Uchaguzi 2020 Tundu Lissu alikuja CHADEMA ikiwa na wabunge zaidi ya 50, anaondoka, ikiwa na Mbunge 1

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu alikuja CHADEMA ikiwa na wabunge zaidi ya 50, anaondoka, ikiwa na Mbunge 1

"Aliingia madarakani nchi ikiwa na demokrasia ya kuridhisha"

Nani huyo mwenye jukumu la kupima demokrasia!

Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. ~Julius.K.Nyerere.
Aliingia madarakani nchi ikiwa na demokrasia ya kuridhisha, hivi sasa anapanga matokeo yawe vipi akiwa ikulu. Hakukuwa na wakimbizi wa kisiasa, ila sasa hivi wapo. Nchi aliikuta ikiwa na mijadala na midahalo, sasa hivi kawageuza wananchi makondoo wa kuhutubiwa na kushurutishwa kutawaliwa...
 
Upinzani Tanzania ni wazee wa matukio tu hawana vision yeyote na malengo ya kuongoza nchi, makosa makubwa wanayo fanya upinzani ni yale yale kila wakati wa uchaguzi ukifika ;

1. Kila chama kujitenga na kujiona ni bora kuliko vyama vingine, hapa namaanisha kulikuwa hakuna ulazima wa kila chama kuwa na mgombea Urais, mnazigawana kura na matokeo yake mnashindwa.

2. Kama tatizo ni tume isiyo huru achaneni Kujihusisha na uchaguzi hadi hapo tume huru itakapopatikana, mnabariki maovu nyie wenyewe.

3. Vijana wengi wa Tanzania ni majanga hao boda boda wanaojaa kwenye mikutano hawapigi kura na 60% hawaja jiandikisha, uchaguzi huu asubuhi kabisa watu wazima ndio huwahi kupiga kura na hao wengi wao ni ccm, tena maccm yana bidii kuhimizana kuwa kesho amka mapema ukapige kura mafiga matatu, vijana hawaonekani wanakuja kwa mbali tena wanakaa kidogo wakiona msululu mrefu Wanaondoka, hapo upinzani Utashinda vipi?

Mfano mimi nina shemeji yangu alikuwa anagombea udiwani, sehemu anakokaa ana mashemeji wengi na watoto wa mashemeji zake zaidi ya 40 na majukuu humo, siku ya kupiga kura mavijana yote yamelala tu, yaani huyo shemeji matokeo yake ni kura 2 , kituo kingine kura moja , yaani ni vituo ambavyo hata ndugu , vijana wengepiga kura angepata kura zaidi ya hamsini, halafu vijana hao wakipata shida Wanamuomba pesa mama huyo.

Tanzania bhana vijana sisi ndo tunawaangusha upinzani licha ya upinzani nao kuwa na matatizo mengi ya ubinafsi, mimi ushauri wangu tuvunje hivi vyama vya upinzani tuunde chama kimoja chenye nguvu, kusiwepo na chama kingine kitakacho toa mwanya kwa ccm pindi upinzani ukisusia uchaguzi , pia chama kimoja kikiundwa agenda ya kwanza tutafute katiba kabla ya yote.
 
Hivi mnapata wapi muda wa kukaa na kuandika upuuzi wenye maandishi mengi kiasi hiki? Hata kama mnalipwa ila sio kiivyo aisee!!
 
Wamemdhamini na lazima arudi. Vinginevyo, hizo nchi tutaziwekea vikwazo vya kiuchumi, moja baada ya nyingine, mpaka waje wanakimbia na "ku-two-pi-gear mar-go-tea" kama ilivyokuwa jamaa yule wa "maksima kapa!"
weweeeen kumbeee mliyavimbia mabeberu?basi tuko vizuri kumbe
 
CHADEMA ambayo ilikuwa inanufaika na ruzuku ya zaidi ya shilingi milioni 328 kwa mwezi imejikuta katika hali mbaya baada ya ''Mtaalam wa sheria'' kuwaaminisha wanaCHADEMA kuwa anakwenda siyo kuifanya ipate ruzuku zaidi bali pia kuifanya iingie Ikulu...
Uchaguzi umeisha fanya kazi acha blabla
 
"Anayeamini kwamba tar 27 na 28 kulikuwa na uchaguzi inabidi apelekwe mirembe" - Mbowe
Jibu swali! Alisema atawaingiza watz barabarani na hatakubali? Mbona yeye ndiyo amekuwa wa kwanza kukimbia kwenda ubalozi wa Ujerumani na baadaye kwao Ubelgiji??
 
