Tundu Lissu akiwa Uganda amemsifia Mwalimu Nyerere lakini ni yeye ndiye aliyemtukana kwenye Bunge la Katiba

Hapa wewe ndio unatakiwa kupimwa akili.
 
Wewe ndiye ukapimwe akili,usiye elewa kueleza wasifu wa mtu wewe unaita matusi. Haya yaeleze hayo matusi aliyotukana Lissu kwenye bunge la Katiba. Lissu kaeleza mazuri ya Nyerere na mapungufu yake pia kwani hakuna binadamu aliye mkamilifu.
 
Hakwenda Makerere kumfurahisha mtu, ila kutoa mhadhara kulingana na mada waliyoiandaa
Sijakataa hayo. Nahakuna pahala nimesema alienda kumfurahisha mtu.

Wapo vijana ambao walimshangaa sana na majibu yake, itoshe karibia mengi aliyo yasema kuhusu Mwl. Nyerere ni yale ya kukaririshwa tu.
 
Hakuna kitu kinakera kama CCM kujifanya mnapenda sana Nyerere wakati miiko yake hamfuati!! Mnapenda kumsifia mdomoni ila matendo yenu ni kinyume kabisa.
 
Hapa nadhani tatzo ni english aliyotumia. Angeongea kiswahili ungemuelewa zaidi.
 
Wakupimwa akili ni wewe sio lissu.
 
...na hii hoja yako ni moja kati ya ushahidi wa udhaifu wa Nyerere. Kujenga taifa lenye watu waoga na wanafiki. Kupinga kiongozi kwao ni matusi. Tuliona wakifanya hivyo kwa Kambona na Abood Jumbe
 
Tundu Lissu mbona ameongea vizuri Legacy ya Mwalimu, mazuri yake na mwishoni aliongelea madhaifu yake
Ni kwamba alivurugwa. Karibia mwishoni alivyotajwa hasimu wake tu, unaona mtu body language yake imebadilika, na majibu yake yakabadilika. Akaanza kuruka ruka.
 
Nyerere Kuna sehemu alikosea pakubwa sana katika Nchi yetu.mfano kutuunganisha na muungano wa kihuni kati ya Zanzibar na Tanganyika pasipo kuzibgatia usawa katika muungano.pia sera yake ya kijana ilikuwa sera ya hovyo kabisa kwenye uchumi wa Nchi yetu yaani ulidumaza na kuwafanya watanzania kuwa na akili finyu kama ilivyo machawa Kwa Sasa.Tundu lisu Yuko sahihi kumkosoa na kumsifia maana Nyerere yote alifanya mazuri na mabaya
 
Hukumsikiliza Lissu au una tatizo la kuelewa lugha? Kampala katoa critique ya Nyerere kama anavyoielezea siku zote akiwa hapa Tanzania. Kama kwako critique maana yake ni kashfa, tafuta mwalimu akueleze maana yake.

Hukuelewa kabisa Lissu alipoonyesha kuwa Mwalimu alivyogeuza nchi kuwa a totalitarian state yenye imperial presidency? Hayo ndiyo maelezo mazuri unayosema hapa?
 
Kwa sababu Wakatoliki wenyewe wana njama mbovu za kumvika utakatifu.

Kwa mantiki hiyo, kuna harakati kubwa ya kumsafisha sana Nyerere hadi atakate, kama ambavyo CDM walimsafisha Lowassa na kumtunuku heshima kubwa ya kupeperusha bendera ya urais.

Wanachofanya wanaanza kumsafisha mabaya yake, kisha wanayasahau, halafu wanamsifia kabla ya kumhusudu na kumwabudu.
 
Hivi wewe πŸ• ulielewa ile presentation yake pale Makerere au lugha ilikupiga kikumbo?
 

..Duh!

..wameishaanza kutekana, kutesana, na kuuana, kwa mambo ya kisiasa kama huku Bongo?

..kazi kweli kweli!!
 
Amemsifia kwa kitendo cha kukubali kuwa na Katiba ambayo inaweka ukomo kwa muda wa uraisi (katiba ya kwanza kwa Afrika kufanya hivyo). Pia kakosoa hatua za kumtangaza Nyerere kuwa mtakatifu akisema kuna maovu mengi hayasemwi. Zaidi kaeleza uhusika wa Mwalimu katika kuingilia masuala ya ndani ya Uganda kwa kuweka na kutoa maraisi kama inavyoelezwa katika kitabu kilichoandikwa na Kanyeihamba.
 
Itabidi sijui urudie darasa pengine kama umesoma na kama hujasoma basi wewe ni wakuhurumiwa kwa sababu umeshindwa kutofautisha kati ya kukosoa na kutukana.Nakumbuka Lissu wakati akichangia hoja katika Bunge la Katiba alisema mwalimu hakuwa Malaika na kwamba hakukosea na akasema hata yeye mwenyewe anaamini hivyo Sasa hizi tafsiri zako ni za wapi?
 
..Duh!

..wameishaanza kutekana, kutesana, na kuuana, kwa mambo ya kisiasa kama huku Bongo?

..kazi kweli kweli!!
Hayo ya kutekana umesma weweπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
πŸ˜‚
Kuuana wanauna na kutesana , wanatesana saaaaaaan tu

kazi muzito.
 
Waganda wengi wanamuheshimu sana Nyerere na hata huu mchakato wa kuchunguza maisha yake ili awe mwenye heri, kwa kiasi kikubwa umeanzishwa Uganda. Kwa taarifa tu, kumekuwa na uzito fulani huku Tanzania kuhusu huo mchakato maana wana taarifa nyingi za JKN na Catholic huwa haikurupuki kufanya michakato hii.

Mama Nyerere akienda kule Namugongo, Uganda wakati wa sherehe ya Mashahidi wa Uganda, huwa anapokelewa kama rais wa nchi.

Kwa waliomsikiliza Lissu jana, alikuwa anauma na kupulizia kuhusu legacy ya Nyerere. Wale vijana wa chuo kuna mengi walikuwa hawajawahi kusikia, sasa kila geni kwao walikuwa wanashangaa.
 
"Mwalimu Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu"
(Lissu 13/04/2014)
Watanzania bado wanashauku na yale mafaili aliyosema anatembea nayo.

Je, alitudanganya na kusema uongo?
 
Haujamsikiliza TAL,itakua umehadithiwa .
 
Lugha ya Malkia imekupitia kando sana.
Lissu kamnanga Mwl Nyerere mwanzo mwisho.

Sehemu pekee aliyomsifu ni kukibali kuachia madaraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…