Tunaposikia ya Makamba na Zitto kutaka kubinafsisha TANESCO, tukumbuke yaliyofanyika TTCL

Dunia ndio inapoelekea uko,huoni ushindani uliopo kwenye mitandao ya simu,je wewe hapo ulipo unaweza kuwa na mtandao na wa Ttcl,ngoja serikali wafungue milango kwa makampuni binafsi uwone kitakachotokea kama hao Tanesco watakuwepo
Tanesco itaendelea kuwepo mzee running cost ya mitandao ya Simu ni Rahisi sana sio tanesco mzee ambapo asset kama transformer ni ghali, Mnara mmoja unaweza kuserve wateja wengi sana gharama ya simcard je si simple sana je leo mwekezaji atakubali Kujenga miundombinu hapo hapo Ulipie 27k hahahaha
 
Kuhusu bei kutakuwepo na ewura yake ya kucontrol bei...kwa kifupi changamoto zote mnazoziainisha hpa zinatatulika ninachoona kwenu ni uknown fear
 
Hapo umeonyesha jazba tu hakuna hoja ya maana.
 
Hakika... Mimi sijawahi kujua Taaluma ya Ndg. February....
 
Wewe uko Dunia ya wapi?!!..Hii 27000 bado gharama sana!!....Tukipata mshindani au kubinafsisha bei itapungua maradufu!!..Tuna vyanzo vingi vya nishati ya Umeme!!
 
Na wewe kwa siku hizi umekuwa usiye maana
 
Wazalishaji wakiwa wengi automatically umeme utashuka bei sababu ya ushindani...ni km ilivyo saiv kwenye mitandao ya simu

Mnapotolea mfano wa mitandao ya simu napata mkanganyiko akilini!

Mitandao hiyo mnayoisema ndio hii inayotupa mabando kwa bei ya juu na kuruhusu matozo ya kila rangi kwenye miamala yetu ama ni ipi?!

Mitandao ya simu ambayo mpaka leo imefanya kupata wireless technology imekua kma starehe na ufahari wa Mali?
 
Sekta binafsi imejenga na kuendesha miundo mbinu na uzalishaji wa umeme dunia nzima, kwanini unafikiri kwa TZ haiwezekani? na serikali badala ya kutoa pesa kwa TANESCO kila siku inaweza kutoa ruzuku kwa wananchi moja kwa moja mfano hiyo 27K tunajua sio bei halisi, hapo serikali inaweza kusaidia ili mwekezaji alipwe market price...ninapoishi market ya umeme yote ni private sector 100% na sijawahi kuona umeme umekatika for the last 20 years na umeme ni bei rahisi sana
 
Dunia ndio inapoelekea uko,huoni ushindani uliopo kwenye mitandao ya simu,je wewe hapo ulipo unaweza kuwa na mtandao na wa Ttcl,ngoja serikali wafungue milango kwa makampuni binafsi uwone kitakachotokea kama hao Tanesco watakuwepo
Je Ushidani unaamisha Ubinafsishaji ?
Je kwahio unataka vyanzo vya Nishati HEP (Kidato, Nyerere n.k. ) tuviuze au ? Kwanini hao so called wawekezaji wasije na vyao vicompete na Tanesco...

Gesi je tuendelee kuwapa au ibaki kuwa mali ya jamii kwa manufaa ya jamii ? Kumbuka Private entities ni Profits at all Costs lakini State Owned mara nyingi ni service oriented (Community Welfare)

Am all for Free Market and what not..., lakini sio watu watumie mali na assests za jamii kwa kujifanya wao ndio waendeshaji wazuri sana..., watengeneze na kuanzisha zao alafu waziendeshe
 
Tatizo kwa sheria za Tanzania sekta binafsi hairuhusiwi ni TANESCO tuu yenye monopoly 100%, unaweza kuzalisha umeme na kuwauzia TANESCO lakini sio wananchi na wanakupangia bei, if you are for free market..thats not free market
 
Hivi kwanini tusiruhusu mashirika huru ya umeme kuanzishwa ili kuondokana na tatizo la umeme nchini?
maana kiukweli TANESCO ni wamezidiwa ile mbaya.
Wazo zuri kabisa.

Lakini nami naomba nikuulize jambo moja.

Hivi kwa nini Tanesco na mashirika mengine ya uma hayawezi kufanya kazi vizuri ili wananchi wafaidike na matokeo ya kazi zao?

Mkuu naomba ueleze hapa sababu unazozijua wewe ambazo zinafanya haya mashirika yasifanikiwe, kiasi kwamba uone kuwa ni muhimu "turuhusu mashirika huru ya umeme" (sijui una maana gani na "mashirika huru"?
 
Haya mawazo ya kubinafsisha Taneco ni bonge ya dili majuto baadae wa walipa Bili za umeme bei itakua inapanda kuliko petroli na sukari
 
Hiyo Gas na Maji nikuongezee na Upepo bado huwezi kuendesha shirika
 
Haya mawazo ya kubinafsisha Taneco ni bonge ya dili majuto baadae wa walipa Bili za umeme bei itakua inapanda kuliko petroli na sukari
Kama Tanesco wananunua Umeme Kwa watu binafsi unaonaje hapo?!;..Je serikali inauza umeme ghali au sekta binafsi
 
Laki
Ni awamu ya tatu walifanya matokeo haya kuwa chanya?
Je kwa sasa wamejipanga je?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…