Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ana marafiki wa kificho, Rais Magufuli ana maadui wa kificho

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ana marafiki wa kificho, Rais Magufuli ana maadui wa kificho

Ninampa Lissu asilimia 70 za kumshinda Magufuli. Hakuna namna, narudia tena, hakuna namna Magufuli anaweza kumshinda Tundu Lissu mwaka huu. Wengi wapo na magufuli usoni ila moyoni wanajua wapo na Lissu. Kama Kuna kura za maruhani mwaka huu ndo atakazoziona magufuli.

Kikubwa Chadema na Lissu wajipange tu. Waandae timu imara na madhubuti ya kumuongoza Lissu kwenye Kampeni. Kumuongoza kwenye hoja za kupiga na namna za kupiga. Hakuna uchaguzi mzuri kwa chadema Kama wa mwaka huu!!
Unaruhusiwa kuota ndoto za mchana ili ujifurahishe.
 
UCHAGUZI wa mwaka huu unatakuwa ngumu na wenye mvuto mkali. Hii ni sawa na pambano lililosubiriwa kwa muda mrefu.

Mapambano kama haya yakitokea hulazimisha shughuli zingine zisimame ili kupisha mpambano mkali na wenye mvuto.

Hivi ndiyo ninavyoona uchaguzi wa mwaka huu. Siyo uchaguzi wa CCM VS CHADEMA. Ni uchaguzi Kati ya Tundu Antipus Lisu na John Pombe Magufuli.

Kwa sababu ya upekee huo, uchaguzi wa mwaka huu hautaamliwa kwa kushindanisha sera za wagombea, bali utaamliwa kwa kushindanisha sifa za wagombea.

Hapa Kuna aina mbili za wagombea. Yupo mgombea mwenye uchovu mwingi dhidi ya mgombea mwenye shauku nyingi.

Yupo mgombea mwenye kuitawala dhamiri yake mwenye dhidi ya mgombea mwenye kufungwa na dhamiri yake mwenyewe.

Yupo mgombea anayependa kuwatisha wenzake dhidi ya mgombea asiyezoea wala kuogopa kutishwa!

Yupo mgombea anayejua matatizo yetu hata kama hatujayasema dhidi ya mgombea anayependa kuahirisha matatizo yetu hata kama tumeyasema hadharani.

Yupo mgombea anayehisi na kuamini kwamba baya lolote likitokea ni hujuma za ndani au nje ya nchi dhidi ya mgombea anaye tambua kuwa makosa yetu ya kimfumo na kitaasisi ndicho chanzo kikuu cha mabaya tunayoyapata.

Yupo mgombea anayeamini hawezi kukosea, na akikosea husingizia wasaidizi wake au watangulizi wake dhidi ya mgombea anayeamini binadamu hatujakamilika, na kufanya makosa ni kuukamilisha utukufu wa MUNGU wetu aliye wema Sana.

Yupo mgombea anayeamini kuwa kila baya ni la watangulizi wake dhidi ya mgombea anayetambua mchango wa kila mtu katika ujenzi wa TAIFA letu. Uongozi ni pamoja na kurithi makosa ya wenzako.

Yupo mgombea mwenye uwezo wa kujenga nchi dhidi ya mgombea mwenye uwezo wa kujenga taifa.

Yaani ujenzi wa miundombinu mingi, sio ujenzi wa taifa. Kuna barabara zingine zinajengwa bila sababu. Nyingine zinaelekea makaburini.

Yupo mgombea anayechukia wakosoaji dhidi ya mgombea anayechukia makosa.

Yupo mgombea anayetenda anasema kila kitu dhidi ya mgombea anayetenda hasemi.

Yupo mgombea mwenye kumbukumbu nyingi kuliko ndoto dhidi ya mgombea mwenye ndoto na maono mengi kuliko kumbukumbu.

Yupo mgombea mwenye marafiki wengi wa kificho dhidi ya mgombea mwenye maadui wengi wa kificho!
Marafiki wa kificho ni wale wanakuunga mkono bila wewe kuwajua. Wapo tayari kulala njaa ili wewe ule na ushibe!

Maadui wa kificho, ni wale ambao wanakuunga mkono unapokuwepo na kuongoza mashambulizi ya aibu dhidi yako unapo wapa kisogo!

