Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa , Jeshi la Polisi Dodoma leo hatimaye limemuonyesha Tundu Lissu gari lake lile lililotunguliwa na risasi zisizo na idadi kwa lengo la kumuua .
Tundu Lissu akiwa mbele ya polisi , amehesabu upya matundu ya risasi alizomiminiwa na watu waliotumwa kumuua ambapo hesabu hiyo imefikia zaidi ya 30 !
Akiwahutubia polisi hao kwenye kituo chao , ameonyesha kushangaa kwamba ilikuwaje pamoja na lundo hilo la risasi hizo akatoka akiwa anapumua , amewaambiwa polisi hao kwamba siku chache zijazo atakuja kulichukua gari lake .
Tunatoa shukrani kwa jeshi la Polisi kwa kumuonyesha Lissu Gari lake , japo ni kwa kuchelewa .
Sent from my SM-J500H usinlissug
JamiiForums mobile app