Uchaguzi 2020 Tundu Lissu alikuja CHADEMA ikiwa na wabunge zaidi ya 50, anaondoka, ikiwa na Mbunge 1

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu alikuja CHADEMA ikiwa na wabunge zaidi ya 50, anaondoka, ikiwa na Mbunge 1

W

Wakati unamshangilia Tundu Lisu awapeleke kikamanda ulidhani anagombea nini?
Wakati mnasema hamtaibiwa kura ulidhani ni kura zipi hazitaibiwa?
Tumieni akiri basi nyie
Wewe ndio hautumii akili kabisa ,si tushasema mambo yaliyotendeka siku ya uchaguzi? Mawakala 50% hawajaruhusiwa,wengine walitishiwa mitutu ,teeth,policcm na nec ndio walikuwa na matokeo na ndio maana yule mpuuzi wa hai alimwambia mbowe "haushindi".
 
Katika kuishi kwangu, kumbukumbu zinaniambia hakuna mwaka taifa liliombea uchaguzi kama 2015
Chadema ilikua na ushawishi mkubwa karibia tuu na ilivyokuwa CCM.

Kwenye ibada za kuuga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 viongozi wa madhehebu yote, makanisani na misikitini waliukaribisha mwaka kwa maombi ya kumpata kiongozi sahihi wa kuongoza taifa hili.

2015 watanzania walikosa matumaini, imani kwa serikali ilipotea. Wengi walitegemea chadema chini msingi imara wa viongozi wake ingeinusuru nchi huku watanzania wakiombea taifakwa zaidi ya miezi9.

Ilipofika wakati wa teuzi kwenye vyama yaliyotokea ilikua miujiza ambayo hakuna aliyewahi kuwazia. Waliotegemewa kupata wakikosa na wasiotegemewa walitokea ghafla na kupata.

Mungu ibariki Tanzania

Kwani sasa wananchi ndio wamekuwa na imani na serikali/ccm? 2/3 ya watanzania wamegoma kupiga kura, je hiyo imani inatoka wapi?
 
Huu uchafuzi ndio mligharamia kwa fedha za ndani?
 
Nani aliwaambia kuwa Tume imejirekebisha? Anyways tunataka msuse tena ili kuondoa malalamiko yenu
Tulisusa uchaguzi SM tukatarajia mmejirekebisha uchaguzi huu, lakini uchaguzi huu kila mtu kaona tulikuwa sahihi kususia uchaguzi ule. Tunataka kujua unataka tususe ili nini kitokee, nijue unachotaka kwenye hilo.
 
Mimi nawashangaa sana CCM. Wapinzani mmeshawamaliza hivi mnahangaika nao wa nini tena.? Tumewaacha muongoze mpaka mtakapo choka. Lakin bado tu mnawafuatilia wapinzani mnawataka wa nn ?
Tena waishie kabisa, tunataka wapinzani wenye kuheshimu mamlaka na kushauri kwa heshima na siyo kutukana, na wakome kabisa, siasa zetu hatutakiwi kuiga za mataifa mengine, let us build our own style of opposition, siyo upinzani wa akina Zitto, yaani wakuangalia namna ya kupata madaraka badala ya maslahi ya taifa. Na bado, tuliwaambia waombe msamaha wameshupaza shingo, the end will never end for them, they are doomed to go that way infinitely!
 
Mkisusia, ccm na selikali wataona aibu kufanya chaguzi peke yao na shinikizo litakuwa kubwa kuundwa kwa tume hurh

Ingekuwa ccm wana uwezo wa kushindana kwa box la kura wangeona aibu. Uchaguzi wa marudio hapo Znz CUF ya Maalim Seif walisusia, mbona hawakuona aibu?
 
Ingekuwa ccm wana uwezo wa kushindana kwa box la kura wangeona aibu. Uchaguzi wa marudio hapo Znz CUF ya Maalim Seif walisusia, mbona hawakuona aibu?
Mnasusia huku mnachungulia mifuko ya hela?
Si unaona viongozi wao walivyoramba teuzi
 
Kwani sasa wananchi ndio wamekuwa na imani na serikali/ccm? 2/3 ya watanzania wamegoma kupiga kura, je hiyo imani inatoka wapi?
Wapo waliogoma kujiandikisha kupiga kura; na wapo hao 2/3 waliojiandikisha wakagoma kupiga kura pia, hawa kwao lolote sawa tuu. Inaonekana majority wako comfortable na hali ya siasa kwa sasa

