Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema ataendelea na Kampeni. Adai Sheria ya Maadili imevunjwa kumsimamisha Kampeni

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema ataendelea na Kampeni. Adai Sheria ya Maadili imevunjwa kumsimamisha Kampeni

Anachokitafuta na Amsterdam wake wanakaribia kukipata. Niliwahi kusema Lissu ana akili nyingi sana za darasani Ila Elimu ya Dunia ni ZERO. No wonder anatembea kwa kuchechemea kwa kutofunzwa na ***** na kufunzwa na ulimwengu. Sasa acha ulimwengu uendelee kumfundisha zaidi.
Nchi hii imezoea maigizo sasa amekuja asiyejua maigizo ila ukweli sheria na kanuni zake.
Hao NEC wanaomzuia watajiju kwani hawajatoa ni kanuni ipi ya sgeria za nec ambayo Lissu hakuifuata.
Kwa mujibu wa sheria za Nec kwa suala la mlalamikaji ni kwa maandishi na anaelalamikiwa anatakiwa kujibu ndani ya saa 48 kwa maandishi kabla ya hatua nyingine.
Hayo hayajafanyika mleleta tu usanii wa siku za kale.
Sasa dunia italazimishwa kujiingiza rasmi katika uchaguzi wa Tanzania.
Suala hili lisipoangaliwa kwa umakini TZ inaingia kwenye vurugu za uchaguzi za mapema zisizotokana na utangazaji wa matokeo.
 
Lissu anachinja dume la ngombe bila kulifunga kamba japo anamalizia kukata koromeo, linapoelekea kukata roho hawezi kukwepa kujeruhiwa na mateke yake.
Kinukisheni sasa acheni vitisho mbuzi
 
Kutokana na agenda yake hilo la kuto tii kila mtu alilitarajia.

Kama watanzania wameshasahau risasi zake 16 asidhani akikamatwa atapata sympathy asilimia kubwa ya watanzania washamuona ni trouble maker tu hana jema.

Badala ya vyombo vya ulinzi kuwekwa ransom na kuangaika na Lissu pekee, hiyo adhabu NEC waipeleke CDM ikiwezekana asipotii wafungiwe kushiriki uchaguzi kama awawezi mdhibiti mgombea wao.
Umeisoma lakini maelezo yake? Au unaandika tu?
 
Wazanzibariiiiiiiiiiiiiiiiiiieeeeeeeeee eeeeeeeee eeeee... amkeni amkeni huu ndio mwaka wa mapambanooo
 
SSA Lissu mbona anakuwa mzembe.akapeleke malalamiko NEC kuhusu JPM na majaliwa kuvunja hizo kanuni. Kama aliyofanya kwenye pingamizi .
Napenda afanye hivyo jumatatu. Asilalamike anakoswa Sifa ya kuwa rais saasa
Amefanya hivyo, zaid ya siku 10 zilizopita, tume ikapiga kimya
 
Salaam Wakuu,

Muda wowote kuanzia sasa, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama cha CHADEMA, Tundu Lissu atakuwa anaongea na Waandishi wa Habari Nyumbani kwake Tegeta.

Nitawaletea kila kinachojiri Kutokea hapa Tegeta.

Agenda kubwa ni kusimamishwa kufanya Kampeni

======

UPDATES:

1654HRS: Waandishi wa Habari wameshafika eneo la tukio.

1704HRS

Tundu Lissu anasema
View attachment 1588251
Karibuni Nyumbani kwangu.

Mchana huu tume ya maadili imenisimamisha kufanya kampeni kuanzia kesho.

Uamuzi huu sio wa kushangaza hata kidogo.

Naomba nizungumze juu ya utaratibu ambao umefanyika.

1. Hadi sasa sijapatiwa tuhuma yoyote ya malalamiko ya mgombea yoyote au chama chochote kuhusu ukiukaji wa maadili yoyote. Sina taarifa yoyote ya maandishi kinyume cha utarsti6.

