Tundu Lissu ana Mali au biashara anazomiliki hapa nchini? Viko wapi vitega uchumi vyake?

Tundu Lissu ana Mali au biashara anazomiliki hapa nchini? Viko wapi vitega uchumi vyake?

Kama ni kweli barrick ndio walimjengea itakua walimhonga.
Si huyu lissu anayesiifiwa kwa kupambana na wawekezaji kutetea wachimbaji wadogowadogo waliyokua wanadhulumiwa ardhi na fidia zao na wawekezaji wakubwa kama barrick? Kumbe mnafiki mkubwa
Alikuwa mtetezi kabla hajafika bei. Walimnunulia hadi Range na magari kadhaa BIG HORN ambayo yalimsaidia kupata Ubunge
 
Hizo tozo na mikopo mnayolalamikia kila siku viko mbinguni au Chadema???Umeme kukatika mara kwa mara ni pazuri na chi ya maziwa na asali??Umbumbumbu na upumbavu vinawaponza nchi inaendelea kuuzwa uarabuni nyie mmekalia nchi ya maziwa na asali,shit kabisa.
Tozo na mikopo zinafanya makubwa, bwawa la Nyerere tayari lishajazwa maji, sgr dar to Moro this January unaanza kupiga mzigo, makandarasi pia wametapakaa vipande vya Moro to makutupori Dom, Dom to tabora, tabora to mza via isaka huko kote makandarasi wanachapa kazi, madarasa na zahanati zinachipuka kama uyoga, hizo ndo return za tozo na mikopo, nchi hii iko pazuri jamani, Mama anautandika mwingi.
 
Acha kupotosha, Lissu alikimbia nchi miaka ya 2000 sababu ya kusakwa na hao watorosha madini. Kuna kitabu kaandika kinaonyesha jinsi tunaibiwa kupitia sheria zetu so amewindwa sana akiwa LEAT Sasa kivipi Tena awe anategemea pesa zao? Kama angetaka hayo si angekua mwanasheria wao rasmi azoe mabilion why aende kwenye siasa??

Msidhani Kila mtu anaongozwa na tumbo, JPM kwenye kampeni alikiri Lissu ni mwanasheria mahiri Hadi akaahidi asigombee Urais ampe cheo!! Ndio sembuse wewe hoehae!!?
Wanaotorosha madini ni mababeru alafu akakimbilia kwa mabeberu kuwakimbia mabeberu?
 
Yes umesema kweli kuwa hana uvumilivu na ufisadi atakulipua tu😅
Lissu anafaa tu kuwa mwanaharakati ila sio siasa. Zile jazba zake za kijinga hazifai kabisa kwenye siasa. Ni mtu wa visasi.
 
Wanaotorosha madini ni mababeru alafu akakimbilia kwa mabeberu kuwakimbia mabeberu?
Sasa umesikia mabeberu wote Wana akili Moja au wanamiliki mgodi mmoja? Funny enough wanaokuja kukuua sio weupe ni weusi wenzetu ambao waligawa mikataba mibovu kwa wazungu mfano Mwanyika alituingiza hasara ya matrillion kupitia Barrick ila CCM mmempa ubunge!!
 
Kutokana na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Viongozi wote huwa Wana Kiri Mali na madeni yao Kila Mwaka kwa Kujaza Fomu maalumu ya Kiapo.

Nadhani ungeanzia hapo, ungeweza kupata taarifa zote za Mali pamoja na Madeni ya Mhe. Tundu Lissu
 
Kama ni kweli barrick ndio walimjengea itakuwa walimhonga. Si huyu Lissu anayesiifiwa kwa kupambana na wawekezaji kutetea wachimbaji wadogowadogo waliyokuwa wanadhulumiwa ardhi na fidia zao na wawekezaji wakubwa kama barrick? Kumbe mnafiki mkubwa
Yaani wewe wala hautumii akili ni sehemu gani hapa tegeta kuna nyumba ya lissu?
 
Wanasiasa kama Lissu naelewa siyo wafanyabiashara, hawana maono yakumiliki Mali, siyo wezi na wameumbwa kupambana wakati wote na matajiri.

Lakini pamoja na ukweli kwamba siyo watu wa kujilimbikizia Mali upo umuhimu wa kufahamu anamiliki nini hapa nchini? Anamiliki kampuni gani? Ana ukwasi kiasi gani?

Tunajiuliza haya maswali Kwa Sababu yeye mwenyewe NI muumini wa kulazimisha watu kuweka wazi taarifa zao za Mali; wapi tutapata taarifa zake za Mali anazomiliki?

Mwisho tukijua Mali anazomiliki tutajua kama atarejea nchini hivi karibuni kuendelea na siasa au ataendelea kibali huko ulaya nakufanya kazi zakumwezesha kulipa gharama za kuendesha familia.

Chawa WA CHADEMA tuambie mgombea Urais wenu ana ukwasi kiasi gani?
Mbona alisjakabidhi fomu ya kiapo cha mali zake wakati wa Kugombea urais? Nenda kamati ya maadili utazikuta taarifa zake.
 
Back
Top Bottom