"Tofauti ya Mrema, Slaa na Lowassa ni 'organization' wakati wa nyuma hakukuwa na 'organization' ila sasa tunayo, tunaweza kuweka mawakala nchi nzima"- @TunduALissu
#“Kutakua na Uhuru kamili wa vyombo vya Habari, katiba yetu haina neno ISIPOKUA, kutakua na Uhuru wa maoni, kutakua na Uhuru wa kutafuta habari, kumekua na ukiukwaji mkubwa wa Uhuru wa Habari, miaka mitano ya Magufuli imekua migumu kwa vyombo vya Habari”.@TunduALissu #Mwanza.
“Kumbe wakati mwingine polisi wanafanya kazi zao kwa weledi lkn wanakuwa victimized wanapokataa maagizo toka juu”. Tundu Lissu.
"Kuna vitu havihitaji utoe pesa ili upate pesa, kuna sehemu unahitaji akili tu"- @TunduALissu.
"Serikali yangu itakuwa na 'complete freedom' ili ku-stimulate uchumi mzima, ukishusha vifaa vya ujenzi watu wataweza kujenga nyumba zilizo bora"- Lissu.
===
Katika Mdahalo huo waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wameuliza maswali mbalimbali ikiwamo namna gani atakavyouondoa ukoloni mambo leo? Umuhimu wa watu wengi kujaa kwenye mikutano, na auala la yeye kutumika na mabeberu.
Aidha alipoulizwa kuhusu serikali yake itapambana vipi kuundoa ukoloni mamboleo Lissu amefafanua kuwa suala la ukoloni mambo leo ni dhana iliyokuwa inabebwa zaidi na viongozi ambao walikuwa wanatawala kwa kufuata mfumo wa kijamaa ila kwa wakati huu dhana hii haipo tena maana hawa tunaowaita wakoloni mambo leo ndio ambao wamekuwa wakitusaidia na tukiwategemea katika kufadhili miradi mbalimbali.
Ameongeza kuwa hao tunaowaita mabeberu ndio wanatusaidia katika kila kitu hata katika vyombo vya usalama kama Polisi n.k. Pia wanatusaidia katika usafiri kama wa ndege na helikopta na wanatusaidia katika kutoa hela za miradi mikubwa mikubwa. Ameeleza kuwa ikitokea watu hao wametuzuia kidogo tu, tumekwisha. Hivyo amesisitiza kuwa watu waache kudanganyika na neno mabeberu na ukoloni mambo leo tutengeneze mahusiano mema na Dunia, kwa sababu dunia haitutegemei sisi isipokuwa sisi tunaitegemea dunia.
Sambamba na hilo, Tundu Lissu ameeleza nchi hii imeharibu uhusiano na nchi nyingine ndani ya miaka mitano iliyopita. Hivyo, wakipata ridhaa ya kuiongoza nchi watahakikisha wanajenga mahusiano mazuri na mataifa mengine ili kuleta maendeleo nchini.
Aidha, akijibu swali kwamba serikali yake itapata wapi pesa za fidia kuwalipa wakazi waliobomolewa nyumba zao, Tundu Lissu amefafanua kuwa kwa sheria ya nchi inasema kuwa pale serikali inapokosea au kubomoa nyumba za watu kimakosa inweza kushitakiwa na kulipa fidia. Hivyo, ukikosewa kwa namna yoyote ile na serikali unastahili kulipwa fidia. Hivyo, kwa namna yoyote Tundu Lissu amesema wakipata nafasi ya kuingia madarakani watatafuta namna ya kuwalipa fidia. Amesisitiza kuwa japo itakuwa bili kubwa ya kulipa fidia lakini itawalazimu watafute pesa hiyo ya kulipa watu fidia.
Aidha, kuhusu suala la watu kujaa kwenye mikutano, Lissu anasema kuwa katika siasa mtaji ni watu, ili kubaini kuwa Mwanasiasa ana nguvu kiasi gani kisiasa lazima uangalie anaungwa na watu kiasi gani. Ameweka bayana kuwa Chadema ya mwaka huu imejipanga zaidi na wana matawi mengi na kutengeneza Organization ya Chama inaitwa Chadema ni Mshindi.
Ama kuhusu uhuru wa vyombo vya habari, Tundu Lissu amesema kuwa serikali ya Chadema itavipa uhuru vyombo vyote vya habari na wataondoa vikwazo vyote mamlaka kama TCRA zitatumika kusajili tu vyombo na sio kuingilia maudhui yao.