Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

Mkuu tuelewane vizuri, naamini hakuna mtu (hata awe mpinzani wa Magu) atakataa kuwa tukidhibiti wizi wa rasilimali zetu (ikiwemo madini) wote tutanufaika.

Na alipoanza hiyo move hata wapinzani walionesha kumsapoti na ndio maana wakajitokeza kutoa maoni (Lissu na Zitto wakiwemo) kuhusu namna nzuri ya kulinda, kudai na kutetea rasilimali zetu.

Kinyume chake akawageuka na kujibinafsishia ule mchakato (sijui kwa nia njema au mbaya) na kuanza kuwaita wengine wasaliti. Ilibidi watu waanze kuhoji kama ana nia njema kwa nini hataki ushauri wa wengine kisa tu ni wapinzani wake kisiasa?

Akaanza kupiga vijembe kwenye press na mikutano yake na kuwaita wengine vibaraka wa mabeberu, ndipo nao wakatoka mbele ya umma kueleza kuwa anachokifanya kitaligharimu taifa na hatutafanikiwa badala yake tutaingia hasara zaidi.

Ndipo hapo issue ya kina Lissu kuomba taarifa Barrick ili wauoneshe umma kile kilichoingiwa kwenye mikataba kati ya serikali na Barrick ili waujue ukweli.

Kinyume chake Magu akatoka tena kusema hawa anaowaita wasaliti wanapeleka siri za nchi kwa Barrick. Sasa unajiuliza ni siri ipi inayozungumzwa wakati ni vitu vilivyo kwenye mikataba?

Miaka mitatu leo, kuna mtu anaweza bisha kuhusu ushauri aliotoa Lissu?
Kwamba hakuna tutakacholipwa, makinikia yataondoka bure, tutashitakiwa na tutaliingiza taifa kwenye mgogoro na wawekezaji?

Hadi leo migodi imesitisha uzalishaji, watu wamepoteza ajira, serikali inakosa mapato (hata yale kiduchu), wawekezaji wanaiogopa Tz, taswira yetu kimataifa imeharibika.

Na kibaya watu wanaangalia tu migodi ya Barrick, mkuu kuna mgodi wa Shanta mining mkubwa pale Ikungi kwenye jimbo la Lissu hadi leo jamaa hawajaufungua kutokana na sera za awamu hii. Jamaa wameuweka under maintainance hadi watakapo jiridhisha ni safe kwao wataweka pesa zao waanze kuzalisha. Tunakosa mapato, ajira na mzunguko wa fedha kwa sababu za hovyo kisa ubabe wa mtu mmoja asiyetaka kushauriwa.
U
 
Mabeberu ndio waliong'oa CCtv camera na kuondoa walinzi eneo la tukio?
Ninyi kutwa kuchwa na mawio si mnasema hao jamaa hawashindwi kitu? Mbona sana kama unadharau uwezo wa 'mabeberu! ?
Ha ha haaa! Hamfurukuti ...this time. Ha ha haaa!
 
Lisu kama alikuwa anafanya hivyo alistahili alichopata!

Nilitoa maoni humu kwamba, huenda Lisu zile harakati zake za toka miaka ya 90 kupigania madini zilikuwa zinamnufaisha yeye binafsi ndio maana alipoona Jpm yuko serious akaamua sasa ageuke kinyonga.

Kuhusi hao waliosaini mikataba, hao tunawasamehe maana walikuwa enzi na akili za kimangungo!

Lakini haka kajamaa haka kako kizazi cha wasomi kumbe kana uza nchi live?
Acha uzwazwa, waliotia hasara nchi unawasamehe, halafu anaetetea maslahi ya nchi unamuadhibu, hivi nyie mnao muabudu jiwe akili zenu ni matope?
 
Kwahiyo T. Lisu amekiri hadharani kuwa yeye ndio msaliti wa nchi hii? Au nimeelewa vibaya.




MAGUFULI4LIFE.

Suppose uwe hujàelewa vibaya, yaani uwe umeelewa kwa usahihi kabisa....

Na suppose kuwa, Tundu Lissu ni msaliti wa nchi....

