Tundu Lissu ameongea na Radio Citizen Kenya asubuhi ya leo, ameleezea hali ya usalama nchini pamoja na suala la Corona

Tundu Lissu ameongea na Radio Citizen Kenya asubuhi ya leo, ameleezea hali ya usalama nchini pamoja na suala la Corona

View attachment 1532649

Hii ndio taarifa mpya inayozagaa mitandaoni kwa sasa .

wote mnakaribishwa

===


Mgombea wa Urais, kupitia Chama cha Upinzania CHADEMA Tundu Lissu, alivyohojiwa na Citizen Online Radio Station, kutoka Nairobi Kenyan Tundu Lissu aongea mengi kuhusu mustakabali wa Tanzania, ambae anagombania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020

Katika mahojiano hayo Waandishi wa habari Vicent Ateya na Meody Sinzore wa kipindi cha Jambo Kenya wamemuuliza masuala mbalimbali ya Kinchi na uchaguzi kwa ujumla.

Wakiuliza kuhusu suala la usalama kwa wagombea wa Upinzani Tundu Lissu amesema "Kama ambavyo nimesema mara nyingi hali ya nchi ya Tanzania sio suala lenye afya hata kidogo. Ukizungumzia sisi wa Chadema, viongozi wetu, wanachama wetu wameuawa katika mazingira ambayo hakuna uchunguzi wa Polisi hakuna chochote kilichofanyika."

"Kuna watu wetu wametekwa nyara miaka zaidi ya miwili mwandishi wa habari Azory Gwanda alichukuliwa nyumbani kwake na hajilikani alipo". Ben Saanane hajulikani alipo tangu Novemba 2016. Watu wameumizwa sana. Mimi nimeponea chupuchupu nimepigwa risasi 16. Mwenyekiti wangu amevunjwa mguu kama mwezi mmoja na ushehe uliopita, hali imekuwa mbaya kwelikweli.

Kwahiyo tunapozungumza kuwa Tanzania ina hali mbaya tuna maana hiyo. Hali ya haki z binadamu imeporomoka sana. Sio sisi tu tunaolalamika bali hata mashirika ya haki za binadamu ya nchini na kimataifa yanasema hivyo hivyo.

Sasa tunakwenda katika uchaguzi Mkuu ambao utakuwa ni wa kihistoria. Rais Magufuli na Chama chake wamesemahadharani bungeni kwamba wakishinda watabadilisha katiba kuondoa ukomo wa madaraka. Maana yake ni kwamba tutakuwa na Rais wa Maisha. Sasa sisi ambao Mwalim Nyerere alisema hatuwezi kuwa na Rais wa Maisha kama ilivyokuwa kwa kiongozi wa Malawi Kamuzu Banda, atuwezi tukakubali kurudi kwenye utawala wa aina hiyo.

Rais Magufuli mwenyewe alitangaza tarehe Febuali 6,2016 kwamba anataka kuangamiza vyama vya upinzani ifikiapo mwaka 2020. Sisi hatutokubali kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Uchaguzi huu utaamua mambo mengi sana katika nchi yetu na tunaamini kwamba watanzania hawatamkubalia Magufuli na ajenda yake na Chama chake ya kuturudisha katika miaka ya giza ya utawala wa chama kimoja.

Aidha, wakimhoji jitihada za Tanzania katika kukabili Covid 19 Lissu ameeleza kuwa Majirani zetu wote wana Corona, Tanzania ukitangaza kuwa kuna Corona ni kosa la jinai. Katika hili Lissu amesema "Sasa serikali inayoamini kwamba hakuna Corona na inawatangazia watu hakuna Corona haijatoa taarifa yoyote ya maambukizi, ya waliofariki, ya waliopona tangu tarehe 29 mwezi wa nne mwaka huu, wanaamini kwamba tukinyamaza basi Corona itapotea. Tusiposema chochote kuhusu Corona maana yake Corona hamna. Huo ndio msimamo wa serikali yetu.

Mwisho, Tundu Lissu amewashukuru Redio hiyo ya Kenya kwa kumhoji na kuweka bayana kuwa tangu amefika nchini mpaka leo hakuna kituo chochote cha habari kilichomwita na kumhoji kwa sababu viombo hivyo vinaogopa kuzuiliwa.
Nimeisikiliza hii video, Lissu kapiga nondo sana, nachoweza sema Lissu ni kidume, Lissu ni jasiri sana, maneno aliyozungumza dhidi ya utawala wa jiwe na hali iliyopo hapa nchini sidhani kama kuna mtanzania yeyote angeweza zungumza

Long live Hon Tundu Lissu
 
Kenya ndo kuna uhuru wa kuongea hapa wakudhubutu wanagunhiwa. Gaxeti la Tanzania Daima liko wap
 
JPM katili sana, ndiye aliyebariki shambulio la Lissu kuchapwa zile mvua za risasi. Muda ukifika tutaweka wazi kila kitu.
 
