Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ana marafiki wa kificho, Rais Magufuli ana maadui wa kificho

Marafiki kificho wa Lissu wapo ccm na watampigia kura lissu lkn huku wakiwa wamevalia magwanda ya kijani huku wakiimba ccm nambari one.
Marafiki kificho wa Lissu hawapi Kura, na Maadui kificho wa JPM hawapigi Kura.
mlinganyo unabalansia hapo tu.
 
Umesahau kitu kimoja muhimu nacho ni kuwahimiza watanzania woote wnawake kwa wanaume, vijana wote wenye sifa za kupiga kura siku ya kupiga kura wajitokeze wakampigie kura Tundu Lissu.
 
Hawezi kabisa kumpigia kura, kuna walio tumbuliwa kisa hawana vyeti, kuna wategemezi wao hao wote kamwe hawawezi kumpigia kura jiwe.

Kuna wakulima wa korosho hawawezi kumpigia kura jiwe
Mkuu hao marafiki wa kificho na maadui wa kificho wengi wao wanajitambua ndo kundi linaloenda kupiga kura kwa hasira, na hawawez kukosa kupiga kura, kwa akili ya kawaida iv kinana anaweza mpigia kura jiwe
 
Kumbukeni wengi walisusia kwenda ku update data zao za kadi za kupigia kura
 
Ndugu. Naona umejitahidi kujenga hoja lakini umesahau kujua hoja na vioja. Hoja kazitoa jana Ndugu magufuli. Na Amejenga hoja vizuri sana na hoja zake zinauzika kwa wananchi walio wengi.

Sasa chadema wasitegemee uruma za wananchi Bila kuwaambia wananchi hoja mufilisi.

Huwezi kudharau hata kidogo kazi iliyofanyika kwa kuwambi wananchi mmenyimwa haki ya kufanya mikutano na kutaka katiba mpya wakati wananchi wanataka kusikia na kuona. Barabara za uhakika. Umeme. Maji. Dawa maosptaĺini. Na shule kuboreshwa. Kudhibiti Ufisadi.

Alafu wewe unakuja kubeza majukwaani na kuwambia wananchi katiba na uhuru wa kuongea na kufanya mikutano. Hapo utaambulia patupu kamanda.

Kimsingi chadema na upinzani mkubalitu Hakuna wa kumpiku magufuli kwa utendaji uo ndio ukweli. Na ilo wanalitambua shida yao ni kutaka ikulu huku wakijua uwezo hawana.
 
Kama umeniona vile kwani nilisusia ku update kitambulisho
Ku update ni kwa wale waliohama makazi kumaanisha kama mwaka 2015 ulikuwa moshi na mwaka 2020 Uko Pwani basi unaenda ku update kama umehamia Pwani na Kura utapigia Pwani. So haikuzuii kurudi kituo ulichopigia kura mwaka 2015 kama kweli una kadi ya mpiga kura.
Mwaka 2015 nilikuwa Njombe na nilipigia kura njombe, mwaka huu Nipo Songea na sikuupdate kuwa nimeamia Songea. Hivyo October 2020 nitarudi Zangu Njombe kupiga kura pale nilipopigia 2015.
 
Tuwekee tu wazi maadui wakubwa wa huyo bwana Sasa watakuwa
1. Walifukuzwa kazi sababu ya vyeti feki. Hao piga ua hawatoi kura CCM
2. Wenye kusaka ajira Hawa nao piga ua hawatoi kura CCM.
3. Waliobomolewa makusudi kupisha barabara au miradi mwingine, Hawa na chuki Kama Nini hawatatoa kura CCM
4. Waliobambikiwa vyesi na kusekwa ndani kufunguliwa vyesi uhujumu uchumi, Hawa Kama mbogo hawatoi kura CCM
5. Wanafunzi waliosajiliwa na kupunjwa mikopo na wale waliokosa kabisa au waliotoa kitu kidogo kupata, Hawa mmmmmm Ni kwa Lissu tu
6. Wastaafu wote waliopunjwa mafao na ambao bado wanasota, kura hizi zitaenda kwa Lissu
7.Watumishi wote walimsikia bwana mkubwa akisema kuwa hakuchaguliwa ili aongeze mishahara, Hawa hawatoi kura CCM
8. Wafanyakazi na wamiliki wa vyombo vya habari walinyanyaswa kufungiwa vyombo vyao na kufungwa wao, familia na wao hawatoi kura CCM.
9. NGOS zilizopigwa ban Hawa na familia zao kutoa kura CCM Ni sawa na kuweka mkono kwenye mdomo wa mamba.
Nasema watanzania kwa mamilioni hapa ndipo wataonyesha ukarimu wao kwa Lissu
 
Mkuu ubarikiwe kwa bandiko murua kabisa. Ntakupa tuzo
 


kujiamini kupita kiasi ni dhambi, anaepita hapo anajulikana huyu mwingine nadhan mtumie mda mfundishe jinsi ya kuongea na wananchi, baada ya uchaguzi mtajua mtego mwingine ccm waliokua wamewategea! as always
 

Hapo sawaaa kabisa sijahama
 
Eti asilimia 70! Unawajua watanzania wewe lissu hana ushawishi wowote mbele ya Magufuli ambaye kazi zake zake zinaonekana kwa vitendo!. Endeleeni kujifariji tu humu Jf ilauo ndo ukweli mchungu.!. Lissu na wapinzani wengine watatoa changamoto tu ila hawawezi kushinda Urais never! ,Hilo hata wapinzani wanalijua . Yaani mnashindana na chama ambacho kimejiekea mizizi toka kwenye mashina/matawi huko kuanzia vijijini hadi mijini , chama chenye rasilimali fedha sa kutosha kuendesha kampeni ,alafu simply tu unakuja hapa eti lissu atashinda 70% unawajua watanzania wewe..!
 
Yupo mgomea anaedhani wapiga kura wanatumia akili za kuvukia barabara hawawezi hata kuyatambua maneneo ya kinafiki
 
Umesahau. Yupo mgombea anayeungwa mkono na kupendelewa na marefa, maadili na sheria za uchaguzi, vyombo vya dola, na mahakama; dhidi ya mgombea anayeungwa mkono na kuhurumiwa na wapiga kura.
Kwa utafiti upi ? Mgombea yupi ana hurumiwa na wapiga kura?? Unafikili kupigwa risasi ndo kutampa huyo mtu wenu Urais?.. Never sio kwa Tanzania na watanzania sio wajinga kiasi hicho!.
 
M
M
Mmmmmmhh
 

Chadema wakimudu kusimamia kura zote kwa uhalali isipotee hata moja, hakika LISSU atashinda kwa 70%.
Kuna changamoto kubwa sana ya mawakala wetu, wengi wanaendeshwa na njaa hivyo anaweza uza ushindi wa jimbo au kura za kituo kizima kwa sh, milioni 2 tu. Hili ni tatizo kubwa sana, linahitaji dawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…