Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu ameingia jimboni kwake Singida Mashariki na kulakiwa na umati mkubwa wa watu kuwahi kushuhudiwa katika Jimbo Hilo.
Akiwa na msafara mkubwa wa magari, pikipiki, bajaji, baiskeli na Punda kiongozi huyo kipenzi Cha Watanzania ameingia rasmi kwenye Jimbo lake la Singida Mashariki alilokuwa mbunge kwa vipindi viwili kabla hajapigwa risasi 16 mwilini mwake na watu wanaoitwa wasiojulikana.
Lissu amelakiwa na wazee, wanawake, vijana, watoto na vikongwe huku wakitandika kanga na nguo ili mwanamapinduzi huyo anayepewa nafasi kubwa ya kushinda Urais kuweza kupitia juu yake.
View attachment 1532086View attachment 1532087View attachment 1532089
Tunaendelea kuwaletea kinachojiri.....Endelea kutufuatilia....