya kutaka jeshi lichukue madaraka.
4. Wanapenda kutumia nguvu kuliko kutumia akili. Ni watu ambao wanaona jeshi ni alama ya kutumia nguvu. Wanaamini katika kutumia nguvu sehemu ambayo panatakiwa kutumia akili. Wanapenda show za kibabe. Ndiyo maana hata marais ambao hawamo jeshini ukiondoa vyeo vya kisiasa kama Commander In Chief, wanapenda kuvaa magwanda ya kijeshi. Wanasiasa washajua wakivaa magwanda ya kijeshi wananchi wanalainika. Just the projection of military power does it for most Tanzanians.
5. Hawana akili za kuangalia mambo kama unintended consequences, bad precedent, na madhara ya muda mrefu ya mapinduzi ya kijeshi. Kifupi ni watu wenye akili fupi sana ambao hawawezi kupima mambo kwa kina.
Jeshi likichukua nchi kuta kitu hata CCM watajifunza watanzania wengi wanataka tukose wote wanaotaka Jeshi lichukue nchi wanataka na CCM wakose wajifunze wana hoja
Hakuna wa kuitamani hii hali. Hii nchi saivi imejifia na inahitaji kufanyiwa overhaul.Jeshi akichukua nchi sio tu tutakuwa tumekosa sote, bali tutakuwa tomekosa zaidi. Hii hali tulionayo sasa tunaweza kuja kuitamani pia ikashindikana.
Kumbuka unaongelea nchi za AfricaHili nalo ni tatizo la msingi.
Wananchi wasiojua wanataka nini ni tatizo.
Wananchi wanatakiwa kuwa na ownership ya mambo yao, kupanga wanachotaka.
Si kusubirisubiri waambiwe tu wafanye nini.
Hapana hauwezi kuwa hivi. Na ni bora kuliko hii ya ssJeshi akichukua nchi sio tu tutakuwa tumekosa sote, bali tutakuwa tomekosa zaidi. Hii hali tulionayo sasa tunaweza kuja kuitamani pia ikashindikana.
Na huku kuuana ,kutekana? Like seriously? Aucsbb wenzetu mifumo inawanufaisha ndo maana mnaona bora hali hii?Wanajeshi ndo wajinga kabisa,bora tubaki na haya mafisadi tu
Hakuna wa kuitamani hii hali. Hii nchi saivi imejifia na inahitaji kufanyiwa overhaul.
Kwa kuwa mifumo yote imekuwa compromised hatuna namna zaidi ya kuanza upya na hapo ndo umuhimu wa Jeshi kuongoza kipindi cha mpito na kutupatia Katiba mpya unapoonekana.
Hapana hauwezi kuwa hivi. Na ni bora kuliko hii ya ss
Maelezo marefuuu upuuzi mtupu .Wewe ndiye unasumbuliwa na fikra finyu.
Kwa sababu badala ya kuchambua hoja umenishambulia mimi binafsi.
This is a logical fallacy, ad hominem logical fallacy.
Halafu pia una uwezo mdogo wa kufikiri. Hujui kusoma kwa ufahamu.
Umefanya logical fallacy nyingine ya logical non sequitur.
Kukataa utawala wa kijeshi si kukataa kupata njia mbadala, ni kukataa kupata njia mbadala ya utawala wa kijeshi. Kuna njia mbadala nyingine ambazo hazihusishi utawala wa kijeshi.
Hapa umefanya logical fallacy nyingine, false dichotomy.
Umefanya kuwa mambo yanayoweza kuwepo ni mawili tu, uongozi wa ufisadi huu tulionao au mapinduzi ya kijeshi. Mimi nakataa options zote hizi mbiki. Nakataa uobgozi wa sasa wa kifisadi na nakataa mapunduzi ya kijeshi pia.
Hujaweza kufungua akili yako na kuona kuwa, kwa mfano, watu wanaweza kuandamana mpaka kuiondoa serikali iliyopo madarakani kwa popular uprising isiyotumia mapinduzi ya kijeshi.
Kwa nini unalazimisha hii false dichotomy ya "uongozi wa kifisadi au mapinduzi ya kijeshi" tu?
