Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aifuta CCM Morogoro

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aifuta CCM Morogoro

Lissu ameshamchanganya Magufuli; kwasasa anaendelea kufuta alikopita Magufuli.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]....mtu anaandika na kujijibu mwenyewe, mnatekenyana na kucheka wenyewe.
 
Tumkubali tumkatae, tumpende tumchukie, Tundu Lissu ni kichwa cha kipekee sana kwenye siasa za Tanzania. Huyu ndiye anathibitisha u-genius wake kwa uhakika na taaluma yake inampa uwanda mpana wa kuonesha hajabaka fani, yaani yupo mahala sahihi kabisa, sio waliosoma Chemistry wanavamia siasa na kuharibu kisha tunaambiwa ni watendaji zaidi kuliko uanasiasa! Si watoke sasa siasani waende kwenye utendaji kuliko kutuharibia nchi yetu!

Historia ya Lissu inambeba tangu hajaingia siasani hadi leo hii, akifungua kinywa kutamka lazima ni mtafutano! Kumbuka kipindi anawalaza na viatu mawakili wa serikali wanapomfungulia vikesi vya kipuuzi.
 
Ccm ingekuwa inategemea sanduku la kura saivi ingesha sahaulika kitambo sana
Ki ukweli upinzani haujawahi kushinda, kinachotokea ni kuhakikisha margin inakuwa kubwa kati ya Ccm na upinzani. (Pride)

Hayo ndiyo yanakuwa purukushani ya zile za maruhani.

Safari hii hata wasipofanya purukushani Lissu hawezi shinda, tatizo ni ahadi ya ushindi wa kishindo.
 
Hivi Lissu anafikiri anaweza kuwalaghai waislamu kwa kuvaa kanzu na kofia kila Ijumaa? Nafikiri Lissu hajui imani ya uislamu! Hata, figisu figisu za mabeberu wameshindwa kujua imani ya usilamu ikoje, sasa huyu Lissu anaona anaweza kuwahadaa simply kwa kuvaa kanzu na balaghshia kila ijumaa! Uislamu siyo maigizo hata kidogo - alijue hilo na asije akajikosesha kura zao kwa kukebehi dini yao.
Mbona sijamuona akivaa kama singasinga!

Kwani imani ya kiislamu iko ndani ya vazi la kanzu? Kwahiyo ukiwa unavaa jezi na njumu lengo lako itakuwa ni ili upendwe na washabiki wa soka? Hilo vazi la kanzu lilivaliwa na waarabu huko mashariki ya kati kwa ajili ya hali ya joto. Waislamu wanalivaa kwa ajili ya mazoea, lakini uislamu ni imani na wala sio vazi la kanzu.
 
Nimecheka huo msafara wa kukodi bodaboda umezurura njia mzima na gari ya matngazo
 
Ukitaka kujua watu wana mapenzi gani n.a. timu iwe Simba au yanga angalia uwingi wa uvaaji nguo za timu kwenye uwanja

Tofauti ya mikutano ya CCM na Chadema ni kuwa CCM inahudhiriwa na wanachama wengi wakiwa wamevaa nguo za CCM Chadema wanaohudhuria ni wasiojulikana ni Chama gani

Huoni zile tshirt za Chadema ushahidi kuwa wanaohudhuria ni wapita njia waliokuja th kumshangaa Lisu

Kwa mtizimo ukitizama picha zote za mikutano ya Chadema wavaa Tshirt za Chadema ni wa kumulika na tochi ni kama hawapo kabisa

CCM mikutano yake unaona wazi kuwa waliofurika wengi ni wafia chama sio wapita njia Chukua picha zote za uzinduzi wa Chadema na za CCM utaona hilo tofauti wazi bila chenga

Kwa taarifa yako kwa sasa watu wengi ni washabiki wa vyama kuliko uanachama. Yaani watu wanapenda vyama toka moyoni na wala hawana muda wa kuvaa uniforms Wala kumiliki kadi. Ccm bado inaamini kwenye nguo, maana ni chama cha kizee hivyo bado kinaamini kwenye mbinu za kizamani za mavazi.
 
Go Lissu, hongera sana Mh.mdada mgombea ubunge nikutake radhi nilikudhania umefika bei kwa Abood kumbe ni fitina za maccm.Nimependa hoja yako ya viwanda moro.
 
..kawauliza wananchi kati ya sgr na viwanda kipi muhimu?

..wananchi wamejibu viwanda ni muhimu zaidi.

..idara ya maji badala ya kusambaza maji imejenga jengo la ghorofa.

 
Back
Top Bottom