Hahaha mnawasha masikio ya serikali, mmeona, ni marufuku media ya ndani kuuungana na media za nje, hivyo maudhui hayo au mahojiani ya Tundu Lisu hatuta yasikia .

Atakaye yarusha wanaye.

Ukisimama nchale na ukikimbia nchale, ukikaa nchale.
 
Kwa hiyo amewaomba mumpigie kura? Au kawatuma mumsaidie kulainisha media za Bongo zimuandike na zimuhoji?
 
Kule Tanzania upinzani wameibuka na moto mkali tangu Tundu Lissu tangu aamue kurejea, ile baada ya kuondolewa kwa marisasi awali. Sasa uongozi kule ni kama umepanic vile, wamezuia kabisa jamaa hapati airtime yoyote, vyombo vyote vya habari vimeufyata, hamna hata kimoja kinadiriki kumhoji, na pia vya kimataifa kama BBC wamewekewa sheria kali hamna tena kueleza chochote cha Tanzania bila uhusika wa muwakilishi wa serikali kuwepo karibu, au hata vyombo vya habari huko vimewekewa kwamba lazima chochote cha BBC au CNN watakachotaka kukionyesha kikaguliwe na serikali kwanza.

Sasa kwa hali hiyo Tundu Lissu akaamua kutafuta mwanya kwa kuhojiwa na chombo cha Kenya ambacho hurusha matangazo yake kwa umbali unaokisiwa kufika EAC yote, hapo sasa ndio katuchonganisha moja kwa moja maana Watanzania wa mlengo wa CCM wamelipuka kwenye mitandao wanatukana hadi balaa.
Ushauri wangu kwa wapinzani wa Tanzania, hehehe pambaneni na hali yenu huko, huu mziki ni wenu, mlizembea tangu mwanzo sasa ndama amekua fahali kabisa, mpo kwenye kupumulia mashini na sioni wa kuwasaidia, tunawapenda majirani lakini kwa hili tunawaacha mtarekebishana ndani kwa ndani, hata sisi tulikua kama nyie zaidi ya miaka ishirini iliyopita na tuliiweka sawa.

===================


Tanzanian opposition leader Tundu Lissu, of Chama Cha Demokrasia (Chadema) on Monday, August 10, was interviewed on Radio Citizen's Jambo Kenya morning show hosted by Vincent Ateya.

Notably, the phone interview on the Royal Media Services (RMS) owned-station was his second appearance on Kenyan media in a matter of days, having answered various questions on KTN's Bottomline Africa days earlier on Thursday, August 6.

While interviews of regional leaders on local media are nothing new, Lissu's interview on Radio Citizen sparked an uproar from a section of Tanzanians who demanded to know why he was appearing on Kenyan media as opposed to local media.

Lissu himself addressed the matter during the interview when he revealed that no Tanzanian television or radio station had extended an invite to interview him since he returned to the country on July 27, for fear of state repression.

Lissu, who survived an assasination attempt in September 2017, only recently returned home after years in recovery and spoke on his plans to challenge incumbent President John Pombe Magufuli of Chama Cha Mapinduzi (CCM) during the presidential elections slated for October.

In recent years, multiple reports have alleged that major TV and radio stations in Tanzania had been barred from covering opposition activities.

Chadema's announcement asking their followers to engage Lissu on Radio Citizen, in particular, sparked heated debate.

"Citizen huku nilipo haipatikani kwanini hasihojiwe na media za ndani msirudie huyu anagombea Tanzania sio Kenya mtaaribu

(Citizen doesn't broadcast where I am, why can't he be interviewed on our local media. He is running in Tanzania, not Kenya, you will ruin it)," stated one Leodegard Cyril.

"Media za hapa zinapokea maagizo toka huu, hata wakialikwa Hawaii mfano mzuri ni [redacted] juzi waliweka taarifa za Lissu akipochukua fomu, ghafla wakazifuta hadi mitandaoni.

