Uchaguzi 2020 Tundu Lissu akiwa Iringa: Upinzani ni Watu, ukitaka kuua Upinzani ua kwanza Watu

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu akiwa Iringa: Upinzani ni Watu, ukitaka kuua Upinzani ua kwanza Watu

View attachment 1541007
View attachment 1541009View attachment 1541010

Huu ndio ukweli wa dunia ya leo , si kazi rahisi kuua upinzani kama baadhi ya viongozi walivyowaongopea wenzao .

Picha ya kwanza hapo juu ni Mgombea Urais wa Wananchi wa Tanzania akiomba udhamini Iringa Mjini leo hii , picha mbili za chini ni za jana jioni alipokuwa anasubiriwa na wananchi bila mafanikio baada ya kuchelewa kufika

View attachment 1541020
Nimeipenda hii.uchumi wakati bila ajira
 
Napenda nikujibu hilo swali lako lakini kwa kuwa ni wewe umeleta bandiko la kusifia umati, unalo jibu kama Mgombea huyo anatafuta wadhamini au yuko kwenye kampeni?

Itoshe kukumbusha kuwa waliojitokeza kugombea ni wengi, ngazi zote, kama kila mgombea atatafuta wadhamini kwa njia hiyo, hakika amani ingekuwa mashakani.

Acha utoto boss, mbona amani isiwe shakani kwenye kampeni, au kwenye kampeni wanakuja watu tofauti? Wavunja amani nchi hii ni ccm, kwa ushirikiano na jeshi la polisi.
 
Huku wakiimba wimbo wa Sarafina wa "Freedom is coming tomorrow", wananchi wa Iringa wamempokea Lissu kwa wingi ambao ni wa kihistoria kwa mji huo.

Wananchi wamefurahi mno kumuona Tundu Lissu akiwa hai baada ya kukosakosa kuuawa katika shambulio lililoitia doa nchi yetu miaka mitatu iliyopita.

Ziara hiyo ya Lissu inafuatia kiu ya wananchi kusikiliza maoni ya upande wa pili baada ya kuwa ni wenye kusikiliza misimamo ya CCM zaidi huku wapinzani wakiwa wamefungwa mikono kutumia haki yao ya kufanya siasa nchini kwa mujibu wa katiba na sheria.

Kwa mapokezi haya ni dhahiri wananchi walikuwa na dukuduku kali dhidi ya serikali hii iliyoko madarakani na inatoa dalili kuwa kama uchaguzi utakuwa huru na haki basi CCM haina chao :

Hii video inaonyesha mapokezi ya Tundu Lissu

Hata kichaa huwa anazungukwa na watu wengi kumshangaa

Watu wakipungua - amechokwa. Wakiwa wengi wanashangaa kichaa.

Mtamaliza misamiati yote.

Kwamba ni kichaa? Mwulize jiwe au yule bwana wa ruangwa.

Habari ndiyo hiyo.
 
View attachment 1541007
View attachment 1541009View attachment 1541010

Huu ndio ukweli wa dunia ya leo , si kazi rahisi kuua upinzani kama baadhi ya viongozi walivyowaongopea wenzao .

Picha ya kwanza hapo juu ni Mgombea Urais wa Wananchi wa Tanzania akiomba udhamini Iringa Mjini leo hii , picha mbili za chini ni za jana jioni alipokuwa anasubiriwa na wananchi bila mafanikio baada ya kuchelewa kufika

View attachment 1541020
Jamani kampeni hazijaanza! Zikianza itakuwaje sasa? Si watu watakufa?
 
CDM msisahau wasimamizi wa uchaguzi ndio wanaochagua mshindi nchi hii.
 
Back
Top Bottom