Tunavyojidanganya kuhusu mapinduzi huko Sri Lanka

Rais na familia yake wametawala miaka kibao na wanaishi kwa kuwakebehi wananchi huku wakila raha

Maisha yamekuwa magumu kiasi ambacho hata mafuta ya magari yakakosekana kabisa na hata chakula Hakuna

Sasa ulitaka wale mawe?

Wanechoka na maisha hayo na ujue hawa jamaa wamepigana wengi na wanaona kabisa hakuna raha mbeleni zaidi ya mapinduzi na kupata wengine wa kuongoza nchi

Ila Waziri Mkuu yamemkuta safi sana na bado
Nyie mnafikiri mtakaa maisha hapo kubadilishana Post wale wale miaka 50
 
Salaam wakuu.
Hivi majuzi kumetokea vurugu huko nchini Sri Lanka baada ya wananchi kutoka kila nyanja ya maisha kuingia ikulu ya Raisi na makazi ya Waziri Mkuu kuwataka kujiuzuru na hadi wakati huu bado wananchi wanaendelea kukalia makazi na ofisi hizo hadi pale viongozi hao watakapo jiuzuru.

Kwa picha ya kawaida tunaweza sema wale ni wananchi ndio waliofanya au wanaotaka kuitoa madarakani serikali ila ukweli ni kwamba nyuma ya pazia ni kuna mkono wa mfumo na idara za usalama au nguvu toka mataifa ya nje.Wengi mataifa ya Afrika wanajidanya kuwa hata wao kuna siku wanaweza fanaya kama walivyo fanya wananchi wa Sri Lanka ukweli ni kwamba kamwe haiwezi tokea.

N.B
Ukiona Raisi anapinduliwa au anauliwaa ujue kuna mkono wa idara a usalama au mataifa ya nje.
Leo nilikuwa nasikiliza BBC World Service.

Kuna mwanasiasa mmoja wa Sri Lanka ambaye anajiandaa kuchukua urais alikuwa anahojiwa.

Akaulizwa, haoni kwamba kuna hujuma za nje katika migogoro hii ya Sri Lanka? Akatajiwa China na jinsi ilivyotoa mikopo mikubwa Sri Lanka, kwa namna ambayo Sri Lanka imeshindwa kulipa mikopo?

Yule mwanasiasa akajibu kwamba, haangalii suala hivyo, kwa sababu hakuna mtu wa nje anayeweza kuiingilia nchi kwa namna hiyo bila viongozi wa hiyo nchi kukubali. Kwamba hata hiyo mikopo ya kutoka China, viongozi wa Sri Lanka waliikubali.

Kwa hivyo, hoja hizi za nchi kuhujumiwa na watu wa nje, mara nyingi zinakuwa haziangalii ukweli kwamba si rahisi kwa watu wa nje kuhujumu nchi bila msaada wa viongozi wa nchi hiyo.
 
Rais na familia yake wametawala miaka kibao na wanaishi kwa kuwakebehi wananchi huku wakila raha

Maisha yamekuwa magumu kiasi ambacho hata mafuta ya magari yakakosekana kabisa na hata chakula Hakuna

Sasa ulitaka wale mawe?
Wanechoka na maisha hayo na ujue hawa jamaa wamepigana wengi na wanaona kabisa hakuna raha mbeleni zaidi ya mapinduzi na kupata wengine wa kuongoza nchi

Ila Waziri Mkuu yamemkuta safi sana na bado
Nyie mnafikiri mtakaa maisha hapo kubadilishana Post wale wale miaka 50
Kuna watu wengi sana wanaopenda kutetea watawala wabovu kwa ujinga wa conspiracy theories za kusema kwamba matatizo ya wananchi yameletwa na mabeberu wa nje, au hata kusema hakuna matatizo kuna njama za mabeberu tu.

Dunia inaendeshwa na geopolitics.

Lakini, rais akijikojolea mwenyewe wakati kalewa huku akitoa hotuba kwa mamilioni ya watu, asisingizie mabeberu.
 
Kwa picha ya kawaida tunaweza sema wale ni wananchi ndio waliofanya au wanaotaka kuitoa madarakani serikali ila ukweli ni kwamba nyuma ya pazia ni kuna mkono wa mfumo na idara za usalama au nguvu toka mataifa ya nje.Wengi mataifa ya Afrika wanajidanya kuwa hata wao kuna siku wanaweza fanaya kama walivyo fanya wananchi wa Sri Lanka ukweli ni kwamba kamwe haiwezi tokea.
Wewe haya umeyajuaje?

