Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu ameingia jimboni kwake Singida Mashariki na kulakiwa na umati mkubwa wa watu kuwahi kushuhudiwa katika Jimbo Hilo.
Akiwa na msafara mkubwa wa magari, pikipiki, bajaji, baiskeli na Punda kiongozi huyo kipenzi Cha Watanzania ameingia rasmi kwenye Jimbo lake la Singida Mashariki alilokuwa mbunge kwa vipindi viwili kabla hajapigwa risasi 16 mwilini mwake na watu wanaoitwa wasiojulikana.
Lissu amelakiwa na wazee, wanawake, vijana, watoto na vikongwe huku wakitandika kanga na nguo ili mwanamapinduzi huyo anayepewa nafasi kubwa ya kushinda Urais kuweza kupitia juu yake.
Hii ni historia.Hakika ndivyo tunavyoweza kusema.Kwa jinsi Lissu alivyolakiwa hapa wale waliotaka kumuua ni Kama Mungu ameshawapiga pigo Takatifu.
Mapokezi yake tumeelezwa na wazee hapa haijawahi kutokea tangia Uhuru wa Tanzania.
Watu Wazimia.
Wapo watu kadhaa ambao walizimia hususan baada ya kumuona.Wengine labda kwa sababu ya Furaha ya kumuona Tundu Lissu akitembea kwa miguu yake mwenyewe.Lakini wengine walizimia kutokana na umati mkubwa wa watu na kushindwa kuhimili.
Nyalandu aongoza mapokezi.
Kingine kilichovutia ni jinsi Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu alivyoongoza mapokezi ya Lissu.Nyalandu aliapa mbele ya umma wa watu wa Singida jinsi atakavyomuunga mkono Lissu mpaka ahakikishe ameapishwa kuwa Rais wa Tanzania.
Viongozi wa Dini na Kimila
Mara baada ya Kuwasili Lissu alifanyiwa maombi maalum na viongozi wote wa kidini na wale wazee wa Jadi.
Maombi hayo ni ya Kumlinda na kumkinga maadui zake hususan wale wabaya waliokula njama na kutaka kumuua.Kwamba wale wote walioshiriki ama kujua na kushindwa kuzuia waangamie kwa uovu wao.
Pia viongozi hao walimshukuru Mungu kwa jinsi alivyomkinga Lissu dhidi ya mkono wa Ibilisi.
Lissu Azungumza.
Akizungumza na halaiki hiyo ya watu Lissu aliwashukuru kwa mapokezi makubwa aliyopata kwenye Kijiji chake Cha Ikungi alikozaliwa.
Lissu amesisitiza kampeni bado hazijaanza na akasema kilichofanyika tu ni mapokezi ya kumlaki mtoto wao aliyeponywa na Mungu kwa makusudi maalum.
Lissu amewaeleza wanakijiji wenzake kwa kirefu jinsi alivyoshambuliwa na matibabu aliyopitia mpaka kupona kwake kwa miujiza.
Mwaka 2015 tuliona picha za kila aina zikiwemo za mifereji, mito, ziwa na Bahari yeye mafuriko lakini zote hazikufua dafu kwa CCM. Tujiandae kisaikolijia.
Mwaka 2015 tuliona picha za kila aina zikiwemo za mifereji, mito, ziwa na Bahari yeye mafuriko lakini zote hazikufua dafu kwa CCM. Tujiandae kisaikolijia.
Jambo jema ame return to his motherland aione hata nyumba yake, familia, majirani, wapiga kura wake, viongozi wa chama chake na wananchi wenye mapenzi mema aibu kwao waliotaka kutoa uhai wake kwamba mipango yao sio mipango ya Mungu