Lisu kaja uiharibu chadema Magufuli kaja kuharibu nchi na wewe unaona ni tatizo kwa Lisu kuiharibu chadema lakini Magufuli ni sawa kuharibu nchi na huoni kuwa Ni tatizo kuna shida mahali kwenye kufikiri kwako

Tuambie pia
Unadhani nani angesimama kugombea urais kwa chadema na angetoa wabunge kutoka 70 kuwa 71?
 
Upinzani Tanzania ni wazee wa matukio tu hawana vision yeyote na malengo ya kuongoza nchi, makosa makubwa wanayo fanya upinzani ni yale yale kila wakati wa uchaguzi ukifika..
Hahahaha mashemeji yamemwangusha diwani!!?? Hahahaha
 
CHADEMA ambayo ilikuwa inanufaika na ruzuku ya zaidi ya shilingi milioni 328 kwa mwezi imejikuta katika hali mbaya baada ya ''Mtaalam wa sheria'' kuwaaminisha wanaCHADEMA kuwa anakwenda siyo kuifanya ipate ruzuku zaidi bali pia kuifanya iingie Ikulu...
Hongereni kwa kufanikisha nchi kuwa ya kidekteta! suburini muone yanayofuata maana mnafikiria nchi ni Lissu pekee
 
"Aliingia madarakani nchi ikiwa na demokrasia ya kuridhisha"

Nani huyo mwenye jukumu la kupima demokrasia!

Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. ~Julius.K.Nyerere.

Karne ya 21 hii bado unaleta nukuu za karne ya 20 za kina Nyerere!
 
"Anayeamini kwamba tar 27 na 28 kulikuwa na uchaguzi inabidi apelekwe mirembe" - Mbowe

".... mwenyekiti (mbowe ) mwenyewe ana elimu ya magumashi"- Zitto

".....Anayeamini maneno ya Mwenyekiti Mbowe 100% inabidi apelekwe Mirembe"
 
Lissu sio wa kwanza kwenda asylum, akina Oscar Kambona walikimbia azimio la Arusha na wengine wengi tu Babu,Uncle Tom,Memba Lee,Ngurumo n.kwa sababu mbali mbali hasa economy asylum ndio walio wengi ughaibuni.

Labda jambo muhimu kwa opposition waliingia uchaguzi mkuu huu wakijua kabisa matokeo hayatakuwa rafiki kwao.Cha ajabu wakajitosa na kilichotokea ni bunge la sasa.

Mwaka 2025 haupo mbali, maadalizi yangeanza mapema,ya kupata katiba mpya which is most likely kwa mategemeo kuwa Raisi wa awamu ya sita atatoka Zanzibar. Ni kawaida ya Bara kutojisikia sawa wanapotawaliwa na Zanzibar.

Kwenye katiba mpya ndio utakuwa ufunguo wa mpya wa siasa za ushindani.
 
CHADEMA ambayo ilikuwa inanufaika na ruzuku ya zaidi ya shilingi milioni 328 kwa mwezi imejikuta katika hali mbaya baada ya ''Mtaalam wa sheria'' kuwaaminisha wanaCHADEMA kuwa anakwenda siyo kuifanya ipate ruzuku zaidi bali pia kuifanya iingie Ikulu...
Kwa sababu "aliibiwa" wabunge 49.
 
Hahahaha mashemeji yamemwangusha diwani!!?? Hahahaha
Ukiwauliza hao vijana kuwa jamani mmepiga kura? majibu yao ilikuwa hata tukipiga kura CCM itashinda tu, kwahiyo tuna kazi kubwa ya kutafuta votes hasa za vijana otherwise tutakuwa tunalalamika miaka yote.

CCM bana yana discipline wakati wa uchaguzi, yaani mbunge wa CCM kazi zao ni kuleta pesa tu kwenye kamati zao za ushindi na hizo kamati zina fanya kazi kubwa kuwaletea ushindi, balozi wa nyumba kumi ana hamasisha watu wakapige kura katika sehemu yake wachague ccm matokeo yake ndo haya, upinzani ujipange upya.
 
Wapinzani wamejimaliza wenyewe
sasa kama wamejimaliza mnawafuatilia na kuwa tajataja wa nini? Si tumewapa nchi muamue mnachofanya sasa wapinzani mnawatakia kitu gani? Kwanza si ni wao ndo walikua wanakwamisha maendeleo?
 
Back
Top Bottom