Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Leo akiwa huko Muheza ‘kwenye kampeni zake za urais’, Tundu Lissu kazungumzia tena suala la Corona.
Japo kalizungumzia kidogo tu, lakini kaligusia kwa kumkosoa tena Rais Magufuli na jinsi alivyoamua kukabiliana nayo.
Kamkosoa Magufuli kwa kuwaambia watu wasivae barakoa, ‘kwanza zinafanana na sidiria za wanawake’.
Sijui ni lini na wapi Rais alisema hivyo. Mnaojua mtanifahamisha.
Ila kwa Tundu Lissu kusimama mbele ya watu ambao hawana ‘time’ na Corona, ambao wamesimama kwa kurundikana bila kuacha nafasi, na ambao wala hawajavaa barakoa, akiwemo yeye mwenyewe, ni unafiki wa daraja la kwanza.
Kila siasa huwa ni za mahali pake. Kwa Tanzania hii, suala la Corona si hoja yenye mashiko, na kwa mtaji huo, si hoja ya ushindi.
Mbaya zaidi ni kutokitenda kile ambacho unakihubiri.
Huyo Tundu Lissu yeye anachukua tahadhari gani dhidi ya Corona tokea aje?
Ile barakoa yake aliyoivaa kwa dakika chache ile siku aliporudi, iko wapi?
Huyu jamaa ni kama vile yuko nje ya mguso na mambo ambayo Watanzania wanayajali.
Hebu mtazame hapa kuanzia dakika ya 6:30.....