Ni kipi kinachokufanya usiamini kuwa watu hao wanao uwezo na utashi wa kufanya wanayofanya wao hadi uje hapa kuhoji; na unahoji na kutueleza sisi kwa nia gani?
 
Kuna watu wengi sana wanaopenda kutetea watawala wabovu kwa ujinga wa conspiracy theories za kusema kwamba matatizo ya wananchi yameletwa na mabeberu wa nje, au hata kusema hakuna matatizo kuna njama za mabeberu tu.

Dunia inaendeshwa na geopolitics.

Lakini, rais akijikojolea mwenyewe wakati kalewa huku akitoa hotuba kwa mamilioni ya watu, asisingizie mabeberu.
Na hata ukitazama mwelekeo wa mahojiano uliyoyagusia hapo juu kuhusu ushiriki wa China, chombo hicho cha BBC ni kama kinapalilia nadharia ile ile ya nchi za Magharibi dhidi ya hizi nyingine zinazoibuka, kama China. Ni kama vita baridi inarudi palepale pa zamani.
 
Mnapendaga kuwapa sifa "usalama wa taifa" wakati sio lolote sio chochote kama jeshi likigoma. Watawala wa dunia hii ni jeshi. Ndo maana utaona duniani kote jeshi ndo huwa wanafanya mapinduzi na si usalama wa taifa. Wakiamuaga jambo lao hakuna wa kuleta fyoko...ikiwamo na hao usalama wako
 
Na hata ukitazama mwelekeo wa mahojiano uliyoyagusia hapo juu kuhusu ushiriki wa China, chombo hicho cha BBC ni kama kinapalilia nadharia ile ile ya nchi za Magharibi dhidi ya hizi nyingine zinazoibuka, kama China. Ni kama vita baridi inarudi palepale pa zamani.
Zamani hata Mimi nilikua naamini wananchi wanaweza wakaamka tu huko waliko wakaenda kumtoa rais ikulu.

Unakumbuka Yale maandamano ya wananchi wa ukraine Ile 2014 kwenda kumng'oa rais wao( Viktor Yanukovych) ikulu?

Ilivuja audio ya mazungumzo ya balozi wa USA nchini Ukraine akizungumza na State department huko USA khs mipango hio.Na kuna picha ikaachiwa Tena ya U.S. Assistant Secretary of State for European na Eurasian Affairs Victoria Nuland na U.S. Ambassador hapo Ukraine Geoffrey Pyatt nao wakiwa kwny maandamano na wananchi.

Hivi fikiria kingetokea kitu gani wkt wa utawala wa Trump ile siku wananchi wanaandamana kwenda kwny bunge la Marekani halafu balozi wa Tz nae akawa pamoja na wananchi wa Marekani wakiandamana?
 
Tena Ile Nchi ilitoka kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe si chini ya miaka 10 iliyopita na waliopindukiwa sasa ndio waliwapindua wenzao..

Kwa hiyo this time around waliopinduliwa wamepata kisingizio ndio maana unaona watu wa Usalama walikaa kimya tuu.
 
..Jeshi haliwezi kuingia ktk VITA ambayo Majenerali wanaamini uwezekano wa kushinda haupo, au ni wa gharama kubwa.

..Wakati mwingine hali halisi / situation on the ground hubadilika kwa haraka na kupelekea jeshi kutokuwa na uwezo kuingilia.

..Kwa Srilanka jeshi lazima limeangalia hali halisi na kuona hakuna namna ya kufanya zaidi ya kuiacha serikali ianguke.
 
Wananchi wakiamua lao hakuna linaloshindikana....nyie endeleeni kuwachosha tu wananchi siku wakichoka ndo utajua hujui

..wakati mwingine mambo hubadilika kwa kasi ambayo usalama wa taifa, na jeshi, wanashindwa kuidhibiti.

..Hali hii inanikumbusha siku Tundu Lissu aliporudi hapa nchini. Polisi walipiga marufuku mapokezi yake, na walijipanga kuyazuia.

..Tatizo Polisi walishindwa kuzuia umati usijipenyeze kuingia UWANJA WA NDEGE.

..Baada ya hapo Polisi walibakia watazamaji tu.

