Ukitaka kuishi maisha marefu ktk nchi hii inaitwa Tanzania basi usitake Sana kujua yanayoendelea ndani ya Hiyo nchi.
Wenye mamlaka ya kuchukua hatua na kuwajibisha nao wanalalamika pamoja na wananchi.
CCM Ni mduara wa wizi/ujambazi uliotukuka.
Hao tunaotaka Rais awachukulie hatua Ni wenzake ndani ya chama na serikali. NANI AMFUNGE PAKA KENGELE?
Rais yeye ni msafi? Hapigi madili? Km anapiga si anapiga na Hawa Hawa tunaotaka wachukuliwe hatua?
Rais Ni mwanasiasa, hadharani anaweza kufika ndani wataenda kukaa na kuona namna ya kuzima Moto.
Tatizo la Tanzania au mfumo, Wala siasa zetu, tatizo la Tanzania Ni Watanzania wenyewe.
Ktk watu zaidi ya milioni 60,marehemu Ni karibia milioni 50.Walio hai Ni wachache. Sisi Ni taifa la wafu, watu wasiohoji, watu wasiochukua hatua. Hatujitambui.