2. Sijapewa fursa yoyote ya kuwasilisha utetezi wa maandishi. Maadili yanasema ikitokea kuna malalamiko, anatakiwa apeleke kwa tume na mtuhumiwa apewe nakala na apewe masaa 42 ya kujibu.

3. Hadi sasa hakuna wito wowote wa kwenda kwenye kikao cha tume ya Maadili.

4. Nimepokea kama ninyi mlovyopokea kwa kupitia vyombo vya habari ambayo ni kinyume cha utaratibu.


HII HAISHANGAZI

Ukifuatilia Mikutano ya CCM, Tume ya Uchaguzi hasa Mahera, Magazeti ya Msiba, Ukiangalia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na CCM au wapambe wao, ADUI NAMBA MOJA NI TUNDU LISSU.

Uamuzi huu unathibitisha kwamba hatuna tume ya Uchaguzi bali tume ambayo inahakikisha CCM inabaki madalakani. Tangu 21 Septemba 2020, CHADEMA tumepeleka Malalamiko Matatu ya vitendo vya ukiukwajo ya maadili ya Uchaguzi dhidi ya Magufuli yanayohusiana na Rushwa.

Anapiga simu Waziri apeleke hela, jenga barabara hapa. Zote zile ni rushwa kwa mjibu wa gharama za Uchaguzi. Ni matendo yaliyokatazwa na sheria kwa sababu ni Rushwa.

Tumepeleka malalamiko hayo hayo kwa msajili wa vyama vya siasa.

Tume haijawahi kusema kwamba wamepokea Malalamiko ya vitendo vya Rushwa. Hakuna nliposikia.

Mnakumbuka Mahera alisema nini wiki iliyopita. Hata kabla sijalalamikiwa. Sijui barua walipeleka wapi.

NINI MSIMAMO WANGU?

Lengo halisi la msimamo huu sio kuniadhibu sababu nimekiuka maadili, bali ni kuhakikisha sifanyi Kampeni kipindi ambacho Magufuli hafanyi Kampeni. Hiivyo wamenisimamisha kipindi Magufuli akiwa Gereji.

Hoja nlizozitoa kwenye Kampeni hakuna Majibu hata moja.

Ujenzi wa Uwanja wa ndege wenye hadhi ya Kimataifa kijijini kwake. Na mlipaji mkuu ni Mtoto wa Kaka. Yote hayana majibu na mengine mengi.

Uamuzi huu sio wq haki, ni uamuzi wa kinyume na Sheria, na Uamuzi huu haukubaliki.
View attachment 1588258
Kamati kuu ya chama chetu inakutana kesho kujadili jambo hili.

Msimamo wangu Binafsi ni kwamba) Kampeni zinaendelea siku ya Jumapili kama ratiba ya tume ya Uchaguzi inavyosema. Huku nikisubiri Maamuzi ya Kamati kuu.

Ya kwangu kwa leo ni hayo.

Majaliwa anafanya Kampeni Maadili yanakataza

Magufuli anafanya Kampeni kwa kutumia Ratiba yake ambayo sio ya tume na hakuna anayehoji

Swali: Huoni unaleta Ukaidi? Sheria inasema nipewe nakala ya Mashitaka, sijapewa

Sheria inasema apewe masaa 48, sijapewa.

Sheria inasema akishitakiwa natakiwa apewe nakala ya Maamuzi, sijapewa.

Hiyo sio Sheria. So ninyamaze nionekane mwema? Ninyamaze niwapendezeshe wakina Polepole? Sijawahi kunyamaza. Natetea haki yangu

Swali: Huoni unafanya mambo kwa Jaziba?

Lissu: Mimi nina Jeshi? Nlisema Hatutokubali kuibiwa kura, hatutokubali kanuni zisipofuatwa. Kama hizo ndo Jaziba basi nina Kaziba

Swali: Kama Kamati kuu ikisema Usubiri Siku 7?

Jibu: Nitasubiri.

