Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu, mimi nili like kabla Lissu hajaanza kuongea, baada ya kuyasoma aliyoyaongea nataka ni Like tena maana anastahili.Salaam Wakuu,
Muda wowote kuanzia sasa, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama cha CHADEMA, Tundu Lissu atakuwa anaongea na Waandishi wa Habari Nyumbani kwake Tegeta.
Nitawaletea kila kinachojiri Kutokea hapa Tegeta.
Agenda kubwa ni kusimamishwa kufanya Kampeni
======
UPDATES:
1654HRS: Waandishi wa Habari wameshafika eneo la tukio.
1704HRS
Tundu Lissu anasema
View attachment 1588251
Karibuni Nyumbani kwangu.
Mchana huu tume ya maadili imenisimamisha kufanya kampeni kuanzia kesho.
Uamuzi huu sio wa kushangaza hata kidogo.
Naomba nizungumze juu ya utaratibu ambao umefanyika.
1. Hadi sasa sijapatiwa tuhuma yoyote ya malalamiko ya mgombea yoyote au chama chochote kuhusu ukiukaji wa maadili yoyote. Sina taarifa yoyote ya maandishi kinyume cha utarsti6.
2. Sijapewa fursa yoyote ya kuwasilisha utetezi wa maandishi. Maadili yanasema ikitokea kuna malalamiko, anatakiwa apeleke kwa tume na mtuhumiwa apewe nakala na apewe masaa 42 ya kujibu.
3. Hadi sasa hakuna wito wowote wa kwenda kwenye kikao cha tume ya Maadili.
4. Nimepokea kama ninyi mlovyopokea kwa kupitia vyombo vya habari ambayo ni kinyume cha utaratibu.
HII HAISHANGAZI
Ukifuatilia Mikutano ya CCM, Tume ya Uchaguzi hasa Mahera, Magazeti ya Msiba, Ukiangalia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na CCM au wapambe wao, ADUI NAMBA MOJA NI TUNDU LISSU.
Uamuzi huu unathibitisha kwamba hatuna tume ya Uchaguzi bali tume ambayo inahakikisha CCM inabaki madalakani. Tangu 21 Septemba 2020, CHADEMA tumepeleka Malalamiko Matatu ya vitendo vya ukiukwajo ya maadili ya Uchaguzi dhidi ya Magufuli yanayohusiana na Rushwa.
Anapiga simu Waziri apeleke hela, jenga barabara hapa. Zote zile ni rushwa kwa mjibu wa gharama za Uchaguzi. Ni matendo yaliyokatazwa na sheria kwa sababu ni Rushwa.
Tumepeleka malalamiko hayo hayo kwa msajili wa vyama vya siasa.
Tume haijawahi kusema kwamba wamepokea Malalamiko ya vitendo vya Rushwa. Hakuna nliposikia.
Mnakumbuka Mahera alisema nini wiki iliyopita. Hata kabla sijalalamikiwa. Sijui barua walipeleka wapi.
NINI MSIMAMO WANGU?
Lengo halisi la msimamo huu sio kuniadhibu sababu nimekiuka maadili, bali ni kuhakikisha sifanyi Kampeni kipindi ambacho Magufuli hafanyi Kampeni. Hiivyo wamenisimamisha kipindi Magufuli akiwa Gereji.
Hoja nlizozitoa kwenye Kampeni hakuna Majibu hata moja.
Ujenzi wa Uwanja wa ndege wenye hadhi ya Kimataifa kijijini kwake. Na mlipaji mkuu ni Mtoto wa Kaka. Yote hayana majibu na mengine mengi.
Uamuzi huu sio wq haki, ni uamuzi wa kinyume na Sheria, na Uamuzi huu haukubaliki.
View attachment 1588258
Kamati kuu ya chama chetu inakutana kesho kujadili jambo hili.
Msimamo wangu Binafsi ni kwamba) Kampeni zinaendelea siku ya Jumapili kama ratiba ya tume ya Uchaguzi inavyosema. Huku nikisubiri Maamuzi ya Kamati kuu.
Ya kwangu kwa leo ni hayo.