..Wangekabiliana na umati ule kungeweza kutokea madhara makubwa.

Cc Tindo
 
Salaam wakuu,

Hivi majuzi kumetokea vurugu huko nchini Sri Lanka baada ya wananchi kutoka kila nyanja ya maisha kuingia ikulu ya Raisi na makazi ya Waziri Mkuu kuwataka kujiuzuru na hadi wakati huu bado wananchi wanaendelea kukalia makazi na ofisi hizo hadi pale viongozi hao watakapo jiuzuru.

Kwa picha ya kawaida tunaweza sema wale ni wananchi ndio waliofanya au wanaotaka kuitoa madarakani serikali ila ukweli ni kwamba nyuma ya pazia ni kuna mkono wa mfumo na idara za usalama au nguvu toka mataifa ya nje.Wengi mataifa ya Afrika wanajidanya kuwa hata wao kuna siku wanaweza fanaya kama walivyo fanya wananchi wa Sri Lanka ukweli ni kwamba kamwe haiwezi tokea.

NB: Ukiona Raisi anapinduliwa au anauliwaa ujue kuna mkono wa idara a usalama au mataifa ya nje.
Sri lanka ni moja ya nchi zinazozalisha mpira (rubber) kwa wingi, inaezekana akina makampuni makubwa ya matairi ndo wanadhamini pambano
 
Salaam wakuu,

Hivi majuzi kumetokea vurugu huko nchini Sri Lanka baada ya wananchi kutoka kila nyanja ya maisha kuingia ikulu ya Raisi na makazi ya Waziri Mkuu kuwataka kujiuzuru na hadi wakati huu bado wananchi wanaendelea kukalia makazi na ofisi hizo hadi pale viongozi hao watakapo jiuzuru.

Kwa picha ya kawaida tunaweza sema wale ni wananchi ndio waliofanya au wanaotaka kuitoa madarakani serikali ila ukweli ni kwamba nyuma ya pazia ni kuna mkono wa mfumo na idara za usalama au nguvu toka mataifa ya nje.Wengi mataifa ya Afrika wanajidanya kuwa hata wao kuna siku wanaweza fanaya kama walivyo fanya wananchi wa Sri Lanka ukweli ni kwamba kamwe haiwezi tokea.

NB:
Ukiona Raisi anapinduliwa au anauliwaa ujue kuna mkono wa idara a usalama au mataifa ya nje.
Kwa maelezo yako una maana Africa hayo au hao wenye mkono hawawezi jitokeza? Mapinduzi ya aina ile yanaweza kutokea popote. Ogopa watu wakifika mahali na kuona kifo ni bora kuliko kuishi.
 
Mkuu hapa kwetu Afrika ni ngumu kutokea, unafikiri vyombo vya usalama hawakupata fununu kuwa kuna watu wanatarajia kupindua serikali? kwanin waliamua kukaa kimya? hapo kuna baraka zote toka idara za ndani za usalama na mataifa ya nje na ndio maana unaambiwa NAVY FORCE ndio wanaompa hifadhi huku hawana mpango wa kumrudisha madarakani.
 
Ndoto za vijana wa vijiweni wengi wenye sifa kama za upande nisiopenda kuutaja hapa wana mawazo finyu kuhusu utawala, mambo yanatofautiana kwa mbaaali sana wanayotaka kulinganisha,

ilikuwa rahisi Kumpindua Nyerere, Mkapa na Magufuli lakini siyo Mwinyi, Kikwete wala Samia, japo na nilio wataja waliokuwa rahisi kupinduliwa ni kwa sababu ya Loss of political ventilation ,,,, NAO ISINGEKUWA RAHISI KWA ASILIMIA ZAIDI YA 50 Maana hatujafika wafanya hivo hatua waliyofikia,,,

mode ya kulinda usalama ni tofauti namsifu samia Kila wilaya wapo watu 1260 politely ambao wapo na shughuli zao za kawaida ila wakifanya kazi ya serikali kwa weledi na wengine hawajuani,,

Mpango mwingine ni wa kuweka vituo bubu vya usalama kila mita 500 ndani ya majiji na miji pia kuweka nyumba kadhaa kusiko na miji zikifanya shughuli nyingine tofauti kumbe ni,,,,,,, mama Huyu kaweza hapo ....

Britanicca
Acha kujidanyangay wewe mkuuu kumbe na wewe unawaza ki popoma?
 
Back
Top Bottom