Pre GE2025 Tundu Lissu amteua John Mnyika kuwa Katibu Mkuu. Ateua Manaibu Katibu Wakuu na Wajumbe wa Kamati Kuu
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwenyekiti mpya wa Chadema, Tundu Lissu amempendekeza kwa Baraza Kuu la chama hicho, John Mnyika aendelee kuwa Katibu Mkuu.

Lissu pia amemteua Aman Golugwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Tanganyika (Tanzania Bara)

Wakili Ally Ibrahim Juma ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar

Uteuzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu
1. Godbless Lema
2. Dkt. Rugemeleza Nshala - Mwanasheria Mkuu wa Chama
3. Rose Mayemba

View attachment 3210393
Aman Golugwa​


View: https://www.youtube.com/live/n57Tc7XtINo


Safi kwa Mnyika.

Nshala hamna kitu.
 
Wajumbe wateule

Lema na tege lake
Screenshot_20250122-191552.png
 
Pole sana kwa walutheri wakiwemo askofu Shoo na Bagonza na waprotestant akina Askofu Mwamakula na walokole akina Askofu Mwanamapinduzi chama chenu cha Chadema wakatoliki wamechukua hatamu za chama kiko chini ya wakatoliki Lisu na Mnyika

Pole ziwafikie pia chama cha Christian Democrstic Union cha Ujerumani baba mlezi wa hiari wa Chadema kwa miaka nenda rudi
 
Safi sana naona kamati ya roho mbaya inazidi kukamilika.
Naomba Mheshimiwa mwenyekiti GODLESS LEMA awe MKURUGENZI WA ITIKADI NA UENEZI WA CHAMA.
HAPO KAMATI YA ROHO MBAYA KWA MAFISADI ITAKUWA IMEKAMILIKA KUWAPELEKEA MOTO WALE NZI WA KIJANI.
100%
 
..nilitegemea Catherine Ruge awe Naibu Katibu Mkuu.

..maadam amechaguliwa mwingine ningefurahi kama atateuliwa kuwa mmoja wa wakurugenzi wa sekretariet.
 
Mwenyekiti Mpya wa CHADEMA ndg Tundu Antipas Lisu amependekeza jina la John John Mnyika kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Baraza Kuu la CHADEMA wamepitisha pendekezo hilo huku wajumbe watatu wakishikilia msimamo wa kutomkubali.

Viva CHADEMA
wajumbe wamepata posho zao?
 
Mwenyekiti mpya wa Chadema, Tundu Lissu amempendekeza kwa Baraza Kuu la chama hicho, John Mnyika aendelee kuwa Katibu Mkuu.

Manaibu Katibu Mkuu
1. Aman Golugwa - Naibu Katibu Mkuu Tanganyika (Tanzania Bara)
2. Wakili Ally Ibrahim Juma - Naibu Katibu Mkuu Zanzibar

Uteuzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu
1. Godbless Lema
2. Dkt. Rugemeleza Nshala - Mwanasheria Mkuu wa Chama
3. Rose Mayemba
4. Salima Musa Kasanzu

View attachment 3210393
Aman Golugwa​


View: https://www.youtube.com/live/n57Tc7XtINo

Moving the right direction 💪🏿🙏🏿👌🏿
 
😂😂😂TL anaogopa Mabadiliko.

Angetakiwa aanze upya na sura mpya 😂😂
 
Back
Top Bottom