MASWALI HAYA NI MUHIMU SANA:

å Rais Magufuli anapata wapi uhalali wa kuamuru RAIA wake auwawe kinyume cha sheria kwa tuhuma za juu juu tu za eti "msaliti wa nchi???"

å Sheria zetu za nchi zinasemaje kuhusu hiki "the so called" - USALITI WA NCHI? Je, zinasema Rais ataamuru na kutuma kundi la majambazi akiwa amewapa na pesa na bunduki kumuua huyo mtu ambaye kwa vigezo vyake Rais amempa jina la "msaliti wa nchi??"

NI HIVI NDUGU YANGU;

• Kama yeye mwenyewe Rais Magufuli atajitokeza na kujitetea kwa hoja hii, basi atakuwa "mjinga" sana na kamwe hawezi kuchomoka kuepuka kifungo cha maisha gerezani....!!

• Na vivyo hivyo, kama wafuasi wake mnamtetea kwa hoja hii ya "kijinga" kabisa, basi hamtamsaidia kumwepusha na adhabu ya "kujaribu kuua kwa kukusudia" kamwe....!!

Kuwa Rais wa nchi ama kuwa na kinga ya "kutoshitakiwa" siyo ishu. Ukiua na wewe lazima uuwawe tu. Remember, KARMA IS A BITCH...!

USHAURI:

Magufuli ajitokeze hadharani na aweke sawa kauli yake.....

Ajitokeze na aseme, kauli yangu hiyo ilikuwa "just by coincidence", kwamba, nilisem vile na ikatokea siku hiyo hiyo niliyotamka Tundu Lissu akashambuliwa.....!!

Ila ukweli ni huu: kuwa, kauli yangu haikuwa ikim - refer Tundu Lissu kabisa. Na sikutoa amri yoyote auwawe....

Atoke sasa hadharani aseme hivyo japo ni hakika kuwa hakuna mtu timamu kiakili atamwelewa na kumwamini....

Else, asidhani kuwa MOYO WA DHAMBI YA UUAJI alionao HAUTAHUKUMIWA....

KINGA YA URAIS ya kutoshitakiwa haitamsadia. Natural justice haizuiwi na "kinga ya Rais kutoshitakiwa". Itapenya tu na lazima kila mtu alipie matendo ya dhambi zake....!!
 
Tatizo taratibu zipo lakini hutaki kuzirejea, matibabu ya nje ya nchi yana taratibu zake mbona hapo unakwepa kueleza? Kama unajiamulia kuondoka nchini kwenda kutibiwa nje ya nchi bila kufuata taratibu, gharamikia matibabu mwenyewe usitafute watu wa kulaumu kwa kulazimisha utaratibu usiokuwepo
Watu wenye akili kama za kuku ndo wanaambiwa taratibu hazikufuatwa na wanakubali na hata wanadiriki kuandika ujinga huo mtandaoni. Lakini wenye akili tunajua huo ni uongo ulio wazi kabisa. Kwani nani hajui kuwa Samwel Sitta alijipeleka mwenyewe kutibiwa huko Uulaya hadi aliposhindwa kumudu gharama gharama ndo akaomba serikali imsaidie ikafanya hivyo? Hakuwa na reference ya Muhimbili kama watu wanaokaririshwa wanavyodai. Kibaya zaidi huyu alikuwa ameshastaafu Uspika. Msituletee pumba zenu.
 
Kasome kuhusu Huria Mhiti katika msahafu wa Kikristu. Mmoja wa makomandoo 30 mahiri na watiifu kwa Mfalme Daudi, Huria mhiti. Alishindwa kuelewa, kutafsiti na kutii amri halali ya mfalme Daudi ili afiche aibu ya mfalme. Aliamriwa aende akalale nyumbani kwake ambapo mke wake alipewa ujauzito na mfalme Daudi Huria akiwa mstari wa mbele vitani.

