Tundu Lissu ameongea na Radio Citizen Kenya asubuhi ya leo, ameleezea hali ya usalama nchini pamoja na suala la Corona

Tundu Lissu ameongea na Radio Citizen Kenya asubuhi ya leo, ameleezea hali ya usalama nchini pamoja na suala la Corona

JPM katili sana, ndiye aliyebariki shambulio la Lissu kuchapwa zile mvua za risasi. Muda ukifika tutaweka wazi kila kitu.
Subiri oktoba atachapwa zile za wanachi kwenye box la kura.

Huyo Lisu wako atachanganyikiwa sana
 
Asingepelekwa Kenya Leo hii angekuwa marehemu. Anaitaja Kenya kutokana na mwelekeo wa maswali. Viruhusuni vyombo vya hapa nyumbani kumuhoji uone kama ataitaja Kenya.
Majibu ya yote haya ni oktoba
 
Lissu awe makini sana kutumia Media za Kenya maana tayari Tanzania na Kenya hatuko na maelewano mazuri.

Ningemshauri atumie Radio ujerumani na BBC hizi ni radio Neutral na zinaushawishi nchini.

Hiki kitengo cha propaganda cha CHADEMA siku hizi kimejaa vilaza watupu.

Fame aliyoijenga Lissu kwa miaka kumi anaweza kuiharibu kwa media talk ya nusu saa tu.

Sijui nani anamshauri kutumia media za Kenya

Cc.CHADEMA
Kwani za ndani anaruhusiwa kusitumia?
 
Kwani za ndani anaruhusiwa kusitumia?
Mkuu changamoto iliyopo ni kubwa na hizo za kimataifa nazo zimefungiwa rasmi.

Ila hizo za kenya awe nazo makini sana wanaweza kutumia kama fimbo ya kumchapia ukizingatia diplomatic tensions zilizopo kati ya tanzania na kenya.
 
Mbona unajihami sana mkuu?

Si ulisema Lisu ni zaidi ya tume?

Ndio, kwani tume pia nayo ni wagombea wa uchaguzi? Narudia tena, magu hawezi ushindani wa box la kura, na hatakaa aweze. Atakachofanya ni kutumia madaraka yake kunajisi uchaguzi huu.
 
CCM ni Tanzania na Tanzania ni CCM kwa hiyo lazima Rais awe wa chama hicho Wananchi Watanzania wapende wasipende....North Korea ya Afrika.
 
Lissu aachane na hii hoja ya corona haitamsaidia.

Ukweli ni kwamba wananchi wengi wamemuelewa sana rais jinsi amedeal na issue ya corona, sasa Lissu akipuyanga kwenye hilo atapoteza mvuto.
 
Ukweli ni kwamba wananchi wengi wamemuelewa sana rais jinsi amedeal na issue ya corona, sasa Lissu akipuyanga kwenye hilo atapoteza mvuto.
Hilo suala la corona Lissu anapaswa kuwa nalo makini sana.
 
Tanzania mko level nyingine bana, mnavunjiana nazi milangoni mpka sasa..
Dar ndio the most developed city in tz na bado watu wanarogana..noma sana

Mastaa nao hawajaachwa nyuma, ni mwendo wa kurogana..viongozi serekalini we acha2
Unaroga nao?
 
Nimesikiliza Mahojiano kwa njia ya simu leo jumatatu 10/8/2010 kati ya Lissu na Citizen Radio kenya kwa jinsi Lissu alivyojibu hoja na kutolea maelezo ya kutosha, nashawishika kuwa sio dk. Slaa wala Lowassa hakuna anayefikia uwezo wa huyu bwana.

Kwanza anatema POINT zenye ukweli ambao ni Jinai kwenye awamu hii ya tano, Point zinazochoma mithili ya pasi na ukweli wenye kuumiza na kutafuna moyo taratibu.

Jamaa ni intelligent, focused, determined, fearless and Audible pia anahoja haongei kama mtu anayetoka povu kama Slaa au anayenongoneza kama Lowasa, Big up Lissu.

Twende na Lissu

Unaweza kusikiza hapa

 
Kama kanuni za uchaguzi zinazuia kutukanana .......... Mbona Lowassa alitukanwa sana 2015 na hatukusikia mtu alilalamika kuwa kanuni zinavunjwa!!
Wapambe siyo wagombea; iwapo wapambe wa CCM ndio walikuwa wanamtukana wao siyo wagombea na wala tume haishughuliki nao. Tatizo ni pale mgombea mwenyewe ndiye anayerusha matusi.
 
Back
Top Bottom