Tundu Lissu anadai pesa ya matibabu kiasi Gani, na kwanini hajalipwa hadi Leo?

Kuna watu wanasema Rais Samia ni mtu wa HAKI!!

Sasa mtu aliyeshambuliwa na wasiojulikana akiwa mbunge kutolipa Hadi sasa haoni hiyo ni fedheha?
Kusema Samia ni mtu wa haki, siamini. Labda tuseme ana-act kuwa mtu wa haki.

Alimweka Mbowe ndani kwa uonevu, na kama isingekuwa sauti za mataifa makubwa, sijui angemsotesha Mbowe jela kwa muda gani!!

Aliyesimamia shambulio dhidi ya Lisu, anafamika, badala ya kutoa maelekezo uchunguzi ufanyike ili wahusika wafikishwe mahakamani, akaamua kumpa madaraka mtuhumiwa mkuu.

Kajitwalia rasilimali za nchi, na kuwagawia watu anaowataka yeye. Kawaondosha wamasai kwenye ardhi yao ya asilia na kuwapeleka mamia ya kilometa, kwa vile tu mwarabu aliyepewa Ngorongoro hawataki wamasai kwenye eneo alilozawadiwa.
 
Umenikumbusha pia kesi ya uhaini wa kina Dr Slaa!!

Miaka hii minne yametokea mambo mazito sana tena Kwa Kasi ya ajabu!!

Mungu atujalie 2025 akabidhi salama.
 
Umenikumbusha pia kesi ya uhaini wa kina Dr Slaa!!

Miaka hii minne yametokea mambo mazito sana tena Kwa Kasi ya ajabu!!

Mungu atujalie 2025 akabidhi salama.

Ni kweli. Fikiria mtu anatetea rasilimali za nchi yake, halafu anatengenezewa kesi ya uhaini ili asihoji uovu waliotendewa wananchi.
 
Apewe pia gari mpya baada ya gari yake kumiminiwa risasi na wasiojulikana.
 
Anayo haki kwa asilimia 100 kurudishiwa gharama zote za matibabu kwa sababu alikuwa bado ni Mhe. Mbunge wa Singida Mashariki. Wasipomrudishia asonge Mahakamani.
 
Anayo haki kwa asilimia 100 kurudishiwa gharama zote za matibabu kwa sababu alikuwa bado ni Mhe. Mbunge wa Singida Mashariki. Wasipomrudishia asonge Mahakamani.
Bunge ni mhimili unaojutegemea,

Kulipeleka bunge mahakamani ni kuingilia Bunge.
 
Sijaona pahali popote pale panaposema mada hii inamhusu Job Ndugai.

Niulize tu, Tundu Lissu alitibiwa ama hakutibiwa? Na nani?
 
Nikisema kuwa wanaochelewesha malipo, walidhamiria asitibiwe,

Nitakuwa nimekosea?

Ndio. Utakuwa umekosea.


Ukweli ni kwamba alitibiwa.

Kwamba "walidhamiria" asitibiwe ni madai yasiyo na mashiko- haina uhalisia ama ukweli wowote ule.
 
Ndio. Utakuwa umekosea.


Ukweli ni kwamba alitibiwa.

Kwamba "walidhamiria" asitibiwe ni madai yasiyo na mashiko- haina uhalisia ama ukweli wowote ule.
Ni Kweli alitibiwa?

Swali ni kuwa, alitibiwa kama mbunge?
 
Uko sahihi kabisa kuna watu wamefika mahali mpaka wanaogopa kudai haki zao eti tu watakuwa termed as wachochezi mara wanaharakati majina kibao
 
Wamefuta Uzi wa kuchangia Lissu gari, mwenye zile AC namba aweke hapa michango iendelee.

@cc Tindo
 
Mkuu unauliza jibu?

Kwa maana hiyo anataka alipwe fedha kwakuwa alikuwa Mbunge. Ama mhanga, ama vyote. Haya.

Je, ingepunguza gharama? Je, matokeo ya matibabu yake awe ni mbunge ama Laigwanan, yangebadilika?
Narudia,

Ni wewe uandikaye, au simmu Iko hacked?
 

Hata mtu asiposema hapa, lakini ukweli ni kuwa lazima zitakuwa pesa nyingi sana...

Huyu mtu alikuwa ni mfu eti wakati ule...

Gharama ya kurejesha uhai wake na kuukarabati mwili wake uliokuwa umechakazwa na risasi zile hata kuwa hivi alivyo leo bila shaka ni kubwa sana na bado anaendelea na matibabu (regular check ups)...

Lakini wapende au wasipende, ni lazima siku moja watamlipa tu haki yake...

Job Ndugai na John P. Magufuli nafsi zao zinawasuta na kuwahukumu huko walipo.

Ndugai bado yupo hai. Mwenzake tayari alishakufa na kumuacha waliyejaribu kumuua akiwa hai na kupumua kwa afya yake...

Ndugai atubu kabla hajafa. Akifa na dhambi hii, asije akamlaumu Mungu. Itakuwa ni ujinga wake kwa kushindwa kurekebisha kwa toba ya ukiri wa mambo yake akiwa hai...
 
Waliomshoot wapo hai nadhani.
 
Muhimu watu tuchangie kwenye AC zilizopo,

Apate pesa ya kununulia gari jipya, na airudishe gharama .

Tukichangia 2,000 Kila Mmoja, wakapatikana watu 2,000,000, atapata 4bn.
 
Muhimu watu tuchangie kwenye AC zilizopo,

Apate pesa ya kununulia gari jipya, na airudishe gharama .

Tukichangia 2,000 Kila Mmoja, wakapatikana watu 2,000,000, atapata 4bn.
Tutafanya hivyo..

Huyu mtu ni wa muhimu sana..

Watu makini hawangependa kumuona akipata taabu katika kuongoza mapambano ya kupigania uhuru wa pili wa Tanganyika toka kwa mkoloni mweusi aitwaye CCM
 
Tutafanya hivyo..

Huyu mtu ni wa muhimu sana..

Watu makini hawangependa kumuona akipata taabu katika kuongoza mapambano ya kupigania uhuru wa pili wa Tanganyika toka kwa mkoloni mweusi aitwaye CCM
Sasa thread za kumhusu Lissu kuchangia anunue gari zinafutwa Ili iweje!!

Tatizo nn Lissu kuchangia anunue gari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…