Hawa wapo wengi. Na wapo kila pahala. Wapo kwenye nyumba za ibada, wapo maofisini, wapo mtaa wa Lumumba, wapo kwenye vikao vyetu vya ndani!

Ndugu zangu, uchaguzi huu ni Kati ya nguvu ya maono dhidi ya nguvu za kufoka na kufokeana.

Uchaguzi huu utusaidie kutenganisha yafuatayo:

Ubabe sio ujasiri. Udhaifu sio busara wala hekima. Kufoka foka hovyo sio Uwajibikaji. Kujipendekeza sio uzalendo! Kupenda serikali sio kupenda nchi. Ujenzi wa nchi siyo ujenzi wa taifa.

Ndimi mkulima wa Bamia, bonde la mto Simiyu - Magu, Mwanza.
Subirini baada ya siku 40 ndiyo mjitathimini na huyo mpiga kelele wenu, alizoea kulala masaa 20 kwa siku sasa atatakiwa kuamka saa 10 usiku na kulala saa sita usiku. Kama atahimili hizo 40/60 mtakuja hapa mtuambie hayo mnayosema.Chezea presidential campaign!!!!!!!!!
 
Kuna mgombea mmoja angalau anajaribu kueleza ataifanyia nini Tanzania mpaka anatamani Tanzania iwe kama ulaya.
Lakini kuna mwengine anaacha kueleza ataifanyia nini nchi yetu anabaki kupayuka hovyo kila kukicha.

Huna sera kajambe hko ulaya na wewe
 
Chadema wakimudu kusimamia kura zote kwa uhalali isipotee hata moja, hakika LISSU atashinda kwa 70%.
Kuna changamoto kubwa sana ya mawakala wetu, wengi wanaendeshwa na njaa hivyo anaweza uza ushindi wa jimbo au kura za kituo kizima kwa sh, milioni 2 tu. Hili ni tatizo kubwa sana, linahitaji dawa
Asilimia 70 za kutoka wapi ? Kwa watanzania!?.. Acheni kudanganyana na kufarijiana mitandaoni humu ! Lissu hana kifua cha kushindana na Jpm !.
 
Yupo mgombea mwenye kumbukumbu nyingi kuliko ndoto dhidi ya mgombea mwenye ndoto na maono mengi kuliko kumbukumbu.
Nimeipenda sana hii, jamaa hana kumbukumbu zaidi ya maono ya Tanzania kuwa kama Ulaya, yaani aanzishe na kurasimisha ushoga.
 
Hili ni bandiko Bora kabisa la jf tangu huu mwaka uanze,mmoja anatumia nguvu kuishawishiwi Jamii Hali mwingine utumia akili kuishawishiwi Jamii.

Jiwe kapata dawa hapa wangepatikana Lisu Kama watatu hivi plus Mtikila hakika uonevu na udhalimu tunaofanyiwa watz ungekoma.watz wenzetu wameuliwa, bambikiwa, wanaishi ukimbizini, fukarishwa, bomolewa nyumba zao, watz tulikuwa wakiwa kwa miaka 5 Sasa yatosha.

Lisu karejesha Imani na moyo wetu wa kutamani kupiga kura again baada ya uhuni ya uliofanyika uchaguzi za serikali za mitaa wa kuchaguliwa wagombea

Serikali ya watu kwa ajili ya watu ndo tuitakayo na si serikali ya watu kwa ajili ya mtu

Mtu mmoja katu hawezi kutuamulia tuishi atakavyo yeye sisi sio familia yake maadamu tu atuvunji sheria

Watz tuwe huru na nchi yetu tulinyimwa kuongea 5 yrs Sasa ni wakati wa kuongea tuteme nyongo zote
Hivi ni mtu mmoja au chama kimoja chenye mamilioni ya wanachama na wafuasi mkuu!?
 
Eti asilimia 70! Unawajua watanzania wewe lissu hana ushawishi wowote mbele ya Magufuli ambaye kazi zake zake zinaonekana kwa vitendo!. Endeleeni kujifariji tu humu Jf ilauo ndo ukweli mchungu.!. Lissu na wapinzani wengine watatoa changamoto tu ila hawawezi kushinda Urais never! ,Hilo hata wapinzani wanalijua . Yaani mnashindana na chama ambacho kimejiekea mizizi toka kwenye mashina/matawi huko kuanzia vijijini hadi mijini , chama chenye rasilimali fedha sa kutosha kuendesha kampeni ,alafu simply tu unakuja hapa eti lissu atashinda 70% unawajua watanzania wewe..!
Tukutane October 2020 ndugu. Lissu ndo Raisi wako kuanzia 2020 upende usipende.

