Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

Tunataka sera atasaidiaje wakulima, machinga, wasomi, wajiriwa,viwanda,uchumi,siasa ,elimu ,aachane na mambo ya risasi
 
Hayo maneno ya Rais aliyarudia hata kule manyara kwenye uzinduzi wa ukuta wa mererani baada ya lisu kushambuliwa kuwa " wamasai eti kama mtu anakuibia ng'ombe wako alafu jirani yako anakucheka huyo mtu utataka aishi karibu yako?
 
Sijawahi kusikia serikali yenye wahalifu wapumbavu kama Tanzania. Inawezekana Magufuli alikuwa hajui kinachpkwenda kutokea, lakini wahuni wakachomeka kwenye hotuba yake ili aonekane alikuwa anajua shambulizi lile na hivi hata yeye uwezo wa kuchuja maneno ni below 0, basi akalipuka nalo.
Kwa nn alinyimwa matibabu na stahiki zake kama mbunge na hatimaye kuvuliwa Ubunge
 
Mgombea Urais wa Chadema katika uchaguzi mkuu ujao mwishoni mwa mwaka huu, ametoa madai mazito mjini Njombe jana katika ziara zake za kutafuta wadhamini, akimuhususisha Rais, kuhusu jaribio la kuuawa kwake, lililofanyika September 7 mwaka 2017

Akihutubia umati wa wananchi, alikumbushia historia ya tukio lake la kumiminiwa risasi, ambapo aliponea chupuchupu kuuawa na kukimbizwa nchi za nje kwa matibabu.

Akisimulia mkasa huo alieleza kuwa kuna "connection" kati ya hotuba aliyoitoa Rais Magufuli, ya uzinduzi wa ripoti ya tume ya madini, masaa takribani mawili, kabla ya kupigwa kwake risasi, aliyotoa akiwa Ikulu, jijini Dar-es-Salaam.

Aliendelea kueleza kuwa katika hotuba hiyo aliyotoa Rais Magufuli, ambayo alidai ipo ndani ya YouTube, alimnukuu Rais akiyatamka maneno yafuatayo "Katika mapambano ya kijeshi, huwa wana kawaida ya kumwua, askari yeyote ambaye anawasiliti katika mapambano yao, vile vile katika vita ya kiuchumi ambayo nchi yetu inapigana hivi sasa, hatuwezi kuruhusu ku-survive kwa mtu mmoja, ambaye imebainika amekuwa akiwasiliana mwanasheria wa kampuni hiyo ya madini, Deo Mwanyika, ili kumwibia taarifa mbalimbali nyeti, katika lengo lao wakishirikana na mabeberu katika kutuhujumu malipo yetu ya madini, hastahili kabisa ku-survive" mwisho wa kunukuu.

Tunajua kuwa katika tukio hilo la kupigwa kwake risasi mwaka 2017, Tundu Lissu, Jeshi la Polsi limekuwa likutaaminisha kuwa uchunguzi wa tukio hilo unakwamishwa na Tundu Lissu, muhanga mkubwa wa tukio hilo, pamoja na Dereva wake, ambao wote walikuwa wameenda nchi za nje kwa matibabu.

Hivi sasa Tundu Lissu amesharudi nchini na amewapa "hints" ya kilichompata siku ile ya kutisha sana, ambapo "watu wasiojulikana" walimpiga risasi mfululizo 16 mwlini mwake katika jaribio la kutaka kumwua na ameeleza mwenyewe nini kilimtokea siku ile, ambapo Jeshi letu la Polisi, limekuwa likidai kuwa limekwamishwa kuendelea na uchunguzi wake, kutokana na kukosekana ushahidi huo wa Tundu Lissu

Kwa hiyo nadhani Jeshi la Polisi lingeanza kufanyia uchunguzi wa tukio lile sasa, kwa "hints" alizozitoa yeye mwenyewe muathirika wa tukio lile Tundu Lissu.
Ohooo.. mie simo!
 
Kwa nn alinyimwa matibabu na stahiki zake kama mbunge na hatimaye kuvuliwa Ubunge
Maoni yangu ni kwamba huyu jamaa anaweza kuwa hakujua chochote, lakini kwa vile ni mtu wa visasi akakubali hata mambo ambayo yanamchonganisha na jamii.
 
Kwa ni uongo si kweli alikuwa anakwamisha juhudi za vita vya kiuchumi kwa jina la makanikia ambavyoTaifa lilikuwa likipambana na wale wezi wa madini. Kwani ni uongo kuwa alikuwa msaliti akitaka kukwamisha vita hiyo. Ajitafakari kaacha tabia yake ya usaliti na uasi au anaiendeleza kwa style nyingine?
 
hatuwezi kuruhusu ku-survive kwa mtu mmoja, ambaye imebainika amekuwa akiwasiliana mwanasheria wa kampuni hiyo ya madini, Deo Mwanyika, ili kumwibia taarifa mbalimbali nyeti
Huyo Deo Mwanyika wa Barrick Gold aliyesema anavujisha siri za nchi kwa Tundu Lissu na kumfunga detention miaka kadhaa na kisha kumwachia I hope sio huyo huyo waliyempitisha leo kuwa mgombea ubunge wa CCM Njombe Mjini.

Ni yeye ???
 
Ndiyo hivyo tena...........

Huyo Tundu Lissu ana "guts" hadi anadiriki kutoa tuhuma nzito kiasi hicho kwa mkuu wa nchi!........

Amewaachia mpira huo waucheze Jeshi letu la Polisi, waliokuwa wanadai kwa muda mrefu kuwa uchunguzi wao utaendelea pale Tundu Lissu atakaporejea nchini na ndiyo hivyo kesharejea na ameamua kuyaweka hadharani mambo yote yaliyomtokea!
Polisi wameshaweka mpira kwapani ndio maana wapo kimya mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom