Ninaandika andiko hili nikiwa katika fikra pevu sana.
Ninakumbuka katika maandiko Yesu aliposulubiwa ilifika hatua Alilia kwa sauti na Kusema Mungu wangu Mungu Wangu,Mbona umeniacha?
Nimefuatilia sana sakata la Lisu,Swali ambalo nimekuwa najiuliza na hata sasa najiuliza Je Tundu Lisu anajtoa kafara au anapigania Haki?Nimeuliza ili swali kimzaa mzaa ila ndani ya Moyo wangu natamani sana swali hili lipate JIBU kwa anayewe za kuleta Jibu;
Kwa uzoefu wangu mahakamani sio sehemu ya kutafuta haki,Mahakama kazi yake ni kutafsiri Sheria kwa kupita facts ambazo zinaleta mbele yake.
Tundu Lisu,amekaa mahabusa kwa muda mrefu sana,katika hicho kipindi sina hakika kama hajatafutwa offrecords ili aridhie terms fulani ili tu kesi yake hii ifikia tamati.Naamini kabisa amefuatwa na sio mara moja.
Unapoona kwamba mpaka sasa kesi bado inaendelea kuna maana kwamba Tundu Lisu amekataa kushawishika.Swali ni Je amekataa kwa sababu anaamini kwamba Mahakama itampa haki,au ameamua kujitoa Mhanga/kafara.
Kwa watakaoweza kumshauri wamwambie tu,atafakari kama anachopigania kina stahili kufia.Kama Jibu ni Ndio ashikilie hapo hapo na kama Jibu ni Hapana basi atafakari na achukue hatua.
Kama taifa tupo katika wakati mgumu sana katika ujumla wake.