Huria akafikiri kwenda kulala nyumbani kwake maana yake ni lazima ulale na mkeo. Na ilikuwa mwiko kwa wayahudi kushiriki tendo la ndoa wewe ukiwa askari mstari wa mbele wakati wa vita. Ilikuwa ni kulinajisi jeshi lote. Huria akakaidi amri ya Mfalme akalala getini na walinzi wa jumba la mfalme. Matokeo yake lengo la kwanza la mfalme kuficha aibu yake halikufanikiwa. Ikabidi mfalme atumie njia mbadala ambayo iligharimu maisha ya wanajeshi wengi mno na kikosi cha jeshi la Isreli kilichokuwa mstari wa mbele kikapata kichapo cha mbwa koko na Huria alikuwa mmoja wapo walio uwawa siku hiyo

Ndiposa tunasema mamlaka hizi zinazo tawala watu zimewekwa na Mungu. Daudi aliadhibiwa na Mungu mwenyewe kadiri alivyoona inafaa Daudi akatubu na matokea yake mwanae mwingine Daudi aliyempata na mke wa huyu mhanga yaani mama Huria akawa ni Mfalme Suleinani mtu ambaye alikuwa ni mwenye hikma haijawahi kutokea duniani na hatatokea. Na Bwana Yesu akawa ni mzao wa Daudi.

Hivyo to some of us wala hizo kelele za Lissu ambazo anapayuka hovyoo bila ya kutafuta hekima ya Mungu ni kazi bure na uharibifu mtupu kwake. Yeye angalimuliza Mungu wake kwa nini umenipitisha njia hii? Kuliko kuendelea kupayuka payuka bila utaratibu akifikiri atapa huruma kwa wanadamu. Huruma ya kweli unaipata kwa Mungu mwenyewe mh, Wala si hii unayoitaka ya kimaslahi zaidi labda eti utakuwa rais.

Mimi nitamuambia sababu ninazo ziona ambazo zote zimejengwa katika msingi wa tamaa zake zakujipatia kipato bila ya kujali ana kipata vipi. Wamedanganya watu wakaingia kupambana na vyombo vya dola na baadhi yao wakapoteza maisha na wengine wakawa vilema. Makaninikia usaliti wake ni ili apate fedha. Hivyo hivyo ukodishaji wa cdm kwa EL.
Rubbish, waliosaini mikataba yeye jiwe akiwemo ndani ya serikali, hakuwachukulia hatuayoyote, na alichosema lissu in kuwa tutashtakiwa, na kweli tunashtakiwa, na kusema ukweli lini no usaliti? Nyinyi wanafiku wakubwa wapenda madaraka ndio mlipiga majofi na kuwazomea wabunge waliokua wanapinga hii mikataba Leo mnajiita wazalendo!
 
Mtasema yote matapeli wakubwa nyie wa Watanzania. Kwa hiyo wao Lissu na Zitto walitaka wajipatie maslahi binafsi ikiwemo political mailage sio?! Na umesema vizuri na kuweka wazi kuwa wanajua kuna maslahi wanayapata katika mambo hayo. Wakafikiri wenzao watafaidi kama wao walivyokuwa wanafaidi hivyo pengine huko nyuma. Jawabu kwao likawa ni kuhujumu mchakato mzima sio. Hawa ndio baadhi ya viongozi wetu. Kazi ipo.
Mkuu, ukiacha hii nimeona comments zako huko juu pia, nahisi una tatizo la comprehension. Maana unapojibu hoja, mtu anaweza akahisi umemquote kimakosa.

Jifunze kusoma ili uelewe usisome ili ujibu.
 
Kwani wewe hukuwepo hapa Tanzania na ulikuwa husikii alivokuwa anapigwa vijembe. Ila jiulize kama ni kweli kwanini alikuwa hashitakiwi na wakati vyombo vyote vya dola viki chini yake ni wazi nia ilikuwa kumchafu kumbuka if you want to kill a dog give it a bad name

Mimi sijui lakini yeye Lissu ndio anatuambia kuwa yeye ndio alikuwa msaliti wa nchi yetu kwa mabeberu alikuwa ana tuuza!
 
Sijaelewa, kwahiyo anaomba kuchaguliwa sababu alipigwa risasi? Yeye ni wakwanza kupigwa risasi? Tumeshuhudia hadi askari wakipigwa risasi sembuse yeye? Atupe sera ataifanyia nn TZ sio blah blah.
muda Wa kampeni bado, ukifika atasema na kunadi Sera zao, kwa sasahivi fahamuni muuaji ni Nani!
 
