Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aongea na Wahariri wa Vyombo vya Habari - Sept 9, 2020, ataenda Mahakamani kwenye kesi zake Kampeni zikiisha

Shida ya Lissu hasemi yeye kama yeye atafanya mambo gani makubwa, tushajua magu hafai. Sasa yeye aache kila siku kumzungumzia magu badala yake aseme yeye kama yeye atafanya yapi

Tatizo lako inawezekana huwa humsikilizi ila unapenda kuhukumu kijumla jumla tu....

Yuko very clear kuhusu atafanya nini...

Ni kwamba SOURCE YA MATATIZO HAYA YOTE NI MFUMO WA KISHERIA, KIKATIBA na UTAWALA wa nchi yetu....

Amesema, atakachofanya yeye tofauti na CCM na MAGUFULI wanavyofanya, ni kufumua mfumo huu wa utawala, kisheria na kikatiba na kutengeneza mfumo mpya wa kiutawala unaowajibika kwa wananchi moja kwa moja....

Huoni kuwa hii ndiyo mwanzo wa suluhisho la matatizo haya?

Nyie nadhani mnataka aahidi ahadi hewa maelfu kisha atende vilevile kiCCM...

Ndugu kama ni ahadi tumeahidiwa sana tangu Uhuru lakini kamwe hazijawahi kutuondolea au kutupunguzia matatizo ya umasikini, maradhi na ujinga wa watu wetu...!!
 
Halafu Tundu Lissu ukimsikiliza unaona kabisa anamaanisha.Huyo msukuma Fix tupu!
 
Kwa hili la lugh naungana na Lissu kwa 100%.

Tubadili sera ya lugha.

Tuchague kusoma kwa kiswahili au kwa kiingereza. Na sio kurukaruka na lugha mbili mwisho wa siku sio kiswahili wala sio kizungu unachoweza kuzungumza.
 
Mkuu,mbona kama unataka kumpa mamlaka(TAL) ,kabla ya....,msaada kama hana bado...!
G.Thinker: Nichomaanisha kumpa taarifa za utoaji wa press conference yake na wahariri haiwezi kutoka kwa weledi wa deep story ila watachuja na kutoa story nyepesi sana.

Nadhani umesikia au kuona kwenye habari za jioni hii na angalia kesho kwenye magazeti.
 
Kwa mujibu wa Post ya kwanza ya uzi huu nina haya machache yaliyonijia kichwani!

Tuanze.

1. Kutokana na majibu ya swali la kwanza aliloulizwa, Lissu, anadhibitisha kuwa ametumwa na mabeberu. Hajakanusha/kataa kuwa anatumwa na mabeberu kwenye majibu yake zaidi amezunguka zuunguka.

Na kuonyesha, Lissu kazama kwenye "tope", ameamua kuzusha! Anadai, Tanzania imeharibu urafiki na nchi nyingine lakini hazitaji nchi hizo (kama mwanasheria anatakiwa kudhibitisha kauli zake kwa ushahidi). Eti,yeye atarudusha diplomasia na mataifa ya nje!!! Uzushi mtupu!!!

Lakushangaza, anadai mabeberu ndiyo wanaombwa msaada! Halafu aache kudanganya hapa...ulimwengu huu wa ki-capitalism na biashara huria...hakuna kitu cha bure (msaada)! Hivi kwa akili ya kawaida uitwe beberu halafu wakati huo huo utoe 'msaada' ! Hivi Lissu anatuona sisi mazuzu sio? Aache dharau zake kwa watanzania!

2. Lissu pia anafanya 'spinning' kiaina ! Anasema hajui hizo picha zilitoka wapi! ha ha haaa!
===
Na hayo, wale 'watani' zangu 'povu ruksa! Ha ha haaa
 
Shida ya Lissu hasemi yeye kama yeye atafanya mambo gani makubwa, tushajua magu hafai. Sasa yeye aache kila siku kumzungumzia magu badala yake aseme yeye kama yeye atafanya yapi
Mpaka leo hujui ilani ya chadema na umo mtandaoni? Hata mambo ya kuboresha Bima ya afya kwa wote, kufidia mishahara ya wafanyakazi, kuunda Tume ya maridhiano kwa madhira yaliyofanywa awamu ya tano, kuimarisha Uhuru wa kujieleza na haki za Binadamu.
Ukiwa na akili nzuri Ukiona mtu analaumu awamu ya tano, ujue kuwa mtu huyo akipewa nafasi ataondoa maovu yote ya awamu ya tano
 
Yawezekana Tundu Lissu 'kasahau' kuwa Media yote ya Tanzania na hasa hasa kupitia tu 'Wahariri' na 'Wamiliki' wapo Mfukoni mwa Dkt. H Abbas.
Mtake radhi Max Melo na wenzake wa hapa JF! Pia na sisi watumiaji wa JF, tafadhali sana!! Usichafue kambi, Mkuu.
 
