Tundu Lissu asafiri kwenda Ubelgiji kuonana na Daktari na kuhuisha visa yake

Tundu Lissu asafiri kwenda Ubelgiji kuonana na Daktari na kuhuisha visa yake

Nilisema humu
Mtu kama unakula vya mzungu bure bila kazi huwezi kukaa mda mrefu nje la sivyo wanakata riziki

Kwa hiyo nikasema atakaa kidogo tu na kurudi huku
Lissu afanyekazi ulaya aache hiyo disability allowance au incapacity la sivyo hawezi kuacha maisha ya bure kwani ni ulemavu pia
 
Watu wana akili za kwenye makalio. Lissu maisha yake amesafiri mara nyingi sana hata kabla ya kushambuliwa na maharamia. Kwani alisema anarudi Tz na hata safiri tena nje ya nchi? Acheni muwasho juzi tu ilikuwa Valentine's day hamjakunwa vizuri?
Chadema ishaanguka kitambo sana, Lissu hawezi tena kuishi Tanzania ni kama vile waafrica waliochomoka kwenda ulaya na kusahau kwao sasa ameramba ya ulaya Tz atakuja kwa kuzugazuga tu
 
Sasa km anaenda kumwona daktari wake shida iko wapi. Watanzania wengine mna roho za kichawi
Nilikuja na uzi humu Tundu Lissu kwa tabu atakaa wiki mbili baadae atadai kurudi kuonana na daktari, ukweli ni kwamba anazugazuga tu tayari ameshatengeneza maisha ya ulaya na hataacha kw sababu ya siasa za Tz, watanzania yafaa kujipanga kwa mwelekeo mwengine wa upinzani sio Chadema hii Tundu lissu na Mbowe
 
Waswahili walisema mbio za Sakafuni huishia ukingoni. Hatimaye sasa rasmi imekuwa wazi hakuna marefu yasiyo na ncha.Hatimaye Lissu achemsha na Kurudi Belgium.

Alikuja kwa mikwara mingi sana, wenye akili tulihoji hao watu anaozungumzia wako wapi? Na tukasema "muda utasema". Hatimaye sasa kachemsha mwenyewe. Hata kuondoka kwake hakuna viongozi wa chama walioenda kumsindikiza.

Pole sana Lissu, wakati mwingine utajifunza.

View attachment 2519055
Sasa wewe unajua karudi kwa sababu gani mpaka useme kachemsha?
 
Acha kuwa sungura kwani kumsindikiza kuna tofauti na kumpokea??? [emoji23][emoji23][emoji23] Eti ushamba na kupoteza muda kwahiyo mlipompokea mlikuwa washamba na mlipoteza muda??? Kweli nyie wazee Wa kubadili gia angani AKA Nyumbuzzzzz[emoji16][emoji16]
Aisee uliona wapi nasifia kupokea au kusindikiza mtu ? Tafuta comment yangu hata moja ambayo nasifia hivyo vitu Petty kama utaiona....

Ni mimi niliyeshagaa wakati Samia anaagwa na kupokelewa kwa watu kuacha kazi zao..., Ni mimi niliyemshangaa JPM na nchi kuacha shughuli eti wanapokea ndege..., Tuache kushabikia vitu visivyo na tija na wakati mwingine vikifanywa na serikali ni ubadhirifu wa pesa zetu
 
Akili za wasomi wetu ndani ya jf inatia walakini, nashindwa kuelewa kwamba tatizo la watanzania ni Lissu au?

Au ushabiki wa kivyama ndo imewafanya wanaojiita wasomi kujitoa ufahamu?

Watanzania tuna matatizo chungu nzima, lakini kama vijana wa nchi hii badala ya kuangalia ni kwa namna gani angalau tunajikwamua kutoka kwenye matatizo hayo, sisi tumeweka mbele ushabiki.

Katiba inahitajika, lakini sisi vijana hatuna habari nayo, tunamuachia Lissu aje aipiganie kwa ajili yetu, wakati sisi vijana tunapiga umbea, tutazidi kuwa masikini coz walio wengi hatujitambui.
 
Kusafiri kosa kisheria?
Chadema imekwisha lazima tuongee ukweli, mimi naichukia ccm lakini sioni upinzani wa chadema tena kama ilivyokuwa hapo kabla, Lissu hataweza kuish Tz kujua shida za Watanzania, ataongelea shida za Wtz kwenye Youtube, yake yanamuendea, Akija kwa uchaguzi ukiisha atarudi zake ulaya it is nonsense kwa siasa za Tz. Tanzania kunahitaji upinzani wa kupambana kama alivyokuwa maalim seif au zaidi ya hapo.
 
Nilikuja na uzi humu Tundu Lissu kwa tabu atakaa wiki mbili baadae atadai kurudi kuonana na daktari, ukweli ni kwamba anazugazuga tu tayari ameshatengeneza maisha ya ulaya na hataacha kw sababu ya siasa za Tz, watanzania yafaa kujipanga kwa mwelekeo mwengine wa upinzani sio Chadema hii Tundu lissu na Mbowe
  • Kwani kusafiri Kwa Tundu Lissu, ndio kusema upinzani umeisha nchini?
  • HIVI UNAJUA MBOWE alikuwa nje ya Tanzania kuanzia Kwa takriban miezi kadhaa kuanzia mwaka 2020 mwishoni hadi 2021
  • Mtu asisafiri? Kusafiri ni kosa?
 
Sasa wewe unajua karudi kwa sababu gani mpaka useme kachemsha?
We elewahivyo tu.
Kwani wakati anakuja sialisema anakuja kwa sababu gani,mbona anaondoka kimyakimya.
 
Chadema imekwisha lazima tuongee ukweli, mimi naichukia ccm lakini sioni upinzani wa chadema tena kama ilivyokuwa hapo kabla, Lissu hataweza kuish Tz kujua shida za Watanzania, ataongelea shida za Wtz kwenye Youtube, yake yanamuendea, Akija kwa uchaguzi ukiisha atarudi zake ulaya it is nonsense kwa siasa za Tz. Tanzania kunahitaji upinzani wa kupambana kama alivyokuwa maalim seif au zaidi ya hapo.
  • CHADEMA imekwisha Kwa sabb Lissu kasafiri?
  • unataka kusema Lissu Hana upinzani wa kupambana?
 
Waswahili walisema mbio za Sakafuni huishia ukingoni. Hatimaye sasa rasmi imekuwa wazi hakuna marefu yasiyo na ncha.Hatimaye Lissu achemsha na Kurudi Belgium.

Alikuja kwa mikwara mingi sana, wenye akili tulihoji hao watu anaozungumzia wako wapi? Na tukasema "muda utasema". Hatimaye sasa kachemsha mwenyewe. Hata kuondoka kwake hakuna viongozi wa chama walioenda kumsindikiza.

Pole sana Lissu, wakati mwingine utajifunza.

View attachment 2519055
Hawa ndio Propagandists wa CCM wanaowategemea..... imagine!
 
Back
Top Bottom