Huyo Magufuli wako aliyoyafanya yanayooneka ni kuharibu uwekezaji, bei ya sukari, uchumi wetu kuepelekea watu wengi kukosa ajira, kuharibu biashara na kufanya wafanyabiashara wengi zaidi kufunga biashara, kupapendelea Chatto kwa maofisi makubwa, uwanja wa ndege na mbuga, kupiga watu risasi na kubambikiwa watu wasiomuunga mkono makesi kama kina Idris Sultan, Wanasiasa wa Chadema , Erick kabendera, mdude nyangali, Tito Magoti n.k
 
Ubabe sio ujasiri. Udhaifu sio busara wala hekima. Kufoka foka hovyo sio Uwajibikaji. Kujipendekeza sio uzalendo! Kupenda serikali sio kupenda nchi. Ujenzi wa nchi siyo ujenzi wa taifa.


Yaani uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu hatari. Subirini tu mtaona jinsi gani ccm watakavyotafutana huku mitaani
 
Tukutane October 2020 ndugu. Lissu ndo Raisi wako kuanzia 2020 upende usipende.

Huyo Magufuli wako aliyoyafanya yanayooneka ni kuharibu uwekezaji, bei ya sukari, uchumi wetu kuepelekea watu wengi kukosa ajira, kuharibu biashara na kufanya wafanyabiashara wengi zaidi kufunga biashara, kupapendelea Chatto kwa maofisi makubwa, uwanja wa ndege na mbuga, kupiga watu risasi na kubambikiwa watu wasiomuunga mkono makesi kama kina Idris Sultan, Wanasiasa wa Chadema , Erick kabendera, mdude nyangali, Tito Magoti n.k
Mkapa aliwauzia watz dhahabu feki rangi halisi kila mtz ameshaiona
 
Ndugu. Naona umejitahidi kujenga hoja lakini umesahau kujua hoja na vioja. Hoja kazitoa jana Ndugu magufuli. Na Amejenga hoja vizuri sana na hoja zake zinauzika kwa wananchi walio wengi.

Sasa chadema wasitegemee uruma za wananchi Bila kuwaambia wananchi hoja mufilisi.

Huwezi kudharau hata kidogo kazi iliyofanyika kwa kuwambi wananchi mmenyimwa haki ya kufanya mikutano na kutaka katiba mpya wakati wananchi wanataka kusikia na kuona. Barabara za uhakika. Umeme. Maji. Dawa maosptaĺini. Na shule kuboreshwa. Kudhibiti Ufisadi.

Alafu wewe unakuja kubeza majukwaani na kuwambia wananchi katiba na uhuru wa kuongea na kufanya mikutano. Hapo utaambulia patupu kamanda.

Kimsingi chadema na upinzani mkubalitu Hakuna wa kumpiku magufuli kwa utendaji uo ndio ukweli. Na ilo wanalitambua shida yao ni kutaka ikulu huku wakijua uwezo hawana.
Nadhani wewe ndo huelewi concept. Miaka 5 ya Jiwe imeshuhudia watz zaidi ya million 4 wakiwa mafukara kabisa, biashara zao zikifa na ajira zao zikikoma.. hilo siyo dogo.. si la kubeza.. mabarabara au reli hata wakoloni walijenga, lakini hakukuwa na namna ilibidi watimliwe.. ndo litakalomkuta Jiwe muda si muda. Kwa mateso tuliyopata tunasema "Never Again".
Tusubiri
 
Maadui wa kificho, ni wale ambao wanakuunga mkono unapokuwepo na kuongoza mashambulizi ya aibu dhidi yako unapo wapa kisogo!

Hawa wapo wengi. Na wapo kila pahala. Wapo kwenye nyumba za ibada, wapo maofisini, wapo mtaa wa Lumumba, wapo kwenye vikao vyetu vya ndani!
Naiona ccm ikiwa mtegoni sasa hivi. Inaonesha mwaka huu wamenasa mtegoni. Ukimya wao unamaanisha wapo chimbo wanafikiria namna ya kujinasua na mtego wa mamba
 
Back
Top Bottom