PreGE2025 Tundu Lissu ahojiwa kwa makosa ya uhaini na kutoa taarifa za uongo, agoma kutoa maelezo Polisi

PreGE2025 Tundu Lissu ahojiwa kwa makosa ya uhaini na kutoa taarifa za uongo, agoma kutoa maelezo Polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ikiwa Nyerere aliwahi kutuhumiwa kwa kosa la Uhaini wewe ni nani mpaka uogope?? Mandela aliitwa mpaka Gaidi leo hii amelala kaburini Heshima yake itadumu milele zote!! waoga hudhani kukamata watu kuwatesa ni tiba hilo sio kweli.
 
Inadaiwa leo Aprili 10, 2025, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mwanasheria Tundu Lissu amehojiwa kwenye na Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa makosa mawili ya Uhaini na kutoa taarifa za Uongo. Inadaiwa pia Lissu hajatoa maelezo yoyote isipokuwa taarifa zake binafsi pekee.

Pia soma: Pre GE2025 - John Heche: Nimepata taarifa za kuaminika kuhusu mpango wa kumkamata Tundu Lissu kwa Kumbambikia Kesi ya Uhaini

View attachment 3298983
Muhaini ni yule anaepora pesa zetu na kuhonga wasanii yeye na mwanae...maza kwa ground hali yake mahamumu bila kuwatumia policeccm na tissccm hawawezi kutoboa hata ujumbe wa mtaa...ndio shida ya kutawaliwa na watu wenye diploma
 
CCM wasitumie dola wakubali kurekebisha Sheria ya uchaguzi waone kama lissu atasumbua!
Hicho chama bila policeccm na Tissccm hawana uwezo wa kupata hata kura laki 5...shida hiko chama kimejaa watu wasiokua na uwezo zaidi ya kufisadi na kuchezea pesa za serikali kuwalioa wasanii uchwara
 
Kwa namna ile ile ambavyo Yesu Kristo alivyogoma kumjibu Pirato baada ya kushitakiwa kwa makosa ya Uongo! Ndivyo alivyofanya Lissu.
Wampeleke sasa Mahakamani wakaone moto wake.
 
Tuandae wimbo kata zote Tanzania


Tuandae siku maalum saa na kuimba nyimbo. Hata wakija na mabomu tutasogea na kuimba nyimbo tuone watauawa wangapi?

Huo ni moja ya mikakati inayotakiwa kuchukuliwa kwa haraka na umma mpana (people's power) kuonesha kuchukizwa na vitendo vya watawala...
 
Inadaiwa leo Aprili 10, 2025, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mwanasheria Tundu Lissu amehojiwa kwenye na Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa makosa mawili ya Uhaini na kutoa taarifa za Uongo. Inadaiwa pia Lissu hajatoa maelezo yoyote isipokuwa taarifa zake binafsi pekee.

Pia soma: Pre GE2025 - John Heche: Nimepata taarifa za kuaminika kuhusu mpango wa kumkamata Tundu Lissu kwa Kumbambikia Kesi ya Uhaini

View attachment 3298983
Wameanza mapema sana, Kwa hali hii hata kampenni hazijaanza wanaanza kunyamazisha wapinzani!!
 
images (1).jpeg
 
Vipi keyboard warriors mbona kimya?Yaani uzungumzie uasi uachwe tu?
 
Kwenye uhaini ,itakuwa mara ya pili ,enzi za mkapa lisu alishitakiwa kwa kosa Hilo

Polisi wa kutoa ushahidi ajiandae presha anatakiwa kupima kilasiku
 
Leo Aprili 10, 2025, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mwanasheria Tundu Lissu amehojiwa kwenye na Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa makosa mawili ya Uhaini na kutoa taarifa za Uongo. Inadaiwa pia Lissu hajatoa maelezo yoyote isipokuwa taarifa zake binafsi pekee.

Pia soma: Pre GE2025 - John Heche: Nimepata taarifa za kuaminika kuhusu mpango wa kumkamata Tundu Lissu kwa Kumbambikia Kesi ya Uhaini

View attachment 3298983
Kengekweli nyie ,mpeni hadhi yake ya mwenyekiti chadema taifa sio kumwita TU ,mwenyekiti
 
Back
Top Bottom