Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

MFAN
O WA NCHI ULIOTOA URUSI YULE MPNZANI KAPEWA SUMU JE MBONA HAWAKUMKAMATA WAMSHITAKI KESI ISIKILIZWE?
 
Alichosema Lissu ndiyo ukweli mwenyewe.............

Na ametoa assignment kwa yeyote anayembishia, aitazame hiyo YouTube ya tarehe 7/09/2017
Hatuongei bila ushahid buddy nenda youtube sikiliza hotuba ya magu ya dakika 47 na sekunde 52 hakuna maneno lisu alilosema ambalo lipo kwenye hotuba ya magu ya tar 7/9 ..
Jamaa ni muongo na mchonganishi na atakipata anachokitafuta....
Magu hakutaja jina deo mwanyika kwenye hotuba yake...
Magu akusema they deserve not to survive..
Magu akutamka neno mabeberu kwenye hotuba yake
Magu akusema wanamawasiliano ya lisu akiongea na mwanyika
Mkuu mshaurini jamaa yenu awe na akiba ya maneno
 
Kwa tafasiri yako,Mimi nahusisha kauli iliyotolewa na Mtu fulani kuwa msaliti lazima auwawe.je adhabu ya msaliti inatolewa na Mtu sio Mahakama?
Comment yangu Ni kuwa lisu kakiri kuwa yeye Ni msaliti Ila anahusisha shambulio lake kuwa Ni hukumu ya(usaliti)wake na kwamba hakubaliani na hukumu hiyo(kushambuliwa)angepewa hukumu nyengine kwa maelezo yake Sasa nakuuliza wewe hukumu ya msaliti kwa taifa lake Ni Nini? Hebu nisaidie kidogo
 
Unamwamini huyu kiongozi wetu? Kwa taarifa yako, mambo mengi anayoyaongea huwa anayatengeneza kichwani mwake kwaajili ya kuwaokota watu wajinga.

Tundu Lisu hajawahi kuwa na mawasiliano na Acacia au kampuni yoyote ya madini. Deo Mwanyika hajawahi kuihujumu nchi hata mara moja. Hajawahi kutakatisha fedha. Ametolewa mahabusu kwa kulipiwa na kampuni ambayo Serikali ni mbia.

Kiongozi wetu amewahi kutoa tuhuma hadi dhidi ya watangulizi wake, Hayati Rais Mkapa na Rais mstaafu Kikwete kuhusiana na mikataba ya madini akiashiria kuwa walikubali mikataba mibaya kwa sababu ya kunufaika binafsi. Tuhuma ambazo nina uhakika wa 100% ni uwongo. Mkapa hajawahi kuhongwa na kampuni yoyote ya madini. Kikwete hajawahi kuhongwa hela yoyote kutoka kampuni yoyote ya madini. CCM wamewahi kuomba pesa na kupewa mara nyingi toka kwa makampuni ya madini licha ya kwamba sheria zetu zinayazuia makampuni kusaidia vyama vya siasa.

Kiongozi wetu huyu amewahi kuwadanganya watanzania kuwa tumeibiwa mabilioni ya dola kupitia makapuni ya madini. Amewahi kufadanganya kuwa makonteni ya makinikia yalikuwa 90% dhahabu. Kwa mwenye akili hata ya kwaida tu anajua ni uwongo. Container lenye 90% hakuna lorry la kuibeba, na hata hilo container wakati wa kunyanyuliwa tu litafumka kutokana na uzito, lakini wajinga waliamini.

Kiongozi wetu huwa anazungumza kwa mkazo sana, lakini uhalisia wa anachoongea huwa ni mdogo sana.

Kwa jinsi anavyowadanganya wasioelewa, mpaka unashindwa kuelewa hata kanisani kama huwa anaenda kweli kusali au huwa anaenda kufanya maigizo!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa hafai kua rais wa JMT. Labda chadema waanzishe cheo kipya cha rais wa mpe lissu lakini kwa JMT hawezi kabisaàaa.
Ungekuwa na akili ningekushauri kitu lakini hukujaaliwa akili, andamana na upumbavu uliojaaliwa hadi siku yako ya jehenam!
 

Point sio kweli au uongo. Kwani hatuna mifumo ya sheria ya kushughulika na watu kama hao!? Kama ndio kwanini haikutumika? Tukianza wote kuchukua sheria mkononi kuwa wa kutawaliwa hapo tena?
 
