Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema ataendelea na Kampeni. Adai Sheria ya Maadili imevunjwa kumsimamisha Kampeni

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema ataendelea na Kampeni. Adai Sheria ya Maadili imevunjwa kumsimamisha Kampeni

Lisu anajitoa ufahamu tu
Tume imepeleka balua ofisini kwenu, Mnyika kapokea, kawajibu kwamba hiyo haiwahusu, wampe mgombea mwenyewe!
Kama vile wewe ni mgombea binafsi siyo wa chadema!
Juzi umesikika ikiwa Tarime kwamba huendi kwa kuwa hukapewa balua!
Sasa je
Huna mawasiliana na chama chako?

Ikiwa hili ,wenzio wanajua lile!
Ikifanya ukaidi utaumia
Polisi watakufungua hivyo vyuma ulivyofunga mwilini kwako
Hata kuandika neno "barua" tu hujui, hiyo akili ya kujibu hoja za lissu utaitoa wapi, ninyi ndio bendera fata upepo!
 
Huyu Lissu ni balaa yeye kapumuzika na Kampeni lakini tume na polisi wanamfanyia kampeni Mimi nilisema wamuache huu muda ni mfupi au tuseme ni mzimu wake unawasumbua kila muda mumutajetaje?
 
Salaam Wakuu,

Muda wowote kuanzia sasa, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama cha CHADEMA, Tundu Lissu atakuwa anaongea na Waandishi wa Habari Nyumbani kwake Tegeta.

Nitawaletea kila kinachojiri Kutokea hapa Tegeta.

Agenda kubwa ni kusimamishwa kufanya Kampeni

======

UPDATES:

1654HRS: Waandishi wa Habari wameshafika eneo la tukio.

1704HRS

Tundu Lissu anasema
View attachment 1588251
Karibuni Nyumbani kwangu.

Mchana huu tume ya maadili imenisimamisha kufanya kampeni kuanzia kesho.

Uamuzi huu sio wa kushangaza hata kidogo.

Naomba nizungumze juu ya utaratibu ambao umefanyika.

1. Hadi sasa sijapatiwa tuhuma yoyote ya malalamiko ya mgombea yoyote au chama chochote kuhusu ukiukaji wa maadili yoyote. Sina taarifa yoyote ya maandishi kinyume cha utarsti6.

2. Sijapewa fursa yoyote ya kuwasilisha utetezi wa maandishi. Maadili yanasema ikitokea kuna malalamiko, anatakiwa apeleke kwa tume na mtuhumiwa apewe nakala na apewe masaa 42 ya kujibu.

3. Hadi sasa hakuna wito wowote wa kwenda kwenye kikao cha tume ya Maadili.

4. Nimepokea kama ninyi mlovyopokea kwa kupitia vyombo vya habari ambayo ni kinyume cha utaratibu.


HII HAISHANGAZI

Ukifuatilia Mikutano ya CCM, Tume ya Uchaguzi hasa Mahera, Magazeti ya Msiba, Ukiangalia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na CCM au wapambe wao, ADUI NAMBA MOJA NI TUNDU LISSU.

Uamuzi huu unathibitisha kwamba hatuna tume ya Uchaguzi bali tume ambayo inahakikisha CCM inabaki madalakani. Tangu 21 Septemba 2020, CHADEMA tumepeleka Malalamiko Matatu ya vitendo vya ukiukwajo ya maadili ya Uchaguzi dhidi ya Magufuli yanayohusiana na Rushwa.

Anapiga simu Waziri apeleke hela, jenga barabara hapa. Zote zile ni rushwa kwa mjibu wa gharama za Uchaguzi. Ni matendo yaliyokatazwa na sheria kwa sababu ni Rushwa.

Tumepeleka malalamiko hayo hayo kwa msajili wa vyama vya siasa.

Tume haijawahi kusema kwamba wamepokea Malalamiko ya vitendo vya Rushwa. Hakuna nliposikia.

Mnakumbuka Mahera alisema nini wiki iliyopita. Hata kabla sijalalamikiwa. Sijui barua walipeleka wapi.

NINI MSIMAMO WANGU?

Lengo halisi la msimamo huu sio kuniadhibu sababu nimekiuka maadili, bali ni kuhakikisha sifanyi Kampeni kipindi ambacho Magufuli hafanyi Kampeni. Hiivyo wamenisimamisha kipindi Magufuli akiwa Gereji.

Hoja nlizozitoa kwenye Kampeni hakuna Majibu hata moja.

Ujenzi wa Uwanja wa ndege wenye hadhi ya Kimataifa kijijini kwake. Na mlipaji mkuu ni Mtoto wa Kaka. Yote hayana majibu na mengine mengi.

