Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

Marekani na Urusi ni mahasimu wakubwa mno,lakini nchi mojawapo ikikamata msaliti au hata jasusi wa nchi hasimu huwapeleka mahakamani na kufungwa.
Je. Marekani na Urusi wakiwakamata raia wa nchi zao ambao ni wasaliti wanawafanyaje? Wewe, ungemkata msaliti wa nchi yako ungemfanyaje? Jitahidi kujibu maswali haya kwa ukweli na ukiwa kwenye 'objective mode'.
FBI na CIA waliopo ubalozi wa marekani walichunguza tukio lote kwa siri wakampa Tundu lisu taarifa na file lote, kampeni zikianza Tundu lisu atamwaga ukweli wote na ndipo utashangaa na kujua Duniani hakuna siri ukitenda mabaya chini ya jua lazima yajulikane tu.
Una uhakika gani kuwa ni ukweli? Usisahau US ni wataalamu wa kutengeneza picha ikaonekana kweli. Hawashindwi kwa mujibu wa maelezo yenu humu jamvini. Ninyi mara nyingi mnapiga kelele humu, kuwa Marekani hashindwi kitu, sasa katika mkutadha huo unawezaje kuzikubali tuhuma hizo kuwa ni za kweli badala ya kuzichunguza kwanza ukizingatia ubora wa teknolojia ya sasa?

Ha ha ha aaa ! Mdogo mdogo tutaelewana.
 
Hii ni kashfa kubwa sana kwa Bw. Magufuli na serikali yake, ingekuwa kwenye nchi zilizostaarabika hangekuwa tena na nguvu za kuweza kusimama na kuomba kura, angelazimika tu kujiuzulu mara moja.

Lkn kwa kuwa ni huku uswahilini ambako rais anajiona Mungu mtu anajifanya kukomaa tu lakini kwa kuwa madai hayo ni ya ukweli hakuna anachoweza kumfanya huyo "mhanga" wake, itabidi tu ale pini japo sifa yake tayari imekwisha haribika kuwa yeye ni muuaji...!!! Very shameful for a Head Of State.
 
Msaliti haitaji kuishi kabisa kwan yeye mwenyewe kuifanya hiyo kaxi ni sawa na muuwaji kabisa. Km kweli yeye ni msaliti kam alivyojiisi hata mm niko tayari kujifunga bomu nife naye ila nchi yangu iwe salama
Usaliti haukusemwa wa kitu chochote,
Ameongelea msaliti
Wewe pia msaliti kwa mkeo, nani ajifunge bomu afe na wewe, kati ya mkeo na watoto wako?
 
Ndiyo hivyo tena...

Huyo Tundu Lissu ana "guts" hadi anadiriki kutoa tuhuma nzito kiasi hicho kwa mkuu wa nchi!........

Amewaachia mpira huo waucheze Jeshi letu la Polisi, waliokuwa wanadai kwa muda mrefu kuwa uchunguzi wao utaendelea pale Tundu Lissu atakaporejea nchini na ndiyo hivyo kesharejea na ameamua kuyaweka hadharani mambo yote yaliyomtokea!
Mkuu kwa tukio la kupigwa risasi lissu ,JIWE na BASHITE hawawezi kuruka hapo!!
 
Kusema "kusaliti nchi ya watu milioni 50", bado haitoshi..

Hebu fungua kamusi ya kichwa chako kwanza....

Tafuta neno " usaliti" ama "msaliti" katika muktadha wa "nchi" au "taifa" kisha tupe maana yake...

Kisha jiulize swali hili la mwisho wewe mwenyewe sasa;

Did Tundu Lissu betray his own country? If the answer is YES, explain how he betrayed it...

Najua hutakuwa na jibu kwa sababu akili zenu LB7 hazifikiri ktk masafa haya...

NIKUELIMISHE KIDOGO:

Kosa la "usaliti wa nchi" kisheria ndilo linaloitwa "UHAINI"...

Anayehukumu kuwa hapa kuna kosa la UHAINI limetendeka, ni mahakama tu...!

Ni lini Tundu Lissu aliwahi kupelekwa mahakamani ni mahakama kumhukumu kuwa ni MHAINI?

Jibu ni: HAKUNA!

Ila katika hii iliyokuwa "Tanzania ya Magufuli" ya miaka mitano inayoisha Oktoba, 28; huyu Magufuli kichwa chake na mawazo yake ndiyo yalikuwa mlalamikaji, mwendesha mashtaka, shahidi na Hakimu/Jaji...

Tena hukumu za "Jaji/Hakimu Magufuli" ni za gizani na kwa kutumia Kundi maalumu la majambazi kufanya excursion ya hukumu hizo...

Hizi ni tabia za viongozi madikteta tu...

Nanyi wafuata upepo bila hata kufikiri, mnaimba na kushangilia tu kama mazuzu huku mkiimba na kushangilia vifo vyenu wenyewe na watoto wenu....

Poor you, Crimea...
Kitaturu
Umempa ukweli mchungu huyo Lumumba buku 7 club.

Hawa jamaa wanataka tutawaliwe, kwa staili ya jungle rule...........

Hajui kuwa baadaye hata yeye na watoto wake wataathirika na staili hiyo ya utawala

Mwenye masikio na asikie
 
Mkuu hebu hayo maswali muulize Lissu maana ni yeye amesema alipigwa Risasi kwa kuisaliti nchi na kudukua taarifa za serikali! Lakini leo ndio nimejua kumbe Lissu ni msaliti

Huyu hapa mwingine kichwa maji....

Swali la kujibiwa ni hili moja tu na ndilo mnalopaswa kumjibu Tundu Lissu...

Hao mnaowaita "wasaliti wa nchi" ndiyo hukumu yao inakuwa hivi?

Ukijibu kuwa "ndiyo, hiyo ndiyo hukumu yao na Tundu Lissu alistahili", Mimi sitajibazana na wewe, nitakuacha kama ulivyo...!!

Lakini kama jibu ni HAPANA, siyo hivyo; basi Tundu Lissu aulizwe swali gani tena na wewe au Mimi??
 
Kwa ni uongo si kweli alikuwa anakwamisha juhudi za vita vya kiuchumi kwa jina la makanikia ambavyoTaifa lilikuwa likipambana na wale wezi wa madini. Kwani ni uongo kuwa alikuwa msaliti akitaka kukwamisha vita hiyo. Ajitafakari kaacha tabia yake ya usaliti na uasi au anaiendeleza kwa style nyingine?
Unaweza kuthibitisha uliyo yaandika? Au unaandika tu nyuma ya keyboard
 
Kwa hiyo Tundu Lissu anakiri yeye ndio msaliti........
Jpm hana haki ya kumuita mtu yeyote kuwa ni msaliti wa taifa kwa sababu sheria zote za nchi zina simamiwa na mahakama so kama alimuita mtu yeyote kuwa ni msaliti alikuwa ana ikanyaga katiba ya nchi wenye haki ya kusema kuwa mtu fulani ni msaliti ni mahakama tena ni baada ya kufuatilia vifungu vya sheria ambavyo vinathibitisha kuwa kwa hiki alicho kifanya fulani sheria inamtaja kuwa ni msaliti
 
Back
Top Bottom