Tundu Lissu akiwa Uganda amemsifia Mwalimu Nyerere lakini ni yeye ndiye aliyemtukana kwenye Bunge la Katiba

Tundu Lissu akiwa Uganda amemsifia Mwalimu Nyerere lakini ni yeye ndiye aliyemtukana kwenye Bunge la Katiba

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Mwanasiasa msanii sana huyu, wakati wa bunge la katiba alimkashifu sana Baba wa Taifa, aliwaudhi watu wengi sana kwa kauli zake dhidi ya Mwalimu Nyerere.

Alivyo mnafiki ameonekana kule uganda akitoa mhadhara na akamwelezea vizuri kabisa Mwalimu Nyerere.

Ukiwa mnafiki utotoni ukifikia uzeeni lazima utakuwa mchawi
 
Mwalimu Nyerere alikuwa binadamu kama binadamu wengine kuna mazuri yake na mabaya yake kwahyo kumkosoa Mwalimu sio kumtukana ila kuthibitisha ubinadamu wake. Kwahyo Tundu hakuwai kumtukana ila alimkosoa katika baadhi ya mambo.
 
Kamjaribu Trump kama hatutakuona kwenye midege yao na pingu shingoni😂😂😂
Trump amefanikiwa kuaminisha ulimwengu kwamba ni Hero au Savior kumbe ni nyoka mwenye vichwa viwili.
 
Mwanasiasa msanii sana huyu, wakati wa bunge la katiba alimkashifu sana Baba wa Taifa, aliwaudhi watu wengi sana kwa kauli zake dhidi ya Mwalimu Nyerere.

Alivyo mnafiki ameonekana kule uganda akitoa mhadhara na akamwelezea vizuri kabisa Mwalimu Nyerere.

Ukiwa mnafiki utotoni ukifikia uzeeni lazima utakuwa mchawi
Amejichanganya sana huyo mzee na pia sidhani Rais Museveni alifurahishwa na maneno yake Juu ya Mwl. Nyerere
 
Tundu Lissu mbona ameongea vizuri Legacy ya Mwalimu, mazuri yake na mwishoni aliongelea madhaifu yake
 
Sasa ulitaka akamtukanie Kwa watu? Hizo ni Siri za ndani
 
Mwanasiasa msanii sana huyu, wakati wa bunge la katiba alimkashifu sana Baba wa Taifa, aliwaudhi watu wengi sana kwa kauli zake dhidi ya Mwalimu Nyerere.

Alivyo mnafiki ameonekana kule uganda akitoa mhadhara na akamwelezea vizuri kabisa Mwalimu Nyerere.

Ukiwa mnafiki utotoni ukifikia uzeeni lazima utakuwa mchawi
Amemsifia katika nini na alimkashifu katika nini?

Kwani mtu hawezi kumsifia Nyerere kwenye mambo fulani, kwa mfano, kusimamia uhuru na umoja wa Afrika, kupinga ubaguzi wa rangi, kujenga umoja wa kitaifa, na pia kumsema vibaya kwenye mambo mengine, kama kufuta vyama vingi miaka ya 1960s, kuminya demokrasia, kuharibu uchumi wa nchi, etc?

Kwa nini unaona kuwa ukimsifia mtu ni lazima umsifie kila kitu, na ukimpinga mtu ni lazima umpinge kila kitu?
 
Shida waswahili hua hamtaki mwalimu asemwe kwa mambo mabaya aliyo fanya mnasahau kwamba mwalimu alikua ni binadamu na alikua anakosea, na moja ya kosa kubwa kabisa alilofanya ni kutuachia muungano wa kipumbavu kabisa kuwahi kutokea duniani na ndio maana yeye mwenyewe akaandika kitabu "tujisahihishe"
 
Trump amefanikiwa kuaminisha ulimwengu kwamba ni Hero au Savior kumbe ni nyoka mwenye vichwa viwili.
Ukimkosoa wewe ni kwisha.

Sasa utaweza kusema, 'oh kule hawateki watu au hawawekwi gerezani' na mengineyo kama hayo. Sawa ila...

Utatengenezewa zengwe na watakutengeneza ipasavyo yaani wanakuua tarativu-killing you softly-na bora uende gerezani yaishe, walakini ile psychological warfare watakayo kufanyia hata poo huwezi kuomba.

Unaenda kujinyamazia na kufa taratibu yani utanyong'onyea tu whatever pension uliyobaki nayo ndio itakayo kulisha, zaidi ya hapo, wewe ni mfu tu.

Ushahidi? fuatilia wote waliomkosea huko nyuma.

Sio majaji, maseneta, ma jenerali na hata magavana. Wametupwa chini

UKiingia kwenye media za MAGA movement ndio utaona na kusikia, Fulani amemkosea na kumtukana, ila kwasababu watanzania wengi hawajui hayo, wanadhani huko hayatokei.
 
Hakuna binadamu asiekosea, ametambua makosa yake amejirekebisha.
Hata mimi nilimkashifu sana Dr John Pombe Magufuli, badae nilimwomba radhi.
 
Amejichanganya sana huyo mzee na pia sidhani Rais Museveni alifurahishwa na maneno yake Juu ya Mwl. Nyerere
Hakwenda Makerere kumfurahisha mtu, ila kutoa mhadhara kulingana na mada waliyoiandaa
 
Back
Top Bottom