Kisha tunamuona muuaji akipiga magoti madhabahuni kwa unyenyekevu fake. Mungu anadhihakiwa sana na wanasiasa wenye roho za kishetani

Kwani Lissu ana maanisha yeye ndio alikuwa msaliti na anadokoa siri zetu na kuziuza kwa mabeberu? Kwa hiyo Lisu kakubali alikuwa ana tusaliti?
 
Nyie mataahira huwa bado tu mnamuamini huyo Meko?

Huyo Deo Mwanyika ambaye alisemwa kutoa taarifa kwa Lissu na baadae kushtakiwa kwa makosa zaidi ya tisini yakiwemo ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha na baadae kuachiwa baada ya kulipa approximately 1.5b after plea burgain, jana kapitishwa kugombea ubunge huko Njombe kwa tiketi ya ccm.
Hivyo vituko utavipata Tanzania pekee!
 
Sasa kama alikuwa anasaliti mahakama si zipo na ushahidi mlikuwa nao kwanini hamkumshitaki kwa hilo kosa maana usaliti ni kosa la jinai. Hivi mtu una vyombo vyote vya ulinzi na usalama halafu unasema kuna mtu anaiba mali ya umma na tunayo mawasiliano ya ushahidi laki humkamati sisi wananchi tutamini hicho unachokisema kweli

Mkuu wewe unaniuliza mimi? Wewe una hakika gani kama msaliti aliyekuwa ana zungumziwa ni yeye? Naomba umuulize Lissu ana maanisha ni yeye alikuwa anaisaliti nchi yetu kwa mabeberu?
 
Tundu Lisu kaadhibiwa na Mungu, some punishment is just, na bado, ...
Ni Yesu sio Mungu, au ulimsikia vibaya Kangi Lugola! Ila pia inasemekana Yesu ni Mungu kwa upande mwingine uko sahihi.
 
View attachment 1543623
Mgombea Urais wa Chadema katika uchaguzi mkuu ujao mwishoni mwa mwaka huu, Tundu Lissu, ametoa madai mazito mjini Njombe jana katika ziara zake za kutafuta wadhamini, akimuhususisha Rais, kuhusu jaribio la kuuawa kwake, lililofanyika September 7 mwaka 2017.

Akihutubia umati wa wananchi, alikumbushia historia ya tukio lake la kumiminiwa risasi, ambapo aliponea chupuchupu kuuawa na kukimbizwa nchi za nje kwa matibabu.

Akisimulia mkasa huo alieleza kuwa kuna "connection" kati ya hotuba aliyoitoa Rais Magufuli, ya uzinduzi wa ripoti ya tume ya madini, masaa takribani mawili, kabla ya kupigwa kwake risasi, aliyotoa akiwa Ikulu, jijini Dar-es-Salaam.

Aliendelea kueleza kuwa katika hotuba hiyo aliyotoa Rais Magufuli, ambayo alidai ipo ndani ya YouTube, alimnukuu Rais akiyatamka maneno yafuatayo "Katika mapambano ya kijeshi, huwa wana kawaida ya kumwua, askari yeyote ambaye anawasiliti katika mapambano yao, vile vile katika vita ya kiuchumi ambayo nchi yetu inapigana hivi sasa, hatuwezi kuruhusu ku-survive kwa mtu mmoja, ambaye imebainika amekuwa akiwasiliana na mwanasheria wa kampuni hiyo ya madini, Deo Mwanyika, ili kumwibia taarifa mbalimbali nyeti, katika lengo lao wakishirikana na mabeberu kutoka nje ya nchi, katika kutuhujumu malipo yetu ya madini, huyo mtu hastahili kabisa ku-survive" mwisho wa kunukuu.

Tunajua kuwa katika tukio hilo la kupigwa kwake risasi mwaka 2017, Tundu Lissu, Jeshi la Polisi limekuwa likutaaminisha kuwa uchunguzi wa tukio hilo unakwamishwa na Tundu Lissu, muhanga mkubwa wa tukio hilo, pamoja na Dereva wake, ambao wote walikuwa wameenda nchi za nje kwa matibabu.

