Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mgombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa na makamu mwenyekiti anayemaliza muda wake, Tundu Lissu, amemteua Godbless Lema kuwa wakala wake katika uchaguzi unaofanyika leo.
Kuteuliwa kwa Lema, ambaye si mjumbe wa mkutano mkuu kwa sasa, kumetangazwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, leo Jumanne, Januari 21, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
"Nimepokea barua toka kwa Tundu Lissu akimchagua Godbless Lema kuwa wakala wake kwenye uchaguzi Mkuu, Miongozo ya katiba inamruhusu" - John Mnyika
Akitoa tangazo hilo muda mchache kabla ya uchaguzi huo kuanza, Mnyika amesema suala hilo halivunji kanuni za uchaguzi.
Soma, Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA nafasi ya Mwenyekiti & Makamu Mwenyekiti 2025: Ni Mbowe au Lissu?