Tundu Lissu aondoka nchini kuelekea Ubelgiji. Asema anakwenda uwanja mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu

Tundu Lissu aondoka nchini kuelekea Ubelgiji. Asema anakwenda uwanja mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu

Hii inaitwa political tourism. Unaenda nchi fulani unagombea Urais, uchaguzi ukiisha unapanda ndege unaenda kuendelea na maisha yako.

Wale waliomuamini wote anawaona mabwege.
Ulitaka abaki ili Magufuli na wapwa zake wamuue? Hukusikie yule bwege akisema safari hii watamchoma sindano ya sumu? Magufuli alishindwa vibaya sana kwenye uchaguzi na asingeweza kumwacha aendelee kuishi.
 
Anakimbia jeshi la kukodi kutoka Burundi lililovishwa jezi za polisi wa Tz
Na wewe unaamini hilo? Kama unadhani Mtanzania mwenzako kakufanyia ubaya mseme kama alivyo. Haina haja ya kumpachika Uburundi.
 
Panya ukimuona nyumbani ukimkimbiza angalia shimo anakokimbilia huko ndio Kwao Lema na Lissu wamekimbizwa Tanzania wamekimbilia mashimo ya Kenya na Kutaka kwenda USA kwa Lema ukimbizi kwa Lema na Lissu katimukia ubalozi wa ugermani na ubelgiji huko ndiko shimo lake alikotokokea.

Mungu mwema katuonyesha watanzania panya hawa tuliowakimbiza wametokea mashimo yepi.

Toka mwanzo tuliambiwa Chadema wamiliki Ni wakenya ,wazungu na wamarekani tumeshadhibitisha wanaenda kwenye mashimo yao.
Hii ina hatari yake. Kumbukeni alipokuwa tunduma yule police alimwambiaje kaka usikitafutie matatizo na police naona alimwelewa akamwacha.

Jamaa amekusanya evidence nyingi sana Mimi nionavyo huyu anakwenda kukinukisha.

Nilidhani serikali ilipaswa hata kumuita balozi aliyemhifadhi aende nae kuwe na mazungumzo ya ana kwa ana na Rais ili Ku resolve hii kitu kuliko kumwachia hivi.

Kumbuka
Issue ya chato akagoma kuondoka
Kumbukeni alivukaje kwenda kisiwa cha ukerewe
Kumbukeni nyamongo
Matukio yote hayo yeye hajajibizana nayo ila anawasiliana na Mwanasheria wake.
Binafsi huyu hakupaswa kuondoka.

Kwa sasa nashauri
Viongozi wana diplomacy wa ccm Nguli pamoja na Rais wetu wawaite viongozi wa chadema wakae nao wazungumze mambo yataisha kabisa. Ila mkataapo haya yataleta kushusha heshima ya Tanzania ilijengwa katika ulimwengu.

Pili, vikwanzo vitaanza kuibuka
Tatu, uchumi utaporomoka

Maoni tu haya
 
Aende mwana kwenda, uwanja mpya anaosema ni hapa JF hamna kwingine
Hapa JF Antipasu hawezi kutia mguu! Anapajua sana. Alijifanya kuomba maswali kutoka kwa memba wa JF wakati wa kampeni eti atoe majibu kuhusu malengo yake kuwania urais, alipopelekewa kalala mbele hakuna hata swali moja alijibu. JF pagumu sana inabidi ujipange!
 
Sasa uliandamana? Au unataka wao watangulie huku wewe ukiwaangalia katika Runinga, Nyumbani kwako? Kama unaona hawajatimiza wajibu wao ipasavyo wewe onyesha mfano. Hakuna mtu ambaye amezaliwa kwa ajili ya kupambania haki zako.
Mimi nilitegemea nimuone Lisu, Mbowe, Halima Mdee na Mnyika waanze wao afu akina sisi huku tukiwaona kwenye TV ndio twende. Kumbe wao walikuwa wanataka sisi tutangulie kikanuke afu wao waamshe wakamcheki Hazard na Lukaku mbashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alichofanya kilitarajiwa na mtu yeyote mwenye akili timamu. Mbona dereva wake alimuacha Ubeljiji kukwepa mashtaka? Na yeye kakwepa kesi kadhaa zinazomkabili ikiwa ni pamoja na shtaka analomkwepesha dereva wake.
 