Siku Watanzania wataguswa na kuyataka mabadiliko watasimama, watapiga kura na watasimamia wanachokitaka bila kuzuiwa na mtu yoyote
 
Ingekuwa vyama vingine vya upinzan vimeongeza idadi ya wabunge uchaguz huu ningesema aTundu kaua chama lakin hakuna chama kilichoongeza wabunge zaid ya kupungua tafsir yake uchaguz uligubikwa na ukakasi

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Wapo waliogoma kujiandikisha kupiga kura; na wapo hao 2/3 waliojiandikisha wakagoma kupiga kura pia, hawa kwao lolote sawa tuu. Inaonekana majority wako comfortable na hali ya siasa kwa sasa

Siku Watanzania wataguswa na kuyataka mabadiliko watasimama, watapiga kura na watasimamia wanachokitaka bila kuzuiwa na mtu yoyote

Watu wamepuuza box la Kura. Mugabe wakati yuko kwenye kilele cha udictator wake, alikuwa anashinda kwa 80%+ kama ccm hivi sasa. Wapambe wake kama ww walikuwa wanasema Mugabe anakubalika kwakuwa ni mzalendo. Wapinzani wake alikuwa anawaua, na kwenye uchaguzi mizengwe ilikuwa mingi ili atangazwe mshindi, kama hapa Tanzania kwa sasa. Ila wananchi uoga ulipowaisha, walimtoa bila kutumia box la kura.
 
CHADEMA ambayo ilikuwa inanufaika na ruzuku ya zaidi ya shilingi milioni 328 kwa mwezi imejikuta katika hali mbaya baada ya ''Mtaalam wa sheria'' kuwaaminisha wanaCHADEMA kuwa anakwenda siyo kuifanya ipate ruzuku zaidi bali pia kuifanya iingie Ikulu.

Matokeo yake amekuwa ni kati ya wanasiasa ambao wameididimiza CHADEMA kimaslahi huku yeye akiamua kwenda kupata ''income support'' nchi za watu.

Kelele za ''mtaalam wa sheria'' kwenye majukwaa zilikuwa ni nyingi huku akiwaaminisha anaenda Ikulu lakini ufanisi ni zero.

Tukumbuke kuwa, Mwaka 2005, ''Mzee wa anga'' aliikuta CHADEMA ikiwa na wabunge 4 na baada ya Uchaguzi akaiacha ina wabunge 5.

Mwaka 2010, ''Baba Paroko'' akaikuta CHADEMA ikiwa na wabunge 5 na baada ya uchaguzi aliiacha ina wabunge 48.

Mwaka 2015, ''Fisadi Papa'' akajitosa na kuikuta CHADEMA ina wabunge 48 na kuiacha ina wabunge 70.

Mwaka huu, ''Mtaalam wa sheria'' ameikuta CHADEMA ina wabunge zaidi ya 50 na ameiacha ina mbunge 1 ambaye kwa aibu hataki kumtambua!

Unaweza kusema lolote au kuchanganua na kuchambua lakini ukweli utabaki palepale kuwa amekuwa ni mmoja wa watu walioiporomosha CHADEMA kimapato na kuikimbia haraka sana!

''Fisadi Papa'' ilimchukua miaka 4 baada ya uchaguzi Mkuu kuikimbia CHADEMA, huyu ''Mtaalam wa sheria'' hata mwezi mmoja baada ya Uchaguzi Mkuu haujaisha ameamua kuikimbia CHADEMA!

Wafuasi wake ''maandazi'' walituaminisha huyu ''mtaalam wa sheria'' sio kama ''Fisadi Papa'' kwa sababu ni jasiri na kwa maana hiyo ''chama cha kijani'' kisimpuuzwe!

Thread zilijazana hapa Jamiiforums za kumsifia ''mtaalam wa sheria'' kwa ujasiri na nguvu za kisiasa alizonazo huku mgombea wa ''chama cha kijani'' akiambiwa ajiandae kukabidhi Ikulu kwa kupenda au kutopenda baada ya Uchaguzi Mkuu.

Mtu mwenye akili timamu atajiuliza, imekuwaje mtu aliyetuambia haogopi lolote akimbie haraka iwezekanavyo!

Hizi ni baadhi ya thread za kumsifia ''mtaalam wa sheria'' ambaye alikimbilia kwenye majengo ya balozi za Ulaya baada tu ya kumaliza kuitisha maandamano yasiyo na kikomo!

