Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ana marafiki wa kificho, Rais Magufuli ana maadui wa kificho

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ana marafiki wa kificho, Rais Magufuli ana maadui wa kificho

Ninampa Lissu asilimia 70 za kumshinda Magufuli. Hakuna namna, narudia tena, hakuna namna Magufuli anaweza kumshinda Tundu Lissu mwaka huu. Wengi wapo na magufuli usoni ila moyoni wanajua wapo na Lissu. Kama Kuna kura za maruhani mwaka huu ndo atakazoziona magufuli.

Kikubwa Chadema na Lissu wajipange tu. Waandae timu imara na madhubuti ya kumuongoza Lissu kwenye Kampeni. Kumuongoza kwenye hoja za kupiga na namna za kupiga. Hakuna uchaguzi mzuri kwa chadema Kama wa mwaka huu!!
Sidhani kama PM au VP, kinana makamba,watampa kura
 
Umemaliza na umepiga mule mule kunakouma.Wanatuona wajinga?Mzee Butiku kamaliza,amepiga nyundo za utosi pale kwenye mkutano wa NCCR Mageuzi.Watanzania wanataka kuthaminiwa UTU wao,watendewe kwa USAWA na wapate HAKI zao bila ubaguzi.
Wapinzani wameaswa kuunganisha nguvu zao kwa pamoja ili kuiondoa CCM mpya madarakani na tuepuke UWOGA.
Tutumie nafasi adhimu ya uchaguzi mkuu tuibadili Tanzania yetu ili Taifa hili lijengeke.
Yule mzee atafanyiwa figisu pale nyerere foundation. Huyu jamaa sio binadamu
 
uchambuzi murua nkaribu hapa kikuyu tunapanga mipango ya kesho.
 
Nakumbuka weekend ile zilitapakaa habari za jamaa mmoja kuwa amezungukwa na wingu la mauti namna lilivyojaza bashasha kwenye nyuso za watu.
 
Mkuu hao marafiki wa kificho na maadui wa kificho wengi wao wanajitambua ndo kundi linaloenda kupiga kura kwa hasira, na hawawez kukosa kupiga kura, kwa akili ya kawaida iv kinana anaweza mpigia kura jiwe

Aisee...

Hili swali,

"...Hivi Kinana au Nnape Moses Nauye ama Makamba Jr na Sr kwa pamoja wanaweza kumpigia kura Jiwe...?"

ni zuri sana....

Wanaweza kumpigia kama kura ni ya wazi kwa kupanga foleni nyuma ya mgombea au kama kura ni ya kunyoosha mikono/vidole juu....!!
 
UCHAGUZI wa mwaka huu unatakuwa ngumu na wenye mvuto mkali. Hii ni sawa na pambano lililosubiriwa kwa muda mrefu.

Mapambano kama haya yakitokea hulazimisha shughuli zingine zisimame ili kupisha mpambano mkali na wenye mvuto.

Hivi ndiyo ninavyoona uchaguzi wa mwaka huu. Siyo uchaguzi wa CCM VS CHADEMA. Ni uchaguzi Kati ya Tundu Antipus Lisu na John Pombe Magufuli.

Kwa sababu ya upekee huo, uchaguzi wa mwaka huu hautaamliwa kwa kushindanisha sera za wagombea, bali utaamliwa kwa kushindanisha sifa za wagombea.

Hapa Kuna aina mbili za wagombea. Yupo mgombea mwenye uchovu mwingi dhidi ya mgombea mwenye shauku nyingi.

Yupo mgombea mwenye kuitawala dhamiri yake mwenye dhidi ya mgombea mwenye kufungwa na dhamiri yake mwenyewe.

Yupo mgombea anayependa kuwatisha wenzake dhidi ya mgombea asiyezoea wala kuogopa kutishwa!

Yupo mgombea anayejua matatizo yetu hata kama hatujayasema dhidi ya mgombea anayependa kuahirisha matatizo yetu hata kama tumeyasema hadharani.

Yupo mgombea anayehisi na kuamini kwamba baya lolote likitokea ni hujuma za ndani au nje ya nchi dhidi ya mgombea anaye tambua kuwa makosa yetu ya kimfumo na kitaasisi ndicho chanzo kikuu cha mabaya tunayoyapata.

Yupo mgombea anayeamini hawezi kukosea, na akikosea husingizia wasaidizi wake au watangulizi wake dhidi ya mgombea anayeamini binadamu hatujakamilika, na kufanya makosa ni kuukamilisha utukufu wa MUNGU wetu aliye wema Sana.

Yupo mgombea anayeamini kuwa kila baya ni la watangulizi wake dhidi ya mgombea anayetambua mchango wa kila mtu katika ujenzi wa TAIFA letu. Uongozi ni pamoja na kurithi makosa ya wenzako.

Yupo mgombea mwenye uwezo wa kujenga nchi dhidi ya mgombea mwenye uwezo wa kujenga taifa.

Yaani ujenzi wa miundombinu mingi, sio ujenzi wa taifa. Kuna barabara zingine zinajengwa bila sababu. Nyingine zinaelekea makaburini.

Yupo mgombea anayechukia wakosoaji dhidi ya mgombea anayechukia makosa.

Yupo mgombea anayetenda anasema kila kitu dhidi ya mgombea anayetenda hasemi.

Yupo mgombea mwenye kumbukumbu nyingi kuliko ndoto dhidi ya mgombea mwenye ndoto na maono mengi kuliko kumbukumbu.

Yupo mgombea mwenye marafiki wengi wa kificho dhidi ya mgombea mwenye maadui wengi wa kificho!
Marafiki wa kificho ni wale wanakuunga mkono bila wewe kuwajua. Wapo tayari kulala njaa ili wewe ule na ushibe!

Maadui wa kificho, ni wale ambao wanakuunga mkono unapokuwepo na kuongoza mashambulizi ya aibu dhidi yako unapo wapa kisogo!

Hawa wapo wengi. Na wapo kila pahala. Wapo kwenye nyumba za ibada, wapo maofisini, wapo mtaa wa Lumumba, wapo kwenye vikao vyetu vya ndani!

Ndugu zangu, uchaguzi huu ni Kati ya nguvu ya maono dhidi ya nguvu za kufoka na kufokeana.

Uchaguzi huu utusaidie kutenganisha yafuatayo:

Ubabe sio ujasiri. Udhaifu sio busara wala hekima. Kufoka foka hovyo sio Uwajibikaji. Kujipendekeza sio uzalendo! Kupenda serikali sio kupenda nchi. Ujenzi wa nchi siyo ujenzi wa taifa.

Ndimi mkulima wa Bamia, bonde la mto Simiyu - Magu, Mwanza.
Mkuu hakuna ulichobakiza hòngera
 
Back
Top Bottom