Pre GE2025 Tundu Lissu amteua John Mnyika kuwa Katibu Mkuu. Ateua Manaibu Katibu Wakuu na Wajumbe wa Kamati Kuu
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nafasi moja ya Mjumbe kati ya zile sita kutoka kwa Mwenyekiti ni nafasi Ya Mzee Slaa...
 
..nilitegemea Catherine Ruge awe Naibu Katibu Mkuu.

..maadam amechaguliwa mwingine ningefurahi kama atateuliwa kuwa mmoja wa wakurugenzi wa sekretariet.
Nakuunga mkono kabisa. Pale juu alihitajika mwanamke. Catherine Ruge angefaa sana kwenye nafasi ya NKM. Au hakuwa upande pendwa?

Amandla...
 
Catherine Ruge aliteleza, mwanzoni alikuwa neutral baadaye dakika za mwisho akawa timu Mbowe, akaharibu.
Kama ni kweli, hakuharibu. Alionyesha kuwa ni mtu mwenye msimamo. Mimi nadhani alikuwa timu Lissu. Kuna watu waliteleza wakamtaja wazi kuwa ni timu Lissu. Na Bawacha ni ya Mbowe. Anastahili heshima kama yule binti mpambanaji wa Dodoma. Lakini kama mnataka watu mfano wa Hilda....

Amandla...
 
Lissu amtafutie kitengo Lema.
Jamaa mtu muhimu sana..
Lissu hawezi kumtupa Lema; ni mtu muhimu kwake na kwa Chadema.
Lissu hana budi kuwa muangalifu na Ansbert Ngurumo na ushauri wake wa kichochezi kwa chama!
 
Hivi ktk wale COVID 19 Mke wa Salim Mwalimu ni yupi ,wa Ben Kigaila je?
 
Nakuunga mkono kabisa. Pale juu alihitajika mwanamke. Catherine Ruge angefaa sana kwenye nafasi ya NKM. Au hakuwa upande pendwa?

Amandla...

..kuna mahali hapa JF nilisikia Ruge alikuwa upande wa TL.

..lakini Ruge ndio alikuwa engine, na msemaji wa Bawacha, tangu maasi ya wanawake 19.

..kwa maoni yangu sio busara kuacha kutumia uwezo na kipaji chake kukitumikia chama.
 
Mwenyekiti Mpya wa CHADEMA, Tundu Lissu akiwa kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Chama ambalo limekutana leo Jumatano, Januari 22, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ameanza kupanga safu yake ya uongozi kwa Kuteua Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu.

Mh. Tundu Lissu amefanya uteuzi kama ifuatavyo

Katibu Mkuu
1. John John Mnyika

Manaibu Katibu Mkuu
1. Aman Golugwa - Naibu Katibu Mkuu Tanganyika (Tanzania Bara)
2. Wakili Ally Ibrahim Juma - Naibu Katibu Mkuu Zanzibar

Wajumbe wa Kamati Kuu
1. Godbless Lema
2. Dkt. Rugemeleza Nshala - Mwanasheria Mkuu wa Chama
3. Rose Mayemba
4. Salma Musa Kasanzu
5. Hafidh Ally Salehe

Pia soma
- Freeman Mbowe akubali kushindwa, awapongeza Lissu na Heche kwa ushindi

Trump wetu yuko faster mara hii kashateua Katibu mkuu!
 
View: https://www.youtube.com/live/n57Tc7XtINo

Viva chadema viva!
 
Kama ni kweli, hakuharibu. Alionyesha kuwa ni mtu mwenye msimamo. Mimi nadhani alikuwa timu Lissu. Kuna watu waliteleza wakamtaja wazi kuwa ni timu Lissu. Na Bawacha ni ya Mbowe. Anastahili heshima kama yule binti mpambanaji wa Dodoma. Lakini kama mnataka watu mfano wa Hilda....

Amandla...
Sultan Mbowe amesha BWAGWA, bado unasumbuka na nini wewe?
 
Back
Top Bottom