Pre GE2025 Tundu Lissu achukua rasmi Fomu ya kugombea Uenyekiti CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kila laheri Lissu...
 
Kitengo cha Kusifia Lumumba Matatani...likiki zimesambaratishwa na Kishindo cha Chadema
 
Hii ndiyo maana ya demokrasia siyo wale w fomu moja
 
CHADEMA chini ya Mbowe ni chama rafiki wa CCM. Mwenyekiti wetu alishapewa tuzo na CHADEMA

Zinakuja siasa za upinzani sasa, yani inakua kama Republican na Democratic ndo maana maccm yanahaha, anyway wajifunze kuzoea tu sasa maana huyu jamaa hasimamishwi na vitisho, majungu, pesa wana mashujaa wa mitandaoni!
 
ngoja tusubiri
Nimependa utulivu wako. Hekima yako. Kuna mambo magumu kama haya ambayo yanahitaji hekima na busara. Hata kama unapendeleo lako linabaki moyoni mwako na huku nje sisi tunakuona uko neutral na kuona lolote litakalotokea ni sawa kwako kulingana na nafasi yako na ushawishi wako ktk chama.
Wengine wamevurunda humu na kuwashambulia wagombea. Na wanajiweka ktk wakati mgumu kama huyo waliyemshambulia atashinda uchaguzi.

Kutoka moyoni nakupongeza sana.
 
Sisiemu wamepotezwa ni vumbiii tu .Chama cha WATANZANIA kipo KAZINI...Chadema kuweni na hurumaa hapa Lumumba njaa ime ngia kama mlipuko wa KIPINDUPINDU kisa nyinyi kutawala MEDIA!!!!
Huko chadema kuna akili nyingi sana zipo huko watu wazungukwa hawaelewi kipi ni kipi wapo wapo tu
 
uko sahihi boss,

yule Boni egg na Nyerere sijui watajificha wapi. kumbe ndio maana kwenye maisha ya duniani kuna wakati ka-unafiki kanakuwa applicable
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amechukua fomu kugombea nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho huku akiwajibu watu wanaokosoa uamuzi wake na kusema jambo hilo si la ajabu na kuwahoji walitaka achukue nani.

Akizungumza jana asubuhi nyumbani kwake Tegeta, Dar es Salaam, kabla ya kwenda kuchukua fomu, Lissu alisema siyo ajabu yeye kugombea nafasi hiyo na wala kupambana na mwenyekiti wake (Mbowe).

Katika mahojiano hayo na kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, Lissu alisema kitu ambacho watu wanakiona cha ajabu ni yeye kuwa Makamu Mwenyekiti na kutangaza kuchukua fomu ya uenyekiti CHADEMA.

“Sasa mlitaka achukue nani kama siyo Makamu Mwenyekiti? Nani ndiye aliyeandikiwa kuchukua na nani asichukue? Kinachoonekana cha ajabu ni hicho tu,” alisema.
 
Harafu ukiwa Makamu si ndio uko karibu kuwa mwenyekiti?
 
Kwa mwanachama anayekipenda Chama na mwenye akili timamu Tundu Lissu ndiye anayefaa kukiongoza CHADEMA. Mtu mmoja anawezaje kuendelea kuwa Mwenyekiti kwa zaidi miaka 20. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA msije mkarubuniwa na rushwa wakati wa uchaguzi. Fanyeni uamuzi ulio sahihi ili kukinusuru Chama.
 
Angalau wewe sasa ndo akili inaanza kukurudia. Hiki ndicho kitu wapenzi wa Lissu wanapaswa kufanya na sio kumtukana Mbowe na kususa kisa kagombea.

Lissu alitangaza nia ya kugombea uenyekiti sio kurithishwa uenyekiti. Ni muda sasa kuelekeza nguvu kwenye ushindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…