Kinachofurahisha zaidi, ameamua kukimbia bila kuwaeleza makamanda ''maandazi'' kama amesitisha maandamano au bado yapo palepale!

LINK>>>
LINK>>>
LINK>>>
LINK>>>

Mkuu, kwa hadhi yako, naamini you can do better than this ukitaka kufikia umati wa GTs. Usitake kuwa kama Trump anayeona kila kitu ni muamala mkavu wa kibiashara tu.

Tuseme unapima ubora wa Lissu kwa hesabu ya idadi ya wabunge na kiasi cha ruzuku ya CHADEMA tu? Kweli? REALITY yote ya yaliyotokea umetupilia mbali? Yaani hukushuhudia ile colossal impact ya Lissu aliyoacha juu ya nchi muda wote alipokuwepo hapa? Aidha, basi tuaminishe kuwa hapa kwetu kura za wananchi ndizo “zinazohesabu” matokeo; kwamba falsafa za Josef Stalin na Niccolò Machiavelli hazikuwa na nafasi kabisa katika Uchaguzi wetu Mkuu wa 2020.

Anyway, naona kwako cha muhimu zaidi ni magoli na si “chenga”. Kwa vile unataka tujadili “transactional politics” basi ingiza pia kigezo (factor) cha maadili kwenye sentenso (equation) uliyotumia kupigia hesabu ya ubora/ubovu wa Lissu. Labda itatusaidia kuushereka kiroho safi kabisa, ushindi wa kishindo (>84%) tuliopata na kuikandamiza CHADEMA magoli kama yote hadi kuigeuza irrelevant nchini overnight!
 
Watu wamepuuza box la Kura. Mugabe wakati yuko kwenye kilele cha udictator wake, alikuwa anashinda kwa 80%+ kama ccm hivi sasa. Wapambe wake kama ww walikuwa wanasema Mugabe anakubalika kwakuwa ni mzalendo. Wapinzani wake alikuwa anawaua, na kwenye uchaguzi mizengwe ilikuwa mingi ili atangazwe mshindi, kama hapa Tanzania kwa sasa. Ila wananchi uoga ulipowaisha, walimtoa bila kutumia box la kura.

Wananchi ndio wenye maamuzi kama ulivyosema. Ila kwa sasa hata viongozi wa upinzani wapige kelele vipi kama asilimia kubwa ya wananchi wana furaha na amani na mfumo mabadiliko bado hayawezi kuwepo.
Lingine ni upinzani wenye malengo na upinzani imara kwa maslahi ya nchi. Chadema walikua imara sana hadi 2015, walijenga heshma kubwa na uaminifu mkubwa sana kwa watanzania, walihubiri vitu vya msingi vilivyogusa maslahi ya wananchi na wananchi wake ambavyo hakuna chama kilikua kinafanya.
Kitendo cha chadema kukusanya na kuyatetea yale maovu yaliyokua yanafanywa na ccm ndio kilichowafikisha wananchi njia panda kuona heri ccm inayopiga vita ufisadi kuliko chadema inayosafisha mafisadi.

Ukiamua kuwa mpinzani mwenye mafanikio lazima uache vile vibaya watawala wanavyofanya na ufanye vile vile vizuri ambavyo chama tawala hawafanyi
 
Asilimia kubwa ya wananchi wana furaha, kisha wanaopiga kura wako chini ya 1/3! Au mimi ndio sijui furaha maana yake ni nini? Kama wananchi wana furaha/imani na ccm, zile kura za kwenye mabeg zilikuwa za nini? Ule umwagaji wa damu ulikuwa wa nini?
 
CHADEMA ambayo ilikuwa inanufaika na ruzuku ya zaidi ya shilingi milioni 328 kwa mwezi imejikuta katika hali mbaya baada ya ''Mtaalam wa sheria'' kuwaaminisha wanaCHADEMA kuwa anakwenda siyo kuifanya ipate ruzuku zaidi bali pia kuifanya iingie Ikulu.

Matokeo yake amekuwa ni kati ya wanasiasa ambao wameididimiza CHADEMA kimaslahi huku yeye akiamua kwenda kupata ''income support'' nchi za watu.

Kelele za ''mtaalam wa sheria'' kwenye majukwaa zilikuwa ni nyingi huku akiwaaminisha anaenda Ikulu lakini ufanisi ni zero.

Tukumbuke kuwa, Mwaka 2005, ''Mzee wa anga'' aliikuta CHADEMA ikiwa na wabunge 4 na baada ya Uchaguzi akaiacha ina wabunge 5.

