Tundu Lissu amvua nguo Lijualikali

Tundu Lissu amvua nguo Lijualikali

Madai ya kwamba Lijuakali alipata ubunge kwa juhudi zake ni uongo , Chadema ndio iliyompigania hadi akafanikiwa kuwa mbunge , Tundu Lissu anadai kwamba hata mwaka 2013 Lissu alimpigia kampeni lijuakali kuwa diwani wa Ifakara kwa gharama zake

Tundu Lissu anadai kwamba Baba yake mzazi Lijuakali ni shahidi wa namna Lissu alivyomtoa mtoto wake jela baada ya kufungwa kwa uonevu kwa lengo la kuvuliwa ubunge .

Mh Lissu anadai kwamba hela za chama cha siasa ni pesa za umma , na hukaguliwa na CAG na mahesabu yake hupelekwa kwa Msajili wa vyama vya siasa , Kwahiyo Tuhuma za Lijuakali kwamba hela za michango ya wabunge zinaliwa zinapaswa kupuuzwa , bali inafahamika kwamba kila anayeondoka Chadema kwenda CCM A ama kwenda CCM B hutoa tuhuma zilezile za miaka nenda rudi ili kuwaridhisha waliomtuma .
Ni kweli hela za vyama hukaguliwa na CAG, ndiyo maana ripoti za CAG za mwaka 2017, 2018 na 2019 zinaonyesha kuwa hela za vyama vya siasa zimekuwa zinatumika kinyume cha sheria.
 
Lissu ameshuka chati,kutoka kubishana na Magufuli mpaka kubishana na juakali
 
Kumbe kweli CHADEMA ilimpigania Lijualikali hadi akafanikiwa kuwa mbunge kama alivyosema mwenyewe namba zilichezewa kwenye ujumulishaji kura za wabunge.

Mengine wana CDM kausheni yule kijana anamwaga mboga mwanzo mwisho. Inaitwa ninyime ugali nimwage mboga, au niguse ninuke.

Sema Lijualikali nae kajiharibia sana kwa kufunguka mambo yale.

Huku Silinde, kule Lijualikali na pale Peter Msigwa, jahazi linapigwa mawimbi kila kona.
Huu mwaka wa mateso sana kila upande.

Episode moja baada ya nyingine vyama vyote. Coronavirus kaja kuchochea moto.
Miezi michche iliyopita CDM walikuwa wanashangilia tamthilia ya CCM na jasusi my uncle Bernad.
Ana tuhuma zishizo na ushahidi chadema kifanye uhuni msajili awe ana kiangalia tu
 
Lijualikali kajidhalilisha sana
Madai ya kwamba Lijuakali alipata ubunge kwa juhudi zake ni uongo , Chadema ndio iliyompigania hadi akafanikiwa kuwa mbunge , Tundu Lissu anadai kwamba hata mwaka 2013 Lissu alimpigia kampeni lijuakali kuwa diwani wa Ifakara kwa gharama zake

Tundu Lissu anadai kwamba Baba yake mzazi Lijuakali ni shahidi wa namna Lissu alivyomtoa mtoto wake jela baada ya kufungwa kwa uonevu kwa lengo la kuvuliwa ubunge .

Mh Lissu anadai kwamba hela za chama cha siasa ni pesa za umma , na hukaguliwa na CAG na mahesabu yake hupelekwa kwa Msajili wa vyama vya siasa , Kwahiyo Tuhuma za Lijuakali kwamba hela za michango ya wabunge zinaliwa zinapaswa kupuuzwa , bali inafahamika kwamba kila anayeondoka Chadema kwenda CCM A ama kwenda CCM B hutoa tuhuma zilezile za miaka nenda rudi ili kuwaridhisha waliomtuma .

In God we Trust
 
Kuna vijana wasingekaa wakawa wabunge au hata udiwani tu katika maisha yao... Chadema imewasaidia kutimiza ndoto zao. Leo wanatumika kusema uongo, uzushi, unafiki na uzandiki dhidi ya viongozi waliojenga taasisi iliyowapa heshima. Kwasababu ya vipande 30, Tuwe na akiba ya maneno
 
Mbowe rudisha billion 8 ulizoibia wabunge

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi inawezekana MTU mmoja akatafuna TSH 8bn na wadau waliomzunguka wanahesabu kuanzia shilling 100 Hadi zinafika 8bn?..kama ni kweli tatizo hapa sio Mbowe, tatizo ni kamati kuu ambayo ndio watchdog wa Mali za chama na wenye uwezo wa kumdhibiti Chairman.. wengine wata argue hapa kwamba wanazidiwa mbinu na Mbowe but nadhani pamoja na brilliance zake still watu anaowaongoza Wana matatizo.(kama yanayoelezwa Yana chembe za ukweli)
 
Kuna vijana wasingekaa wakawa wabunge au hata udiwani tu katika maisha yao... Chadema imewasaidia kutimiza ndoto zao. Leo wanatumika kusema uongo, uzushi, unafiki na uzandiki dhidi ya viongozi waliojenga taasisi iliyowapa heshima. Kwasababu ya vipande 30, Tuwe na akiba ya maneno
Watalipwa kwa kadri ya matendo yao
 
Back
Top Bottom