Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

View attachment 1543623
Mgombea Urais wa Chadema katika uchaguzi mkuu ujao mwishoni mwa mwaka huu, Tundu Lissu, ametoa madai mazito mjini Njombe jana katika ziara zake za kutafuta wadhamini, akimuhususisha Rais, kuhusu jaribio la kuuawa kwake, lililofanyika September 7 mwaka 2017.

Akihutubia umati wa wananchi, alikumbushia historia ya tukio lake la kumiminiwa risasi, ambapo aliponea chupuchupu kuuawa na kukimbizwa nchi za nje kwa matibabu.

Akisimulia mkasa huo alieleza kuwa kuna "connection" kati ya hotuba aliyoitoa Rais Magufuli, ya uzinduzi wa ripoti ya tume ya madini, masaa takribani mawili, kabla ya kupigwa kwake risasi, aliyotoa akiwa Ikulu, jijini Dar-es-Salaam.

Aliendelea kueleza kuwa katika hotuba hiyo aliyotoa Rais Magufuli, ambayo alidai ipo ndani ya YouTube, alimnukuu Rais akiyatamka maneno yafuatayo "Katika mapambano ya kijeshi, huwa wana kawaida ya kumwua, askari yeyote ambaye anawasiliti katika mapambano yao, vile vile katika vita ya kiuchumi ambayo nchi yetu inapigana hivi sasa, hatuwezi kuruhusu ku-survive kwa mtu mmoja, ambaye imebainika amekuwa akiwasiliana na mwanasheria wa kampuni hiyo ya madini, Deo Mwanyika, ili kumwibia taarifa mbalimbali nyeti, katika lengo lao wakishirikana na mabeberu kutoka nje ya nchi, katika kutuhujumu malipo yetu ya madini, huyo mtu hastahili kabisa ku-survive" mwisho wa kunukuu.

Tunajua kuwa katika tukio hilo la kupigwa kwake risasi mwaka 2017, Tundu Lissu, Jeshi la Polisi limekuwa likutaaminisha kuwa uchunguzi wa tukio hilo unakwamishwa na Tundu Lissu, muhanga mkubwa wa tukio hilo, pamoja na Dereva wake, ambao wote walikuwa wameenda nchi za nje kwa matibabu.

Hivi sasa Tundu Lissu amesharudi nchini na amewapa "hints" ya kilichompata siku ile ya kutisha sana, ambapo "watu wasiojulikana" walimpiga risasi mfululizo 16 mwlini mwake katika jaribio la kutaka kumwua na ameeleza mwenyewe nini kilimtokea siku ile, ambapo Jeshi letu la Polisi, limekuwa likidai kuwa limekwamishwa kuendelea na uchunguzi wake, kutokana na kukosekana ushahidi huo wa Tundu Lissu

Kwa hiyo nadhani Jeshi la Polisi lingeanza kufanyia uchunguzi wa tukio lile sasa, kwa "hints" alizozitoa yeye mwenyewe muathirika wa tukio lile Tundu Lissu.
Hii hapa
 

Attachments

  • Subpost 2 - Connect dot's utaelewa tu... - NoHateNoFear - SasaBasi - TunduLissu2020 ( 264 X 48...mp4
    1.1 MB
Nchi ina miaka 59 haina maendeleo licha ya kuwa na rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani, kama ingekuwa siyo CCM mda huu Tanzania ingekuwa ni level ya America, German, China, England, Urusi na mataifa mengi tajiri Duniani na ingekuwa na kura ya veto, CCM imedumaza maendeleo na hasa CCM hii ya sasa iliyo kwenye utandawazi inayotumia pesa nyingi kudidimiza demokrasia, kuwabambikia kesi kuwapiga risasi wapinzani, kudhoofisha chadema kuua upinzani kwa nia ya kurejesha mfumo wa chama kimoja pekee, pesa nyingi inapotelea kwenye mambo yasiyo na tija kwa Taifa badala ya maendeleo.
 
Sijawahi kusikia serikali yenye wahalifu wapumbavu kama Tanzania. Inawezekana Magufuli alikuwa hajui kinachpkwenda kutokea, lakini wahuni wakachomeka kwenye hotuba yake ili aonekane alikuwa anajua shambulizi lile na hivi hata yeye uwezo wa kuchuja maneno ni below 0, basi akalipuka nalo.

..Jpm aliharibu zaidi baada ya tukio kutokea.

..SERIKALI ilipaswa kuchukua jukumu la kumtibu popote pale duniani.

..tungeweza kuomba hata kwa nchi WAHISANI zitusaidie ktk matibabu ya TL.

..badala ya kufanya hivyo Magufuli na Ndugai wakaendelea kumuadhibu TL kwa namna ambayo inaonyesha hawana UTU/UBINADAMU.
 
Basi alipata alichostahili!

Na huyu anazidi kujivua nguo! Anafikiri anaongea ukweli kumbe anajianika jinsi alivyokuwa analisaliti taifa!
Subiri tutamuinesha adhabu yake hapo oktoba.