Swali: Barua inasema wamempa barua yako Katibu Mkuu.

Jibu: Haya maadili yalisainiwa na Wagombea.

Kuna maadili ya Chama na Maadili ya Mgombea.

Chadema haikuwa Mlalamikiwa aliyekuwa Mlalamikiwa ni Tundu Lissu. Kama Mlalamikiwa ni Tindu Lissu anayepelekewa ni nani?

Mimi nafuata ratiba ya Tume, Natembea na Askari Polisi amekaa nyuma ya kiti changu, Polisi magari Mawili ya Polisi, kila ninapolala Polisi Wanalinda. Hivyo tume wanajua nilipo, Wasingeshindwa lete barua.

Tume wana hofu kubwa ya kuniita. Wanakiuka maadili ili wasikutane na mimi Uso kwa uso.

Nizungumzie mgogoro wangu na Polisi.

Wito wa Polisi sio barua ya Mapenzi. Wito wa Polisi ni Amri. Kwa sababu ni amri ya Kisheria ina mashariti yake. Polisi hatakiwi kukuita kwa lolote bila kuambiwa Makosa yako.

Nmemsikia Sirro jana eti niende kujieleza Moshi. Kwa kosa lipi?

Mumeona barua ya Wambur7, umeona kosa lake? Eti nikajieleze kwa Matamshi. Matamshi gani?

Mimi sina Mpango huo wa kukanyagwa na watu wasiofuata Sheria. Unatakiwa Useme kosa. Sitakuja sababu najitambua. Asiyeelewa haki zake akiitwa na Polisi anaruka anaenda. Sio mimi.

Polisi alinifuata akasema asingefuata Ushauri ingeleta maafa.

Kwamba CCM walikua wanawaambia Polisi piga Mabomu. Watu waligoma kuondoka.

Mimi silisindikizwa na Polisi usiku ule hadi kwenye Mkutano pale Moshi nikasema mida umeisha, tawanyikeni wakatawanyika. Kosa langu ni lipi? Mlitaka wapigwe Mabomu?

Nyamongo mimi sikiwa na ratiba. Siku hiyo nlisindikizwa na Polisi OCD yupo mbele mimi katikati Polisi wengine Nyuma. Tulofanya mikitano Mitatu. Polisi wakikuta watu wananisubiri Wanasimamisha msafara nasalimia. Mimi na Nyamongo tuna urafiki kwani Wakati wa Mkapa nlikuwa nawatetea kuhusu Madini, Wasingekubali nipite bila kuongea.

Wale Polisi Walipiga Mabomu hadi yakawaishia watu wakaanza kurusha Mawe. Ikabidi nishuke kwenye gari baada ya kupiga Mabomu. Nikasema fanyeni mnachotaka. Tukafanya mkutano. Hao hao waliotupiga Mabomu baada ya Mkutano wakatusindikiza na Magari 10 mpaka Serengeti.

Kama ni sahihi kwa Magufuli ni sahihi kwa Tundu Lissu.

Feedback ya Mikoani si mnaona Nyomi? Ukweli ni kwamba tulipopita pote tunampiga Magufuli mapema sana. Tunampiga Mwanza, Geita, Kigoma. Na wakiiba hatukubali.. Kitanuka. Tunataka kama ni kushindwa tushindwe kihalali.
Lissu angekuwepo tangu zamani nchi hii mkoloni asingegusa , ama kama angegusa basi kiukweli hii nchi ingepata uhuru tangu 1930
 
Hapo ndio anaingia kwenye kumi na nane,akiendelea na kampeni wanamtoa kabisa, jeuri haina faida yeyote tena unae mfanyia jeuri ndio ana ubavu zaidi yako. Hivi jina likikatwa kwenye list ya wagombea atafanya nini?
Mataga mna tabu,msidhani Kama akitolewa uchaguzi utakuwepo,mchakato utaanza upyaaaaaaaaa!
Ndo mtazidi kumpa umaarufu
 
Back
Top Bottom