Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Mgombea Urais wa Chadema katika uchaguzi mkuu ujao mwishoni mwa mwaka huu, Tundu Lissu, ametoa madai mazito mjini Njombe jana katika ziara zake za kutafuta wadhamini, akimuhususisha Rais, kuhusu jaribio la kuuawa kwake, lililofanyika September 7 mwaka 2017.Akihutubia umati wa wananchi, alikumbushia historia ya tukio lake la kumiminiwa risasi, ambapo aliponea chupuchupu kuuawa na kukimbizwa nchi za nje kwa matibabu.
Akisimulia mkasa huo alieleza kuwa kuna "connection" kati ya hotuba aliyoitoa Rais Magufuli, ya uzinduzi wa ripoti ya tume ya madini, masaa takribani mawili, kabla ya kupigwa kwake risasi, aliyotoa akiwa Ikulu, jijini Dar-es-Salaam.
Aliendelea kueleza kuwa katika hotuba hiyo aliyotoa Rais Magufuli, ambayo alidai ipo ndani ya YouTube, alimnukuu Rais akiyatamka maneno yafuatayo "Katika mapambano ya kijeshi, huwa wana kawaida ya kumwua, askari yeyote ambaye anawasiliti katika mapambano yao, vile vile katika vita ya kiuchumi ambayo nchi yetu inapigana hivi sasa, hatuwezi kuruhusu ku-survive kwa mtu mmoja, ambaye imebainika amekuwa akiwasiliana na mwanasheria wa kampuni hiyo ya madini, Deo Mwanyika, ili kumwibia taarifa mbalimbali nyeti, katika lengo lao wakishirikiana na mabeberu kutoka nje ya nchi, katika kutuhujumu malipo yetu ya madini, huyo mtu hastahili kabisa ku-survive" mwisho wa kunukuu.
Tunajua kuwa katika tukio hilo la kupigwa kwake risasi mwaka 2017, Tundu Lissu, Jeshi la Polisi limekuwa likutaaminisha kuwa uchunguzi wa tukio hilo unakwamishwa na Tundu Lissu, muhanga mkubwa wa tukio hilo, pamoja na Dereva wake, ambao wote walikuwa wameenda nchi za nje kwa matibabu.
Hivi sasa Tundu Lissu amesharudi nchini na amewapa "hints" ya kilichompata siku ile ya kutisha sana, ambapo "watu wasiojulikana" walimpiga risasi mfululizo 16 mwlini mwake katika jaribio la kutaka kumwua na ameeleza mwenyewe nini kilimtokea siku ile, ambapo Jeshi letu la Polisi, limekuwa likidai kuwa limekwamishwa kuendelea na uchunguzi wake, kutokana na kukosekana ushahidi huo wa Tundu Lissu
Kwa hiyo nadhani Jeshi la Polisi lingeanza kufanyia uchunguzi wa tukio lile sasa, kwa "hints" alizozitoa yeye mwenyewe muathirika wa tukio lile Tundu Lissu.