Bavicha kwa sound za kitoto hamjambo.. Hamna jipya mnaloweza kufanya ambalo haliwezi kuwa handled, vitisho peleka kwa wenzio vijiweni
 
aina ya uongozi wa lisu na sawa tu na wengine waliopita nothing will be changed mkuu.Kwanza chama chao hakiwezi kuleta maendeleo kwa watu mpaka wao watakapo jiweka sawa hilo lazima ujue.hawez leo kuingia ikulu aanze kukutazama ww lazima a take breath ya kula kwanza yy na kizazi chake ndo aje kwa raia.kule moshi hasa machame hakuna lolote alofanya mbowe tulimpokea kama mtu wetu tukajua atatuangalia lkin shida za maji barabara za mashuleni hakuwa tokea hat siku moja.leo anarud anataka tumpe kura mkuu.kila mtu anaumia kwa upande wake me nalia kwa mengi bora wakose tu hap chadema tumewapenda sana lkn kwa hili watuache
 
Acha porojo FBI wanaruhusiwa kuoperate Nje ya ardhi ya marekani ikiwa tu watakua wameruhusiwa nahio nchi husika
 
Wewe bwana Lisu kwa mdomi wake kasema alipigwa risasi kwa usaliti nadhani wewe sasa ni muda wa kwenda kumhoji sababu ya kusaliti nchi ya watu milion 50?

Kusema "kusaliti nchi ya watu milioni 50", bado haitoshi..

Hebu fungua kamusi ya kichwa chako kwanza....

Tafuta neno " usaliti" ama "msaliti" katika muktadha wa "nchi" au "taifa" kisha tupe maana yake...

Kisha jiulize swali hili la mwisho wewe mwenyewe sasa;

Did Tundu Lissu betray his own country? If the answer is YES, explain how he betrayed it...

Najua hutakuwa na jibu kwa sababu akili zenu LB7 hazifikiri ktk masafa haya...

NIKUELIMISHE KIDOGO:

Kosa la "usaliti wa nchi" kisheria ndilo linaloitwa "UHAINI"...

Anayehukumu kuwa hapa kuna kosa la UHAINI limetendeka, ni mahakama tu...!

Ni lini Tundu Lissu aliwahi kupelekwa mahakamani ni mahakama kumhukumu kuwa ni MHAINI?

Jibu ni: HAKUNA!

Ila katika hii iliyokuwa "Tanzania ya Magufuli" ya miaka mitano inayoisha Oktoba, 28; huyu Magufuli kichwa chake na mawazo yake ndiyo yalikuwa mlalamikaji, mwendesha mashtaka, shahidi na Hakimu/Jaji...

Tena hukumu za "Jaji/Hakimu Magufuli" ni za gizani na kwa kutumia Kundi maalumu la majambazi kufanya excursion ya hukumu hizo...

Hizi ni tabia za viongozi madikteta tu...

Nanyi wafuata upepo bila hata kufikiri, mnaimba na kushangilia tu kama mazuzu huku mkiimba na kushangilia vifo vyenu wenyewe na watoto wenu....

Poor you, Crimea...
 
Alichosema Lissu ndiyo ukweli wenyewe kwa asilimia 100.

Na ametoa assignment kwa yeyote anayembishia, aitazame hiyo YouTube ya tarehe 7/09/2017

Kwa hiyo Lissu ndio msaliti wa nchi alikuwa ana shirikiana na mabeberu..?
 

Sasa kwa hiyo Lissu sio aliyekuwa anaongelewa kwenye hotuba!
Kwani Lissu ndio msaliti? Ndio alikuwa anatumika na Mabeberu?
 
Kwenye mazungumzo mengine, nje ya ile hotuba, alimtaja na jina. Ukifika wakati yote yatakuwa mezani.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hahahahah alimtaja nani jina? Hata siku moja Rais hajawai taja jina la Lissu!

Swali Lissu amejuaje kama ni yeye ndio alikuwa anongelewa? Kwani ni yeye msaliti? Ni yeye alikuwa ana kwapua taarifa za serikali na kuzivujisha?
 

Mkuu hebu hayo maswali muulize Lissu maana ni yeye amesema alipigwa Risasi kwa kuisaliti nchi na kudukua taarifa za serikali! Lakini leo ndio nimejua kumbe Lissu ni msaliti
 
Baada ya kupokea hiyo ripoti ..walienda nje kupiga picha..wakiwa wamekaa kwenye viti alikuja kijana" kipepeo" akamnong'oneza PM alafu PM akaongea jambo na mkubwa wake..baada ya dk 15 tukasikia Mh Lissu ameshambuliwa..ukienda sasa hivi YouTube kipande hiko kimetolewa..unganisha dots
 
Hahahahah alimtaja nani jina? Hata siku moja Rais hajawai taja jina la Lissu!

Swali Lissu amejuaje kama ni yeye ndio alikuwa anongelewa? Kwani ni yeye msaliti? Ni yeye alikuwa ana kwapua taarifa za serikali na kuzivujisha?
Unajua Mr Amsterdam anaendelea na uchunguzi wake?kuna jitu litaenda The Hague
 
Lee van Cliff! Jina lako linaonesha fika wewe ni raia wa nchi gani. Haya unayouliza ya sheria za nchi yetu yanakuhusu nini? Nyie ni kati ya washirika wa huyu Tundu Lissu. Na Adam Robertson alishajitokeza. Tunasema mtukome.
 

Kwa hiyo Tundu Lissu anakiri yeye ndio msaliti........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…