Aloshasema mengi kama hujasikia usimlaumu mtu hapa
Shida ya Lissu hasemi yeye kama yeye atafanya mambo gani makubwa, tushajua magu hafai. Sasa yeye aache kila siku kumzungumzia magu badala yake aseme yeye kama yeye atafanya yapi
Us
 
Mtake radhi Max Melo na wenzake wa hapa JF! Pia sa sisi watumiaji wa JF, tafadhali sana!! Usichafue kambi, Mkuu.
How can any logical person think we can survive another five years or more of that dude from the green?
 
Shida ya Lissu hasemi yeye kama yeye atafanya mambo gani makubwa, tushajua magu hafai. Sasa yeye aache kila siku kumzungumzia magu badala yake aseme yeye kama yeye atafanya yapi
Amekwambia Tz imepoteza diplomasia nje ya mataifa akiwa rais atarepair...

Anatoa KASORO na KUZITOLEA usuruhisho pindi akiwa Rais
 
Mtake radhi Max Melo na wenzake wa hapa JF! Pia na sisi watumiaji wa JF, tafadhali sana!! Usichafue kambi, Mkuu.

Tumia 'Akili' kidogo ninayoizungumzia hapa hasa ni ile 'Mainstream Media' na siyo hizi 'Social Media' sawa? Acha 'Kukurupuka' najua nisimamia nini.
 
Tumia 'Akili' kidogo ninayoizungumzia hapa hasa ni ile 'Mainstream Media' na siyo hizi 'Social Media' sawa? Acha 'Kukurupuka' najua nisimamia nini.
Sawa Mkuu, nawe pia tumia 'Akili' kubwa basi ili uwe unajitahidi kufafanua specifics ya issues badala ya ku'generalise' masuala unayotaka kuhabarisha umma wa JF na kwingine. Hiyo, itatusaidia sisi wenye kupenda kutumia 'Akili' kidogo kutoingia kwenye utata wa kuelewa mada zako.

Kumbuka, JF iliwakilishwa na Wahariri wake kwenye Kikao hicho hiyo jana.

Hapa nitakuwa nimejieleza vyakutosha nadhani.
 

Sina tatizo na JamiiForums na ningekuwa ni 'Mpumbavu' wa 'Kutukuka' kama na Wao ningewahusisha katika ile 'Comment' yangu iliyokuchanganya.
 
Mgombea Uraisi wa chama fulani alisema kuwa watanzania hawajui kingereza, hasa wanatia aibu wanapokuwa huko ughaibuni. kisha nikajiuliza; je, Kiswahili chetu hiki, watanzania wote wanakifahamu kwa usanifu na usadifu wake?

kitu ambacho naamini sio kweli, yawezekana mwenyewe nikawa miongoni mwa wahanga hao. Sasa yanini kulilia kujua kingereza kwa ufasaha wakati kiswahili chenyewe tunamakosa mengi kwenye kukizungumza na kuandika. siku zote ukitaka kuwatambua wengine anza kujitambua mwenyewe. jambo jingine la kufurahisha hapa, sijawahi kusikia wazungu wakichekana ati wanaaibisha mataifa yao kwa kuongea kiswahili kibovu, mbali zaidi wengine wanakuja huku hata kingereza chenyewe hawajui, na wanafundishwa na wabongo hiyo broken.

Me nadhani wanaotucheka kwa kuongea kingereza kibovu hapa nchini na ughaibuni si wazungu bali ni sisi wenyewe. Je! kuna ulazima sana siye kujua Kingereza ili tufike Nchi ya ahadi?, Mataifa kama Uganda, Zimbabwe, Kenya n.k ambayo yasemekana yanawazungumzaji wazuri wa kingereza Wamefika Kanani?
(Nchi ya Ahadi).

Mi nadhani kheri yule mwenye Maarifa, busara na hekima, na hajui kingereza. kuliko ajuaye kingereza na akakosa vitu vitatu. kikubwa Elimu iboreshwe watu wapate Maarifa yanayoenda na wakati, na si lazima wote tujue kingereza ndio maana kuna watu wanasomea utafsri wa lugha, na Maranyingi mataifa ya Asia ya mbali wanatumia sana lugha zao hata wakiwa nje ya Nchi zao na wakalimani huhusika sana kwenye masuala yanayohusu lugha tofauti na yao.

Je, Mataifa hayo hayajapiga hatua ya kimaendeleo? Kwahiyo hili suala la kutojua kingereza Mheshimiwa aliliongelea kwa upande mmoja wa sarafu. mihemko( emotions) inatupofusha kutazama mambo yaliyo mbali zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…