Pre GE2025 Tundu Lissu: Abdul (mtoto wa Rais Samia) alitaka tukutane kwenye hoteli moja Masaki anihonge, nikamwambia njoo kwangu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Abdul anatuhumiwa kwa kugawa rushwa mama yake Yuko kimya

Haya ndo mambo huangusha watawala natawala
 

..Video clip uliyowasilisha inatakiwa kuwekwa ktk post ya kwanza kwa uzi huu.
 
Okay
 
Kwa mamaye. Niulize mamaye anatoa wapi hayo mabulungutu ya hela? Jibu: anaiba kwa watanzania.
 
Mbona mnanichanganya nyie wanasiasa au kila mda mna edit kutokana na wafuasi wanataka kusikia nini
Sebuleni walipeleka hongo au kupokea document aaaghhh
 
Yaani Alikataa pesa za Abduli Ila akampa document Abdul huyo huyo amsaidie kupata pesa?
 
Washatuona mafala sana hawa. LIssu nae anajikanyaga sana

Ngoja wakafie mbele
 
Yaani Alikataa pesa za Abduli Ila akampa document Abdul huyo huyo amsaidie kupata pesa?
Kwa maelezo yake, hakutaka kupokea pesa zisizo na utaratibu - ambayo kimsingi ni rushwa, adui wa haki. Alitaka pesa yake halali kupitia mfumo unaoeleweka.

Mbona hii taarifa imeshafafanuliwa mara elfu? Jifunzeni kuchunguza mambo wenyewe, msingoje kutafuniwa kila kitu.
 
Huyo Abdul ni zuzu?
Tatizo ni kwamba Lissu alisema Abdul aliletwa na Wenje kumhonga ili aache kumsumbua mama yake. Hii clip inaendana kabisa na simulizi za Wenje na Yericko. Lakini bado kuna watu watamtetea.

Amandla...
 
Simulizi zake za awali ni kuwa Abduli alitaka kumhonga. Na alimuonyesha wengine waliokuwa tayari wamekubali. Na hizo taarifa alipeleka kwenye kikao cha Kamati Kuu.

Amandla...
 
Back bencher huyo huwa hawaelew haraka.
 
Sema mwana anaropoka sana!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…