Mwaka 2010, ''Baba Paroko'' akaikuta CHADEMA ikiwa na wabunge 5 na baada ya uchaguzi aliiacha ina wabunge 48.

Mwaka 2015, ''Fisadi Papa'' akajitosa na kuikuta CHADEMA ina wabunge 48 na kuiacha ina wabunge 70.

Mwaka huu, ''Mtaalam wa sheria'' ameikuta CHADEMA ina wabunge zaidi ya 50 na ameiacha ina mbunge 1 ambaye kwa aibu hataki kumtambua!

Unaweza kusema lolote au kuchanganua na kuchambua lakini ukweli utabaki palepale kuwa amekuwa ni mmoja wa watu walioiporomosha CHADEMA kimapato na kuikimbia haraka sana!

''Fisadi Papa'' ilimchukua miaka 4 baada ya uchaguzi Mkuu kuikimbia CHADEMA, huyu ''Mtaalam wa sheria'' hata mwezi mmoja baada ya Uchaguzi Mkuu haujaisha ameamua kuikimbia CHADEMA!

Wafuasi wake ''maandazi'' walituaminisha huyu ''mtaalam wa sheria'' sio kama ''Fisadi Papa'' kwa sababu ni jasiri na kwa maana hiyo ''chama cha kijani'' kisimpuuzwe!

Thread zilijazana hapa Jamiiforums za kumsifia ''mtaalam wa sheria'' kwa ujasiri na nguvu za kisiasa alizonazo huku mgombea wa ''chama cha kijani'' akiambiwa ajiandae kukabidhi Ikulu kwa kupenda au kutopenda baada ya Uchaguzi Mkuu.

Mtu mwenye akili timamu atajiuliza, imekuwaje mtu aliyetuambia haogopi lolote akimbie haraka iwezekanavyo!

Hizi ni baadhi ya thread za kumsifia ''mtaalam wa sheria'' ambaye alikimbilia kwenye majengo ya balozi za Ulaya baada tu ya kumaliza kuitisha maandamano yasiyo na kikomo!

Kinachofurahisha zaidi, ameamua kukimbia bila kuwaeleza makamanda ''maandazi'' kama amesitisha maandamano au bado yapo palepale!

LINK>>>
LINK>>>
LINK>>>
LINK>>>
Kwani kulifanyika uchaguzi?

Uchaguzi unaouzungumzia ulifanyika ulifanyika kwa kufuata sheria ipi ambayo kila mmoja aliridhika nayo ili akubaliane na matokeo halali ya uchaguzi wenyewe?

Sheria ndiyo inavyosema kama muteke,mpige kura feki mpeleke ndani ya vyumba, msiwaapishe mawakala wa vyama vyengine, muuwe, na ufedhuli mwengine halafu mnakuja hapa na kujisifu mmpeshinda kwa ushindi wa kishindo labda ushindi wa wizi.
 
Mimi nawashangaa sana CCM. Wapinzani mmeshawamaliza hivi mnahangaika nao wa nini tena.? Tumewaacha muongoze mpaka mtakapo choka. Lakin bado tu mnawafuatilia wapinzani mnawataka wa nini?
Hata mimi nilijua wanapanga mikakati ya kuifanya Tanzania iwe kama ulaya ifikapo mwaka 2025.

Wamebebeshwa mzigo mzito sijui watamsingizia nani
 
Tatizo la hawa maccm yanataka kuwaaminisha watu upuuzi wao kuwa ndiyo ukweli. Nafsi zinawasuta mno kuvikalia viti ambavyo siyo vya kwao.
Na ndiyo sababu hasira za Mungu zimeanza kuwashukia............

Hadi hivi sasa kabla ya kuapishwa madiwani, wanne tayari "wame-dead"

Na bado Mungu ataendelea kuishusha hasira yake hadi mnyooshe mikono juu, kutokana na Uchafuzi mlioufanya katika uchaguzi huu uliopita
 
"Anayeamini kwamba tar 27 na 28 kulikuwa na uchaguzi inabidi apelekwe mirembe" - Mbowe
Kuna kila sababu kuiomba USAid na WHO & EU watupe msaada wa upimaji wa akili na vinasaba vya Watanzania,hasa hasa wafuasi wa CCM,kisha ufanyike utafiti juu ya sababu ya matokeo hayo ya upimaji.
Kuna tatizo kubwa sana la kiakili kwa wanambogamboga huko nyumbani.
 
Back
Top Bottom