Bora ameondoka angeuawa. Ongera kwa balozi wa Ujerumani kumwezesha kuondoka maake walitaka kumungangania. Uko atakuwa salama zaidi na mapambano anaenda kuyaweka sawa sas. Nchi hii chin ya utawala huu haitabiliki. No rule of law but statement of meko turns law of the land!
 
Kama tungekuwa na viongozi wenye akili wangejitahidi kuhakikisha hawa viongozi wa upinzani wanabaki nchini.

Sasa ushindani kati ya Jiwe na Wapinzani unaenda kwenye ngazi ya kimataifa, ambako kwa kipimo chochote kile, Jiwe ni dhaifu sana.
Naam umeona mbali sana . wengi wanashabikia tu ila hawaoni kesho ya Tanzania yenye athari kubwa sana
 
Pasi shaka yoyote, hizi kesi ndio imebaki turufu yao kuu ya kummaliza Tundu Lissu, kumbe yeye alishauona mchezo kungali mapema kabisa.
Hizo kesi za kimagumashi walizombambika zitayeyuka tu.
 
Yule anaweza kufanya lolote kwa sababu hata busara kidogo hana
Hapana.

Ni mwoga sana huyo.
Ukiondoa vyombo vya ulinzi anavyovitegemea (ambavyo pasi shaka watamkatalia kusambaza vita vyake na hawa watu); yeye kama yeye ni mwoga mkubwa.
Kama huamini, jaribu kuangalia kumbukumbu zake akiwa waziri, wakati hana kinga ya mitutu ya bunduki na takataka nyingine anazotumia sasa kuwakandamiza wengine.
 
Nilidhani serikali ilipaswa hata kumuita balozi aliyemhifadhi aende nae kuwe na mazungumzo ya ana kwa ana na Rais ili Ku resolve hii kitu kuliko kumwachia hivi.
Tanzania ni kubwa; therefore, she won't be intimidated by selfish asylum seekers!
 
Haina uwezo huo kama kuna makubaliano tayari na anaenda under diplomatic escort. Wingefanya trespassing mziki wake hawauwezi.

Kumbuka kila bosi ana BOSS wake
yes.
432ba896-5d6c-452e-badf-be640b522c32.jpg
 
Hapana.

Ni mwoga sana huyo.
Ukiondoa vyombo vya ulinzi anavyovitegemea (ambavyo pasi shaka watamkatalia kusambaza vita vyake na hawa watu); yeye kama yeye ni mwoga mkubwa.
Kama huamini, jaribu kuangalia kumbukumbu zake akiwa waziri, wakati hana kinga ya mitutu ya bunduki na takataka nyingine anazotumia sasa kuwakandamiza wengine.
Uoga siyo busara
 
Kama haukawahi kuwa ktk hali ya kupigania uhai wako kwanza, hauwezi kuelewa wanachokifanya Lisu na Lema, me nawaelewa sana.

Hakuna ushujaa roho ikishakutoka, tutakukumbuka siku mbili tatu tuwasahau.

Nendeni mkaweke maiaha yenu salama kwa ajili yenu, na watoto wenu na wake zenu.... najisikitikia sisi tunaowabeza tukidhani tupo salama.

Yajayo TANZAGIZA yanasikitisha,
 
Mimi nilitegemea nimuone Lisu,Mbowe,Halima Mdee na Mnyika waanze wao afu akina sisi huku tukiwaona kwenye TV ndio twende. Kumbe wao walikuwa wanataka sisi tutangulie kikanuke afu wao waamshe wakamcheki Hazard na Lukaku mbashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya ndiyo tunaita mawazo ya ki-nyani nyani. Udikteta na uongozi mbovu wa Magufuli na wapwa zake unaathiri watanzania wote. Mabadiliko yakitokea na kwa faida ya watanzania wote na tukiendelea na huu uongozi mbovu ni hasara ya watanzania. Ni jukumu la watu wote kuipigania nchi yetu. Kama wewe unaona kuna wenye wajibu zaidi basi utabaki na upumbavu wako huku ufukara ukindelea kukutafuna unless uwe kwenye inner circle ya Magufuli na wapwa zake.
 
Hivi chadema wangekua wamechukua majimbo yote kasoro mawili kwenye uchaguzi, halafu CUF na CCM wakapata kitu kimoja kimoja mngesema CCM waachiwe baadhi ya majimbo ili kuweka balance bungeni?