Huyo mhujumu uchumi mwenyewe waliotuaminisha katuibia hela ambazo kila mtanzania angeweza kununuliwa Noah leo amekuwa mgombewa wenu.Msitufanye wajinga,sisi siyo wajinga.Mlitaka kunyamazisha Lissu ili asiibue uozo wenu.Imekula kwenu,Mungu wa Haki amewaonyesha kwamba huyo hakustahili ku uawa kwa kuwa ALISIMAMIA HAKI NA KWELI.
 
Huyo Deo Mwanyika wa Barrick Gold aliyesema anavujisha siri za nchi kwa Tundu Lissu na kumfunga detention miaka kadhaa na kisha kumwachia I hope sio huyo huyo waliyempitisha leo kuwa mgombea ubunge wa CCM Njombe Mjini.

Ni yeye ???

..Deo Mwanyika anayegombea CCM ndiyo alikuwa mtumishi wa ngazi za juu wa Barrick hapa Tz na baadae Afrika.
 
Sijui ni kwanini watetezi hawa wa Rais Magufuli hawana uwezo wa kuelewa...

Ni wazi kabisa ndani ya mioyo yao wanajua kuwa Mzee wao huyo alichemka na anaendelea kuchemka siku hadi siku...

Sasa wameamua kuuvaa ujinga kutetea kila ujinga na upumbavu ili mradi wao wanalipwa....
Kwani wewe hujasikia kuwa mwanachama yeyote wa CCM, kwanza analazimika kuu-surrender, ubongo wake pale Lumumba.......

Ndipo uruhusiwe kuendelea na shughuli za chama 😁 😛
 
Nafikiri unachanganya kati ya Ujasiri na mental disorders!
Bila shaka mwenye mental disorder utakuwa ni wewe thats why umeshindwa kutofautisha kati ya ujasiri na mental disorder wahi milembe faster
 
..Deo Mwanyika anayegombea CCM ndiyo alikuwa mtumishi wa ngazi za juu wa Barrick hapa Tz na baadae Afrika.
JokaKuu
Ndiyo huyo huyo.......

Hebu jaribu ku-imagine namna huyu Magu, anavotugeuza watanzania wote kuwa wapumbavu na malofa

Hivi utawezsje kumteua mtu kwenye nafasi kubwa kama hiyo ya uwakilishi, wakati mtu huyo huyo umemtukana sana na kumuita mwizi na anatumika na mabeberu?
 
Kumbe ni kweli alikuwa anatoa information kwa mabeberu, watu type yake ni cancer kwa taifa na dawa yake ni kuwa multply by zero.
We mbwa unazo taarifa za ununuzi wa ndege kutoka kwa mabeberu...... Zimefungiwa chato hakuna hata mwanaccm moja anayejua ni yy na watoto wa dada tu ndo maana ni siri kali ikihoji unapotezwa fastaaaa......
Kwa Maneno Lissu ni wakala wa mabeberu lkn kwa VITENDO wakara wa mabeberu ni magufuli......
Kesi nyingi tulizoshitakiwa kwa kuvunja mikataba kiholela tunashindwa inasemekana Magu alifanya makusudi ili mabeberu wakishinda naye anamgawo wake........

Hii nchi ni kubwa na ina siri mbaya zaidi ya ujuavyo....... Hapo nimekuibiwa ili kukutoa matongotongo upate mwanga na uanze kuelewa ccm maana yake nini
 
Bado anatafuta kura za huruma?
kibaraka wa mabeberu hapewi nchi na watanzania, hata asimulie mwanzo mwisho wa tukio lake mpaka anarudi.
 
Tundu lisu ndiye aliwaleta wachimbaji madini wa kizungu Tanzania? Uwekezaji wa mkapa na Lisu wapi na wapi? Aliyewaleta hao wazungu Nchini ndiye msaliti, Usikute wewe ndiyo umemuua mzee mkapa kwa kisingizio cha usaliti , kumbe tunahangaika kujua nini kilimuua mkapa? Kumbe wewe ndiyo ulimuua mkapa na upo unadunda
Lisu Ni msaliti baada ya serikali kuona mkataba una kasoro (Japo serikali ndio iliyoingia mkataba na kutaka kuuvunja) mabeberu walimpa fedha lisu na ndio akawa wakili wao na kuanza kututisha kuwa haturuhusi kuvunja mkataba na tukiuvunja tutashitakiwa MIGA na tutalipa milioni ya dollar Cha ajabu tulimpuuza na tukavunja mkataba tukawapa mkataba tunaotaka sisi(sio wa lisu na mabeberu) na tukalipwa sisi mamilioni ya dollar,lisu Ni msaliti na ni wakala wa mabeberu
 
Tatizo taratibu zipo lakini hutaki kuzirejea, matibabu ya nje ya nchi yana taratibu zake mbona hapo unakwepa kueleza? Kama unajiamulia kuondoka nchini kwenda kutibiwa nje ya nchi bila kufuata taratibu, gharamikia matibabu mwenyewe usitafute watu wa kulaumu kwa kulazimisha utaratibu usiokuwepo
Ndungai alitibiwa india kwa bilion 12 ni utaratibu gani ulitumika kumlipia gharama kubwa hivyo?
 
Back
Top Bottom