Majaliwa anafanya Kampeni Maadili yanakataza
Magufuli anafanya Kampeni kwa kutumia Ratiba yake ambayo sio ya tume na hakuna anayehoji
Swali: Huoni unaleta Ukaidi? Sheria inasema nipewe nakala ya Mashitaka, sijapewa
Sheria inasema apewe masaa 48, sijapewa.
Sheria inasema akishitakiwa natakiwa apewe nakala ya Maamuzi, sijapewa.
Hiyo sio Sheria. So ninyamaze nionekane mwema? Ninyamaze niwapendezeshe wakina Polepole? Sijawahi kunyamaza. Natetea haki yangu
Swali: Huoni unafanya mambo kwa Jaziba?
Lissu: Mimi nina Jeshi? Nlisema Hatutokubali kuibiwa kura, hatutokubali kanuni zisipofuatwa. Kama hizo ndo Jaziba basi nina Kaziba
Swali: Kama Kamati kuu ikisema Usubiri Siku 7?
Jibu: Nitasubiri.
Swali: Barua inasema wamempa barua yako Katibu Mkuu.
Jibu: Haya maadili yalisainiwa na Wagombea.
Kuna maadili ya Chama na Maadili ya Mgombea.
Chadema haikuwa Mlalamikiwa aliyekuwa Mlalamikiwa ni Tundu Lissu. Kama Mlalamikiwa ni Tindu Lissu anayepelekewa ni nani?
Mimi nafuata ratiba ya Tume, Natembea na Askari Polisi amekaa nyuma ya kiti changu, Polisi magari Mawili ya Polisi, kila ninapolala Polisi Wanalinda. Hivyo tume wanajua nilipo, Wasingeshindwa lete barua.
Tume wana hofu kubwa ya kuniita. Wanakiuka maadili ili wasikutane na mimi Uso kwa uso.
Nizungumzie mgogoro wangu na Polisi.
Wito wa Polisi sio barua ya Mapenzi. Wito wa Polisi ni Amri. Kwa sababu ni amri ya Kisheria ina mashariti yake. Polisi hatakiwi kukuita kwa lolote bila kuambiwa Makosa yako.
Nmemsikia Sirro jana eti niende kujieleza Moshi. Kwa kosa lipi?
Mumeona barua ya Wambur7, umeona kosa lake? Eti nikajieleze kwa Matamshi. Matamshi gani?
Mimi sina Mpango huo wa kukanyagwa na watu wasiofuata Sheria. Unatakiwa Useme kosa. Sitakuja sababu najitambua. Asiyeelewa haki zake akiitwa na Polisi anaruka anaenda. Sio mimi.
Polisi alinifuata akasema asingefuata Ushauri ingeleta maafa.
Kwamba CCM walikua wanawaambia Polisi piga Mabomu. Watu waligoma kuondoka.
Mimi silisindikizwa na Polisi usiku ule hadi kwenye Mkutano pale Moshi nikasema mida umeisha, tawanyikeni wakatawanyika. Kosa langu ni lipi? Mlitaka wapigwe Mabomu?
Nyamongo mimi sikiwa na ratiba. Siku hiyo nlisindikizwa na Polisi OCD yupo mbele mimi katikati Polisi wengine Nyuma. Tulofanya mikitano Mitatu. Polisi wakikuta watu wananisubiri Wanasimamisha msafara nasalimia. Mimi na Nyamongo tuna urafiki kwani Wakati wa Mkapa nlikuwa nawatetea kuhusu Madini, Wasingekubali nipite bila kuongea.
Wale Polisi Walipiga Mabomu hadi yakawaishia watu wakaanza kurusha Mawe. Ikabidi nishuke kwenye gari baada ya kupiga Mabomu. Nikasema fanyeni mnachotaka. Tukafanya mkutano. Hao hao waliotupiga Mabomu baada ya Mkutano wakatusindikiza na Magari 10 mpaka Serengeti.
Kama ni sahihi kwa Magufuli ni sahihi kwa Tundu Lissu.
Feedback ya Mikoani si mnaona Nyomi? Ukweli ni kwamba tulipopita pote tunampiga Magufuli mapema sana. Tunampiga Mwanza, Geita, Kigoma. Na wakiiba hatukubali.. Kitanuka. Tunataka kama ni kushindwa tushindwe kihalali.
