Mimi sipo katika imani ya ukristo ila nimeona swali lako nikaona nichangie...Kwanini Mungu hana maadili?
Kuwekewa maadili ni jambo linaloonesha kuwa upo chini ya sheria fulani ulizoamrishiwa kutoka katika mamlaka iliyo juu zaidi inaweza kuwa mzazi, serikali, ofisi au hata Mungu.
Miongoni mwa sifa za Mungu ni kuwa yeye ndiye wa mwanzo na wa mwisho, ni mmoja hana mshirika katika utawala wake, ni mkuu na yeye ndiye mfalme na ndiye mshindi.
Mungu ndiye Mkuu kwa maana yake hakuna yeyote kumzidi yeye. Muweza wa kila kitu lakini licha ya hayo bado Mungu amejihukumia mwenyewe kuwa Rehema na huruma yake izidi hasira na ghadhabu zake. Ndio leo hii unaona licha ya viumbe kufanya kila aina ya uovu hapa ardhini bado Mungu anatupa chakula, maji, hewa n.k...anawapa mali watu waovu kabisa ambao laiti kama wewe ungekuwa umepewa hayo mamlaka basi usingewapa watu hao hata tone moja la maji kutokana na ubaya wanaoufanya. Mungu anawapa mpaka wale wanaomkana.
Mungu ndiye mfalme hakuna wa kumpangia, anaamua mambo kutokana na hekima na busara zake ambazo wewe mwanadamu huna uwezo wa kuzielewa hata kidogo.
Mfano anaweza kukupa mtoto kisha akamfisha angali mchanga,kikawaida wewe mwanadamu huwezi elewa hekima zake Mungu ila kumbe huyo mtoto aliyemchukua angali mchanga pengine angekuwa chanzo cha wewe kufedheheka hapa duniani na hata kujuta kwanini ulimzaa...mfano labda huyo mtoto angekua na kuja kuwa Shoga.!!
Mungu kwa elimu na hekima zake anaamua kumfisha angali mchanga then anakupa mtoto mwingine mwema atakae kuja kukufaa baadae. Hakuna ajuae haya isipokuwa Mungu mwenyewe. So Mungu hapangiwi wala haulizwi wala hawekewi uzio wa kutenda (maadili).
Hao watu unaosema walikuwa ni wajawazito,watoto n.k waliogharikishwa wakati wa Nuh. Unajua kuwa Mtume Nuh alitumia zaidi ya miaka 950 kuwaita waelekee katika njia ya Mungu ila waliishia kumdhihaki na kumkufuru Mungu ila Mungu aliwavumilia miaka yote hiyo, mwisho akamwambia Nuh kuwa hata afanye jitihada gani kuwaita hawawezi kuitikia na kuamini na hawatazaa isipokuwa wale ambao nao watarithi ukaidi wa baba zao,hvyo Mungu mwisho akaamua kuteketeza na kuangamiza kizazi chote cha wasioamini.