Tundu Lissu afanya Mahojiano na Voice Of America (VOA)

Tundu Lissu afanya Mahojiano na Voice Of America (VOA)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mh Tundu Lissu amefanya Mahojiano Muhimu sana na VOA , ambapo amefafanua masuala mbali mbali ya namna hali ya kisiasa ya nchini Tanzania ilivyo kwa sasa (Tutajaribu kuweka video ikiwezekana)

Lissu ambaye yuko Marekani kwa ziara ya kikazi , hasa kuhusiana na masuala ya kisiasa na kidemokrasia anahitajiwa na Vyombo karibu vyote vikubwa vya Marekani kwa ajili ya Mahojiano , Sisi tayari tunaye mwakilishi kwenye ziara yake hiyo na tutajitahidi kuweka video za mahojiano yake yote hapa hapa JF kwa ajili ya faida ya wadau , Endelea kututegea sikio .

Mh._Tundu_%0ALissu__Akifanya_mahojiano_na_kituo_cha_Voice_Of_America_VOA..jpg


 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mh Tundu Lissu amefanya Mahojiano Muhimu sana na VOA , ambapo amefafanua masuala mbali mbali ya namna hali ya kisiasa ya nchini Tanzania ilivyo kwa sasa (Tutajaribu kuweka video ikiwezekana)....
Tupia video, twende sawa
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mh Tundu Lissu amefanya Mahojiano Muhimu sana na VOA , ambapo amefafanua masuala mbali mbali ya namna hali ya kisiasa ya nchini Tanzania ilivyo kwa sasa (Tutajaribu kuweka video ikiwezekana)...
Bado kuna vyombo vya habari vina muda wa kupoteza na Lissu really?
 
Siasa za Tanzania upande wa Chadema zimebadilika, hii hali wanayoipitia hivi sasa wakabiliane nayo kwa werevu ili wathibitishe ukomavu wao.

Ni kama vile CCM na polisi wameamua kuwavuruga viongozi wa Chadema ili kuwatawanya wanachama wao, piga kiongozi ili waliobaki wakose uelekeo, na shughuli za chama chao zipoe.

Kumsubiri Samia awaruhusu Lissu na Lema warejee nchini wakati akijua fika huko kutakuwa ni sawa na kuiimarisha Chadema linaweza kuwa suala gumu, asisubiriwe, mapambano yaendelee.

Muhimu viongozi waliopo washirikiane na waliopo nje kupanga mikakati mipya namna ya kufanya siasa, namna ya kuimarisha chama, wananchi wasiachwe walale sababu Mbowe yupo gerezani, madai ya Katiba Mpya yaendelezwe hata kama polisi wanaendelea kukamata wanachama kila kukicha.
 
Back
Top Bottom