Upinzani Tanzania ni wazee wa matukio tu hawana vision yeyote na malengo ya kuongoza nchi, makosa makubwa wanayo fanya upinzani ni yale yale kila wakati wa uchaguzi ukifika ;
1. Kila chama kujitenga na kujiona ni bora kuliko vyama vingine, hapa namaanisha kulikuwa hakuna ulazima wa kila chama kuwa na mgombea Urais, mnazigawana kura na matokeo yake mnashindwa.
2. Kama tatizo ni tume isiyo huru achaneni Kujihusisha na uchaguzi hadi hapo tume huru itakapopatikana, mnabariki maovu nyie wenyewe.
3. Vijana wengi wa Tanzania ni majanga hao boda boda wanaojaa kwenye mikutano hawapigi kura na 60% hawaja jiandikisha, uchaguzi huu asubuhi kabisa watu wazima ndio huwahi kupiga kura na hao wengi wao ni ccm, tena maccm yana bidii kuhimizana kuwa kesho amka mapema ukapige kura mafiga matatu, vijana hawaonekani wanakuja kwa mbali tena wanakaa kidogo wakiona msululu mrefu Wanaondoka, hapo upinzani Utashinda vipi?
Mfano mimi nina shemeji yangu alikuwa anagombea udiwani, sehemu anakokaa ana mashemeji wengi na watoto wa mashemeji zake zaidi ya 40 na majukuu humo, siku ya kupiga kura mavijana yote yamelala tu, yaani huyo shemeji matokeo yake ni kura 2 , kituo kingine kura moja , yaani ni vituo ambavyo hata ndugu , vijana wengepiga kura angepata kura zaidi ya hamsini, halafu vijana hao wakipata shida Wanamuomba pesa mama huyo.
Tanzania bhana vijana sisi ndo tunawaangusha upinzani licha ya upinzani nao kuwa na matatizo mengi ya ubinafsi, mimi ushauri wangu tuvunje hivi vyama vya upinzani tuunde chama kimoja chenye nguvu, kusiwepo na chama kingine kitakacho toa mwanya kwa ccm pindi upinzani ukisusia uchaguzi , pia chama kimoja kikiundwa agenda ya kwanza tutafute katiba kabla ya yote.