Mi nimeshawaambia hao wanaolitegemea jeshi lichukue nchi, kuwa imekula kwao.Hilo la jeshi ni wazo la kijinga mara mbili.
Ni wazo la kijinga kifalsafa. Kwa sababu kutaka demokrasia, haki, na uhuru kwa juweka jeshi ni contradiction.
Lakini pia, hata ukiondoa habari za falsafa, ni wazo la kijinga practically.
Kwa sababu wanajeshi wenye uwezo wa kupindua nchi karibu wote wahalelewa na kifadhikiwa chini ya CCM. Hawawezi kuiasi CCM. Wanasema wanatetea katiba hawawezi kupindua nchi.
Mnakuwa kama fisi anayemfuata mtu anayetembea mkitumaini kuwa kuna siku mkono wa yule mtu utaanguka.
Wakati mkono hauanguki.
Kama mnategemea jeshi tutarudi hapa 2030 na 2035 tunalialia hivihivi.
Mkuu Kiranga siyo dhamira yangu kubishana ,lengo langu nikutafuta uelekeo unaofaa .Ukisharuhusu mapinduzi ya kijeshi mara moja umeruhusu mapinduzi ya kijeshi mara zote.
Kwa marais wote, wanaofuata katiba na wasiofuata katiba.
Maana yake nyie mtampindua rais wa CCM mkamuweka wenu, na CCM nao watatafuta wanajeshi wao na kumpindua rais wenu.
Angalia nchi zote zenye mapinduzi ya kijeshi huwa na tabia ya kurudiarudia mapinduzi hayo, usijidanganye kuwa utafanya mapinduzi mara moja tu.
This is like the proverbial genie out of the bottle.
Once out, you can't contain it.
Huelewi wapi?
Unataka kumpanda Chui mgongoni akufikishe unakotaka kwa kasi, wakati ukishampanda huyo Chui huna namna ya kum control aende wapi, huna namna ya kumsimamisha kumwambia hapa nishafika ninapotaka kwwnda, na hata ukiweza huna uhakika ukishuka hatakuua.
Huelewi wapi?
Kaka heshima kwako kwa uwezo mkubwa wa kujenga hoja uliouonesha dhidi ya huyu juha wa kujiita Kiranga tangu mwanzo mwa huu uzi mpaka hapa mlipofikishana.Maelezo marefuuu upuuzi mtupu .
Hoja ya msingi ni hii ,KWANINI UNADHANI WATANZANIA watamani utawala wa kijeshi na siyo utawala wa kidemocrasia?
Sababu ni nyepesi tu .
SETTING MODEL YA MFUMO WA UTAWALA WAKIDEMOKRASIA umeshindwa kutoa maajabu na ndiyo maana watanzania wanaona hawana tena njia nyingine .
Swali linaweza kuwa je! Hakuna mfumo mwingine Bora zaidi ya huo ?
Jibu ,unaweza ukawepo lakini kwasababu ya political model yetu imepeleka madaraka makubwa kwenye chama tawala , umesababisha kusiwe nalango mwingine wakutupeleka huko , unless otherwise huo upande uwe na maslahi ya chama tawala na nikitu ambacho tuseme zitabaki kuwa ndoto .
Labda tu nihitumishe kwa kusema .
Hakuna anaependa au kutamani kuona Taifa letu likiongozwa na jeshi lakini hakuna njia nyingine mbadala zaidi ya hiyo ,kumbuka yamajadiliano yanayobebwa na dhamira safi hayajawahi kuwapo zaidi ya yake ya ujanja ujanja
Ukweli ni ukweli tu, haujali uko Africa au Antarctica.Kumbuka unaongelea nchi za Africa
Hatuna uhakika kama jeshi litaheshimu katiba, ila tuna uhakika kuwa waliopo sasa hawaheshimu katiba. Kama jeshi halitoheshimu tutakuwa tumepata hasara gani ilhali tayari tunaishi katika nchi isiyoheshimu katiba? Si ni bora tuwape wavunja katiba wapya kuliko kuendelea na hawahawa
Si ni bora tuwape wavunja katiba wapya kuliko kuendelea na hawahawa