Pre GE2025 Tundu Lissu amteua Lema kuwa wakala wake uchaguzi CHADEMA

Pre GE2025 Tundu Lissu amteua Lema kuwa wakala wake uchaguzi CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mgombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa na makamu mwenyekiti anayemaliza muda wake, Tundu Lissu, amemteua Godbless Lema kuwa wakala wake katika uchaguzi unaofanyika leo.
View attachment 3209003
Kuteuliwa kwa Lema, ambaye si mjumbe wa mkutano mkuu kwa sasa, kumetangazwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, leo Jumanne, Januari 21, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

"Nimepokea barua toka kwa Tundu Lissu akimchagua Godbless Lema kuwa wakala wake kwenye uchaguzi Mkuu, Miongozo ya katiba inamruhusu" - John Mnyika

View attachment 3209007
Akitoa tangazo hilo muda mchache kabla ya uchaguzi huo kuanza, Mnyika amesema suala hilo halivunji kanuni za uchaguzi.

Soma, Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA nafasi ya Mwenyekiti & Makamu Mwenyekiti 2025: Ni Mbowe au Lissu?
Lema lazima atazua uongo baada ya Lissu kushindwa.

Lema ni mnafiki, laghai na mchonganishi.
 
Uchaguzi wa mwaka huu upo wazi sana kwa wajumbe Wala hauna ugumu wowote wa kujiuliza wamchague nani, kitendo Cha mbowe kuungwa mkono na CCM hiyo ilitosha kumchinja mbowe bila kumuangalia usoni.

Siku zote CCM hawependi watu strong wenye misimamo, CCM wanapenda watu walegevu wenye misimamo ya kuyumba yumba ndio maana CCM wote wameungana na mbowe. Wajumbe mkimchagua mbowe mjue mmechagua kibaraka wa CCM na mmewasaidia kazi kubwa ya kimkakati kazi kwenu.
 
Sisi tunaangalia, maamuzi ni yao kutupatia ujumbe kama wapo serious na mabadiliko au wanatamani kujiunga na vyama 14 marafiki wa CCM na kufanya idadi yao ifikie 15.
tunaomba hao wajumbe wapiga kura wasiigeuze CHADEMA kuwa chama cha 15 marafiki wa CCM. Tunataka chama cha upinzani wa kweli
 
Finally, Mbowe kaliwa kichwa ama hakika CHADEMA wameamua ku appy UBAYA UBWELA.
 
Kwa jicho pevuu huu uchaguzi una ngumi hapo baadae kama sahivi tu kwenye kuhakiki majina watu wanazozana hivi asbuhi wapiga kura walitangazwa kuwa906 kufikia sahivi idadi imepiga u turn ni1007 Mpaka matokeo kutangazwa jumla ya kura ni2000
Tuonyeshe hizo Ngumi Mzee
 
Back
Top Bottom