Tundu Lissu apata mapokezi ya Kifalme Kijijini kwao Singida

Tundu Lissu apata mapokezi ya Kifalme Kijijini kwao Singida

Umeona mapokezi ya membe na Maalim seif huko Zanzibar?. Yale ndio mapokezi ya mgombea urais. Haya ya kwenu ni kikao cha familia.
 
Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu ameingia jimboni kwake Singida Mashariki na kulakiwa na umati mkubwa wa watu kuwahi kushuhudiwa katika Jimbo Hilo.

Akiwa na msafara mkubwa wa magari, pikipiki, bajaji, baiskeli na Punda kiongozi huyo kipenzi Cha Watanzania ameingia rasmi kwenye Jimbo lake la Singida Mashariki alilokuwa mbunge kwa vipindi viwili kabla hajapigwa risasi 16 mwilini mwake na watu wanaoitwa wasiojulikana.

Lissu amelakiwa na wazee, wanawake, vijana, watoto na vikongwe huku wakitandika kanga na nguo ili mwanamapinduzi huyo anayepewa nafasi kubwa ya kushinda Urais kuweza kupitia juu yake.
View attachment 1532086View attachment 1532087View attachment 1532089
Tunaendelea kuwaletea kinachojiri.....Endelea kutufuatilia....
Wamekuja kushuhudia muujiza siyo Chadema!
 
Mapokezi huwa naamini ni picha za barabarani au mtu anapowasili ila hizo picha

raia mbona wamekaa wote nadhan na mgeni rasmi kashafika meza kuu katulia

ingependeza ungetuonesha picha za mapokezi ya kifalme mithili ya yesu akiingiia yerusalem

nadhani unakumbuka ingia na mapokezi ya yesu alivyokua akiingia yerusalem,picha za namna hyo sasa.
Hauwezi kuzipata.
 
Sasa Kama jimboni kwake watu waliojitokeza ni wachache kiasi hiki, halafu bado ana matumaini ya kushinda.

Yaani CDM kwa propaganda za uongo mko vizuri hayo ndiyo mapokezi ya kifalume aseee , waliopata mapokezi ya kifalume ni ACT kule Zanzibar.
 
Hivi Wana Sacco's wa Cha Domo Alie waroga ni Nani Kuna amsha amsha,shangwe na nyomi Kama la lowasa? Na alishindwa zile Ni vionjo vya kusindikiza ushindi wa mgombea wa CCM na hivi mnavyo viona kwa huyo mgonjwa wa sonona lisu Ni muendelezo wa shamra shamra za ushindi wa CCM?
Lowasa alishinda kamwachia Magu baada ya mazungumzo na wazee wa ccm,kwa Lisu musahau magu lazima aangukie pua
 
Tunaomba na clip ya hotuba yake tuongeze siku kwa aina ya faraja tunayopewa na huyu mfariji wetu.

Siyo yule anaongea utopolo tu na vibwagizo vyake ni vya kingono ngono tu.Hafai
 
Tupingane kwa hoja na si mitutu ya bunduki, kutekana na kutupwa kwenye viroba, matumizi ya nguvu za dola na kupigwa risasi mchana kweupe tena kwa kutumia silaha za kivita.
Musiba na Le Mutuz wamteka nani
 
Hivi Wana Sacco's wa Cha Domo Alie waroga ni Nani Kuna amsha amsha,shangwe na nyomi Kama la lowasa? Na alishindwa zile Ni vionjo vya kusindikiza ushindi wa mgombea wa CCM na hivi mnavyo viona kwa huyo mgonjwa wa sonona lisu Ni muendelezo wa shamra shamra za ushindi wa CCM?

Lowassa hakuja na nyomi cdm, bali alikuta nyomi cdm. Lisu kaitwa msaliti na hajafanya siasa kwa muda wa miaka mitatu, alitakiwa apokelewe na familia yake tu, maana Magufuli ndio amekuwa akifanya siasa peke yake, na kujenga madaraja, treni, bwawa la umeme nk.
 
Apokewa kifalme Singida....
IMG-20200809-WA0058.jpg
 
Back
Top Bottom