" Ni kipaji tu",sio wote wenye kipaji hiki.Nani yuko nyuma ya lissu mbona anajiamini Sana
Wee TAGA tuKama Lisu akishindwa kutii sheria bila shuruti atasaidiwa kukaa mahabusu kwa siku saba siku ya nane wataendelea na campaign. Dawa ya kibri ni kuwa na kibri zaidi yake.
Huku tunako kwenda,muda wowote Lissu anaweza akajitangaza Kama Raisi wa Tanzania maana yeye hata hiyo Tume ya Uchaguzi aiheshimu kabisa!!Sijaongelea kuwa au kutokuwa muhalifu. Sijaongelea kupata haki au kukosa haki. Nimeuliza anapata wapi ulinzi regardless ya anachotaka kufanyiwa na mamlaka kuwa ni haki au si haki. Nani anamlinda Tundulisu?
Hivi umeyaelewa maelezo yake au kwa kuwa kaandika kidhungu?Kama haiamini tume kwanini ashiriki uchaguzi? Si angeacha? Hiyo ingeleta maana kuwa kuna matatizo kwenye tume. Ni sawa na muumini anayemuomba Mungu bila kujua kuwa Mungu anaweza kufanya hicho anachokiomba. Wote wanaomuomba Mungu wanatumaini kuwa yupo na anaouwezo.
Kubahatisha hakufai
Wananchi kwa kupitia katiba yao.Sijaongelea kuwa au kutokuwa muhalifu. Sijaongelea kupata haki au kukosa haki. Nimeuliza anapata wapi ulinzi regardless ya anachotaka kufanyiwa na mamlaka kuwa ni haki au si haki. Nani anamlinda Tundulisu?
Amesoma, hakuacha elimu chuo kama wengine yeye aliondoka nayo.Nani yuko nyuma ya lissu mbona anajiamini Sana
Chama siyo yeye. Tatizo anachukulia yeye ni zaidi ya chama kwasababu mabeberu wanamjua yeye. Anataka afanye fujo ili mabwana zake wazungu waone.
Mataga mna tabu sana,ukisoma maelezo yake vizuri,huwezi kuandika ujinga Kama huuAnatafuta triggering factor...ya kuanzisha vurugu. Yawezekana ni moja ya kazi alizopewa, maana inasemwa si mwananchi mwenzetu yule. Fuatilieni ukweli wa hili.
Lissu kasema hawezi kuvumilia kukanyagwa na wa watu ambao wanatakiwa wafuate sheria.Hivyo hawawezi mfanya chochote sababu hawana kifungu cha sheria kinachowalazimu kumdhibiti.Hili taifa wote tunalielewa..... Tunajua matokeo ya kutokutii sauti za mamlaka.
Swali ni nani anamlinda Lisu? Kwann mamlaka zinapata shida kumdhibiti?
Tuache tu mapambano yaendelee boss.Iseme ww.
Lissu anachinja dume la ngombe bila kulifunga kamba japo anamalizia kukata koromeo, linapoelekea kukata roho hawezi kukwepa kujeruhiwa na mateke yake.Umma uko nyuma yako Tundu Lissu, umekwisha tuambia hawa polisi hawawezi kutuua wote, wengine ni watoto wetu, binamu zetu, jirani zetu.
Haki huchelewa lakini huwa inafika.
Tuache tu mapambano yaendelee boss.
Hilo jina linatumiwa hata na majambazi wakiponea chupuchupu kukamtwa.We una mwamini Mungu tuanzie hapo kwanza?
Anapambana na aliyeshika mpini. Busara ilikuwa ni chama chake kitoe tamko siyo yeye binafsi.
Yani ulipoandika 'balua' badala ya 'barua'nikagundua ww sio!?Lisu anajitoa ufahamu tu
Tume imepeleka balua ofisini kwenu, Mnyika kapokea, kawajibu kwamba hiyo haiwahusu, wampe mgombea mwenyewe!
Kama vile wewe ni mgombea binafsi siyo wa chadema!
Juzi umesikika ikiwa Tarime kwamba huendi kwa kuwa hukapewa balua!
Sasa je
Huna mawasiliana na chama chako?
Ikiwa hili ,wenzio wanajua lile!
Ikifanya ukaidi utaumia
Polisi watakufungua hivyo vyuma ulivyofunga mwilini kwako