Chadema tafuteni mlipokosea mtengeneze, manenomaneno, matusi, uasi, ukimbizi hautamsaidia mtanzania yoyote zaidi ya hao viongozi wenu wabinafsi na wanaojifikiria wenyewe.

Chama mlikinajisi wenyewe kwa kumwita mliyemtuhumu fisadi kugombea urais, tena mbaya zaidi mlimkaribisha baada ya chama chake kumwambia hawawezi kumpa nafasi ya kuongoza dola sababu sio muadilifu.

Nyie sababu ya tamaa zenu za pesa mkamsafisha bila haya ili mshirikiane nae kufisadi nchi.
Hamkujifunza kwa Lowasa 2015.

Na ilipofika 2020 mkakinajisi tena chama kwa kumuweka mgombea mtetezi wa mataifa ya nje asiyejali maslahi ya wananchi. Eti mgombea wenu akaanza kampeni awe mbwembwe huku akiwatukana watanzania wasomi na wasio wasomi hadi maJaji kuwa hawajui Kiingereza, eti mkawadharau police na kuwaambia wamechoka na wana hali mbaya, mgombea wenu akawa mjuaji wa kila kitu akamdharau hadi baba wa taifa Nyerere.

Kwa kampeni zake hakuna kilichofanyika Tanzania tangu wazungu waondoke; analazimisha eti hata kwenye reli hakuna kilichofanyika ila reli imejengwa na Mjerumani.

Juu ya yote akawaahidi waliomtuma hadi kwenye ilani ya chama chenu kwamba akiingia ikulu ataweka madini kama dhamana kwao ili wampe pesa.

Kampeni mwanzo mwisho mgombea wenu alikua akituringishia nguvu ya wazungu, akijidai wakili wake anafuatilia kitu. Watanzania walijiuliza hivi tukimpa kura atatuongoza yeye au atatuongoza kwa amri ya hao mabwana aliowaahidi kuweka mali zetu rehani kwao?

Hivi kweli hadi Karne hii bado kuna wasomi wa Tanzania tunatumia elimu tuliyo nayo kuweka rehani nchi yetu kwa wazungu badala ya kutumia ujuzi na elimu yetu kuvuna rasilimali zetu kwa faida? Tundu amelifedhehesha sana taifa

Hivi mlifikiri watanzania ni wajinga kiasi cha kumchagua mtu kama huyo kuwa rais wa nchi?

Wafuasi wa Tundu ambao ni wachache sana wana mienendo kama ya Tundu.

Tuliwashauri mapema mkawe mawakala ili mkasimamie haki mnayoiimba hapa jf hamkuskia, tena badala yake chama chenj kikatafuta ambao hadi leo hakijawalipa posho zao.

Matokeo yake kila siku mnarudi hapa kulalamika kwamba mmeibiwa kura, hivi hamjisikii aibu kila uchaguzi mnalalamikia tatizo lilelile kama sababu ya kushindwa? Hamuoni kama nyie ni chama kisichoweza kutatua matatizo ya chama wala ya wananchi?

Haya sasa wananchi wamewakataa kwenye kura, wamewakataa kwenye maandamano, wamewakataa kwenye kuigomea serikali na hii inaonyesha chama chenu sio cha wananchi bali ni cha viongozi ndio maana mmebaki wenyewe mkihangaika.

Ingekua wananchi wanawapenda kungekua na maandamano yasiyozuilika kama maji ya jangwani kipindi cha mafuriko ila wananchi wana raha na amani tele, hata wale mliowaandaa kwa malipo sasa wanajuta na hawawezi rudia

Kwa tamaa zenu 2015 mliua kile chama tulichokipenda, Ile chadema ya wananchi, chadema iliyokua tumaini la wanyonge, chadema ya Mzee Ndesamburo na Dr Sla na wale viongozi wengine makini. Laana itawaandama kama hamtawaambia wananchi mliwakosea ili muanze upya

Maisha sio rahisi kwa mtanzania yoyote hata kwa Rais, huu ni muda wa kujenga uchumi wetu tuliouharibu na huduma za kijamii kwa maslahi yetu wote. Acheni kulalamika sasa

Tundu asafiri salama, tunamshukuru kwa kushiriki
 
Back
Top Bottom