Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amuunga mkono Maalim Seif Urais Zanzibar

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amuunga mkono Maalim Seif Urais Zanzibar

ACT wazalendo haiwezi Ingia Mtego wenu wa kitapeli ambao hayuko hata kisheria maamuzi kama Hayo hufanywa na kamati kuu ya chama na mkutano mkuu .Lisu kajitamkia tu hana back up ya kamati kuu wala mkutano mkuu na hakuna minute za kikao chochote cha Chadema kilichotamka hivyo!!
Hii habari imekuwa ni mwiba mkali mno kwa CCM, sasa ni dhahiri CCM watumie uzoefu wao kumwomba msaada Bernard na Zitto waokoe jahazi kitu ambacho si chepesi.
 
Lissu ni mwanasheria anayeheshimika, lakini kwahili la jana nimepata mashaka kidogo kalifanya kienyeji mno.

Chadema ni taasisi iliyosajiliwa na inaendesha mambo yake kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu, sasa hili la kuachiana ugombea na ACT mlikubaliana lini? MoU iko wapi? Lissu kama mwanasheria wa chama hebu tuambie ni kikao gani kilichokaa mkakubaliana kumwachia maalimu saif Zanziber?...
Maswali hayo hayo waulize tlp na nccr ambao wamemtangaza Magufuli kua mgombea wao....

Lissu atawafumua sn mwaka huu... Magufuli labda ataambulua 10% watz wanataka mabadiliko kila mahali sio kanda ya ziwa wala kati sio kaskazini wala kusini wote hawataki kusikia takataka za ccm
 
Subiri kimbunga na Chadema na ACT wana mikakati mizito.
Usijipe matumaini hewa. Hakuna huo mpango. Wagombea wote wameshapoteza hela zao kwa sasa sahau.

CHADEMA haijwahi kuwepo Zanzibar na hapo ndio maana Lissu kaona aunge tu mkono.
 
Ndugu zangu,

Baada ya kuusoma upepo Zanzibar Lissu abadili gia angani badala ya kumnadi mgombea urais wa CHADEMA amemnadi Maalim Seif.

Muda unatoa majibu sasa.


Kwani nyie uliona vibaya kuungwa mkono na akina Cheyo na Mrema?
 
Kwani nyie uliona vibaya kuungwa mkono na akina Cheyo na Mrema?
Wale walikaa vikao vya vyama kuamua kuunga mkono mgombea wa CCM

Hakuna kikao cha Chadema kilikaa kutengua uteuzi wa mgombea uraisi Zanzibar kupitia chadema na kuamua kuwa kinamuunga mkono Maalim Seif

Hatukatai kufunga mkono lakini wanachama maamuzi yao ni muhimu kupitia vikao vya kamati kuu na mkutano mkuu ndicho tunahoji .
 
Mh. Lissu kweli anatisha! Yaani hata yale yaliyofyatuliwa kwenye mikesha ya mwenge yanafuatilia yanayojiri huko Zanzibar! Ulitaka Mh. Lissu amnadi nani huko Kisiwani?
Itakuwa alitaka amnadi mwinyi
 
Usijipe matumaini hewa. Hakuna huo mpango. Wagombea wote wameshapoteza hela zao kwa sasa sahau.

CHADEMA haijwahi kuwepo Zanzibar na hapo ndio maana Lissu kaona aunge tu mkono.
Tuliza mshono dogo, mambo ya siasa waachie mabosi wako kina chakubanga ndiyo wanao jua ukweli.

Safari hii ccm ndiyo bye [emoji112]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maswali hayo hayo waulize tlp na nccr ambao wamemtangaza Magufuli kua mgombea wao....

Lissu atawafumua sana mwaka huu... Magufuli labda ataambulua 10% watz wanataka mabadiliko kila mahali sio kanda ya ziwa wala kati sio kaskazini wala kusini wote hawataki kusikia takataka za ccm
Nakuunga mkono kwa 100%, watanzania wanahitaji mabadiliko na CCM haina nafasi tena mioyoni mwa Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom