Tundu Lissu alishambuliwa na watanganyika, mzanzibari akaenda kumpa pole, aliwakimbia watanganyika, mzanzibari kamrudisha

Ulitaka aseme magu ndo alimpiga risasi hajipendi?
 
una uhakika huo ni kwamba watanganyika walimshambulia.. nadhani wewe utakua una ushahidi tosha kwa kushambuliwa kwa TUNDU.. Mana ushasema ameshambuliwa na Watanganyika!
 
Alikugawia pesa za epa na mgodi wa kiwira?
Alitengeneza miundombinu ambayo hapo awali ilikuwa shida.Akafuta kodi ya Kichwa na kodi mbalimbali za Halmashauri ambazo hazikuwa na tija.Ndiyo kipindi Tanzania ilipiga hatua kuliko wakati wowote.Ametuachia uwanja wa Mkapa,Chuo Kikuu Dodoma.Aliboresha shule za Msingi karibia Tanzania nzima.Vijana waliokuwa wamehitimu Form Four,Form Six aliwapa ajira ya Ualimu bila gharama yoyote.Alilipa madeni yote ambayo Serikali ya Mwinyi ilikuwa imekopa.Ni mtu pekee aliyefanya Tanzania iheshimiwe na majirani.Mungu amtunze sehemu nzuri.
 
Acheni kutafuta kuhurumiwa. Mwacheni Lissu auseme ukweli kuhurumiana ndo kumetufikisha hapa kama taifa.

Sidhani km lengo la Samia kwenda kumuona au kumpa passport lilimaanisha kwamba atakapokuja kuwa rais asielezwe mabaya yake. Hilo alilofanya ni jambo jema japo akikosea lazima akosolewe bila kujali alifanya nini kabla.
 
una uhakika huo ni kwamba watanganyika walimshambulia.. nadhani wewe utakua una ushahidi tosha kwa kushambuliwa kwa TUNDU.. Mana ushasema ameshambuliwa na Watanganyika!
Hata Anti mwenyewe huwa anawataja
 
Una uhakika gani kama waliomshambulia ni Watanganyika, kwanini wasiwe wazanzibari? 🙁
 
Hizi ni akili kisoda kabisa hizi, kwako wewe ukipewa msaada, mambo yote utayoambiwa na mtoa msaada utayatii hata kama yanadharilisha utu wako siyo?
 
Kamrudisha? Wapi? hapa ni KENYA? hapa nikwao lazima arudi CCM mmeishiwa hoja...
 

Mambo hayo waliyasema Uamsho miaka ile na wakabambikiziwa kesi ya ugaidi pamoja na kusekwa gerezani kwa miaka 9
 
Mbona kama hujui siasa zilivyo? Siasa huinua na pia siasa hushusha, hakuna rafiki wa kudumu siasani na hakuna adui wa kudumu siasani. Ni michezo ya kisiasa tu, by the waya wanasiasa wanapendana sana nje ya siasa
 
Hizi ni akili kisoda kabisa hizi, kwako wewe ukipewa msaada, mambo yote utayoambiwa na mtoa msaada utayatii hata kama yanadharilisha utu wako siyo?
Tumia kichwa kufikiri, sio kubebea kamasi
 
Lissu ndiye MTU anayempenda Mh Samia kuliko ninyi,kwa kuwa anamsaidia kumuonyesha pale atendapo NDIVYO SIVYO..sio ninyi wengine kutwa KUSIFU tu!
 
Sasa huyo ndo mwasisi wa maufisadi yote mpaka baba wa taifa alishuka na masikitiko kaburini
 
Sasa huyo ndo mwasisi wa maufisadi yote mpaka baba wa taifa alishuka na masikitiko kaburini
Ufisadi uliasisiwa na Nyerere pale alipotupa Muungano usio na faida kwetu,pili alizuia tusichimbe madini kitu ambacho kilikuwa haramu kwa wakati huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…