(Media here is under instructions from above, even if they are invited to cover something they won't. A good example is a (leading station), they aired the news when Lissu submitted various forms only do delete it everywhere including online," claimed one Deo Ryoba.









  • "Kwani mtanzania kuhojiwa na BBC ,Dw,Ntv ni vibaya? Au ni wigo mpana wa huyo mtu kufahamika zaidi huko na wanajua ukweli wake na ukubwa wa ujengaji hoja.
    (What's wrong if a Tanzanian is interviewed on BBC, DW or NTV? Or does it show his reach to many people and that even in other places they respect his arguments?)" wrote Haule Baraka.
    The interview made headlines for other reasons as well, as Lissu declared that Chadema lacked trust in Tanzania's electoral body to conduct a free and fair election.
    "The chairman and the chief executive of the electoral commission were appointed by President Magufuli. They have proved over the years that they are not independent," he stated.


    Listen to Lissu during the interview below:


    Tanzanians Up in Arms Over Radio Citizen Interview [VIDEO]

Tundu labda awe Raisi wa Kenya hawezi kuwa Raisi wa Tanzania na hata hana uwezo wa Kumuwazisha magufuli
 
Ukweli sasa hivi ni kuwa nyie mtabana redio zenu ila option ya kumsikiliza ni mkubwa mno kupitia redio za nje na televisheni
 
JPM katili sana, ndiye aliyebariki shambulio la Lissu kuchapwa zile mvua za risasi. Muda ukifika tutaweka wazi kila kitu.

Mm namlaani aliyemkosa Tundu Lissu,natamani ningekuwa na uwezo,hiyo jamaa ningemmaiza mm. Angemmaliza ningeagiza soda! Namchukia huyu Tundu Lissu mpaka mwisho!
 
Yaani mie huyu simuelewi kabisa, hivi wapiga kula wake wako kenya?, Watanzania wangapi wana access na hizo radio za kenya!
Wewe ni nani? Tundu Lisu ataongea na vyombo vyote vya ndani na nje ya nchi. Tanzania sio kisiwa.
 
Mm namlaani aliyemkosa Tundu Lissu,natamani ningekuwa na uwezo,hiyo jamaa ningemmaiza mm. Angemmaliza ningeagiza soda! Namchukia huyu Tundu Lissu mpaka mwisho!
Hahahaha, wewe ni JPM au Makonda?
 
Mm namlaani aliyemkosa Tundu Lissu,natamani ningekuwa na uwezo,hiyo jamaa ningemmaiza mm. Angemmaliza ningeagiza soda! Namchukia huyu Tundu Lissu mpaka mwisho!
Kamroge, mbona tz wachawi tele..unaumia nini na wakati wazee wa tawire nambari moja kabisa duniani hko wapo..
 
Huy anatabia yakujipendekeza kwa siasa za Watanzania
Ili apate sifa kumbe Boya tu

Sijakuelewa hapa, mgombea urais wa Tanzania amehojiwa na redio ya Kenya, maana kwamba hayo mahojiano yamepeperushwa nchini Kenya, una maana nisitolee neno?
Humu huwa tunajadili hata siasa za Marekani.....
 
Hivi Lisu anataka urais wa tz au Kenya?

Maana ukiangalia hata katika hotuba zake zote hakuna inayoisha bila kutaja Kenya

Asingepelekwa Kenya Leo hii angekuwa marehemu. Anaitaja Kenya kutokana na mwelekeo wa maswali. Viruhusuni vyombo vya hapa nyumbani kumuhoji uone kama ataitaja Kenya.
 
Nahisi mikutano ya kampeni ya Lissu itazingirwa pande zote nne na mipolisi ili kuwatisha watu
 
Lissu ajielewi na hicho ndio kitu kikubwa kitakachomwangusha hata kama vyombo vya hapa havimpi nafasi bado wapiga kura wake wapo Tanzania.Toka mwanzo alivyoanza kufanya mahojiano na vyombo vya nje utaona kabisa matamshi yake hayaendani na nini wanachotaka watanzaniaa.Kuna mambo mengi ambayo watanzania wangependa kusikia toka kwake kama maswala ya pensheni za wafanyakazi na vitu vingine lakini yeye amejikita na mambo ambayo si tu hayamsaidii mtanzania bali pia hayakubariki.

Mkuu Lisu anaalikwa kwenye vipindi na hivyo vyombo vya nje, hivyo anajibu kutokana na maswali. Ni juu ya vyombo vya hapa nchini kumhoji hayo watakayo watanzania.
 
Back
Top Bottom