Hivi sasa Tundu Lissu amesharudi nchini na amewapa "hints" ya kilichompata siku ile ya kutisha sana, ambapo "watu wasiojulikana" walimpiga risasi mfululizo 16 mwlini mwake katika jaribio la kutaka kumwua na ameeleza mwenyewe nini kilimtokea siku ile, ambapo Jeshi letu la Polisi, limekuwa likidai kuwa limekwamishwa kuendelea na uchunguzi wake, kutokana na kukosekana ushahidi huo wa Tundu Lissu

Kwa hiyo nadhani Jeshi la Polisi lingeanza kufanyia uchunguzi wa tukio lile sasa, kwa "hints" alizozitoa yeye mwenyewe muathirika wa tukio lile Tundu Lissu.
Kama movie hivi
 
Hahhaha... Yeye ndio kawaambia watu kwamba Magufuli alimpiga risasi baada ya kuwa anasaliti nchi

Hukumu ya tuhuma ya "usaliti wa nchi" wa kubumba usiyo na uthibitisho kutoka kwa raia wa nchi unayoingoza ni kumpiga risasi kwa kutumia majambazi yaliyolipwa na kukingiwa kifua na serikali?

Kwa kutoa adhabu ya namna hiyo isiyojengwa ktk msingi wa kisheria, moja kwa moja inathibitisha kuwa hakuna kosa la "usaliti wa nchi" lililotendwa na yoyote....!!

Whether you like it or not, Magufuli si Rais. Huyu ni jambazi tu anayetumia mamlaka na nguvu ya "Urais" kulinda maslahi yake na majambazi menzie huko CCM....

Aliamua kutumia mamlaka yake ya Urais kumuua Lissu ili asiwe kikwazo cha wao kuendeleza ujambazi wao....!!

Tusidanganyane hapa. Watu tuna akili bwana. Tunaona na kupima kila lifanyikalo. Hatuwezi kuburuzwa na kudanganywa na wajinga wachache wanaodhani wao ni miungu fulani wenye nguvu fulani....
 
Mi nadhani hata kampeni zikianza mgombea wa ccm asije kujishughulisha kujibu hoja yoyote ya lissu maana naona kadri lissu anavomtuhumu akakosa response ni kama anazidi kujikuta anaropoka vitu vya ajabu ambavyo baadae vitamfanya akose majibu ya kuwapa watanzani watakapoamua kumuhoji maswali magumu kwenye majukwaa ya kampeni. Alianza kwa kujichanganya kwenye ishu ya corona leo anajichanganya kwenye ishu ya madini. Mwisho wa siku atajianika yeye ni mtu wa namna gani linapokuja suala la maslahi na uzalendo kwa nchi.
Ccm endeleeni kumpotezea msimjibu, ukimya wake utazidi kumfanya ajikaange
 
muda Wa kampeni bado, ukifika atasema na kunadi Sera zao, kwa sasahivi fahamuni muuaji ni Nani!
Msaliti yeyote kifo ni halali yake. Sio TZ tu, nchi yoyote ukizingua unawaishwa. Ila Lisu alipigwa na mabeberu.
 
Nyie mataahira huwa bado tu mnamuamini huyo Meko?

Huyo Deo Mwanyika ambaye alisemwa kutoa taarifa kwa Lissu na baadae kushtakiwa kwa makosa zaidi ya tisini yakiwemo ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha na baadae kuachiwa ka baada ya kulipa approximately 1.5b after plea burgain, jana kapitishwa kugombea ubunge huko Njombe kwa tiketi ya ccm.
Hakika kuanza sasa sitamuamini hata kidogo kwa lolote atakalosema Jiwe.......

Hivi pamoja na kumrundikia mashtaka yote yake ya uhujumu uchumi, yasiyopungia 90, Leo hii chama hiko cha CCM ndicho cha kumpa ridhaa Deo Mwanyika kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM??
 
Back
Top Bottom