Uamuzi huu sio wq haki, ni uamuzi wa kinyume na Sheria, na Uamuzi huu haukubaliki.
View attachment 1588258
Kamati kuu ya chama chetu inakutana kesho kujadili jambo hili.

Msimamo wangu Binafsi ni kwamba) Kampeni zinaendelea siku ya Jumapili kama ratiba ya tume ya Uchaguzi inavyosema. Huku nikisubiri Maamuzi ya Kamati kuu.

Ya kwangu kwa leo ni hayo.

Majaliwa anafanya Kampeni Maadili yanakataza

Magufuli anafanya Kampeni kwa kutumia Ratiba yake ambayo sio ya tume na hakuna anayehoji

Swali: Huoni unaleta Ukaidi? Sheria inasema nipewe nakala ya Mashitaka, sijapewa

Sheria inasema apewe masaa 48, sijapewa.

Sheria inasema akishitakiwa natakiwa apewe nakala ya Maamuzi, sijapewa.

Hiyo sio Sheria. So ninyamaze nionekane mwema? Ninyamaze niwapendezeshe wakina Polepole? Sijawahi kunyamaza. Natetea haki yangu

Swali: Huoni unafanya mambo kwa Jaziba?

Lissu: Mimi nina Jeshi? Nlisema Hatutokubali kuibiwa kura, hatutokubali kanuni zisipofuatwa. Kama hizo ndo Jaziba basi nina Kaziba

Swali: Kama Kamati kuu ikisema Usubiri Siku 7?

Jibu: Nitasubiri.

Swali: Barua inasema wamempa barua yako Katibu Mkuu.

Jibu: Haya maadili yalisainiwa na Wagombea.

Kuna maadili ya Chama na Maadili ya Mgombea.

Chadema haikuwa Mlalamikiwa aliyekuwa Mlalamikiwa ni Tundu Lissu. Kama Mlalamikiwa ni Tindu Lissu anayepelekewa ni nani?

Mimi nafuata ratiba ya Tume, Natembea na Askari Polisi amekaa nyuma ya kiti changu, Polisi magari Mawili ya Polisi, kila ninapolala Polisi Wanalinda. Hivyo tume wanajua nilipo, Wasingeshindwa lete barua.

Tume wana hofu kubwa ya kuniita. Wanakiuka maadili ili wasikutane na mimi Uso kwa uso.

Nizungumzie mgogoro wangu na Polisi.

Wito wa Polisi sio barua ya Mapenzi. Wito wa Polisi ni Amri. Kwa sababu ni amri ya Kisheria ina mashariti yake. Polisi hatakiwi kukuita kwa lolote bila kuambiwa Makosa yako.

Nmemsikia Sirro jana eti niende kujieleza Moshi. Kwa kosa lipi?

Mumeona barua ya Wambur7, umeona kosa lake? Eti nikajieleze kwa Matamshi. Matamshi gani?

Mimi sina Mpango huo wa kukanyagwa na watu wasiofuata Sheria. Unatakiwa Useme kosa. Sitakuja sababu najitambua. Asiyeelewa haki zake akiitwa na Polisi anaruka anaenda. Sio mimi.

Polisi alinifuata akasema asingefuata Ushauri ingeleta maafa.

Kwamba CCM walikua wanawaambia Polisi piga Mabomu. Watu waligoma kuondoka.

Mimi silisindikizwa na Polisi usiku ule hadi kwenye Mkutano pale Moshi nikasema mida umeisha, tawanyikeni wakatawanyika. Kosa langu ni lipi? Mlitaka wapigwe Mabomu?

Nyamongo mimi sikiwa na ratiba. Siku hiyo nlisindikizwa na Polisi OCD yupo mbele mimi katikati Polisi wengine Nyuma. Tulofanya mikitano Mitatu. Polisi wakikuta watu wananisubiri Wanasimamisha msafara nasalimia. Mimi na Nyamongo tuna urafiki kwani Wakati wa Mkapa nlikuwa nawatetea kuhusu Madini, Wasingekubali nipite bila kuongea.

Wale Polisi Walipiga Mabomu hadi yakawaishia watu wakaanza kurusha Mawe. Ikabidi nishuke kwenye gari baada ya kupiga Mabomu. Nikasema fanyeni mnachotaka. Tukafanya mkutano. Hao hao waliotupiga Mabomu baada ya Mkutano wakatusindikiza na Magari 10 mpaka Serengeti.

Kama ni sahihi kwa Magufuli ni sahihi kwa Tundu Lissu.

Feedback ya Mikoani si mnaona Nyomi? Ukweli ni kwamba tulipopita pote tunampiga Magufuli mapema sana. Tunampiga Mwanza, Geita, Kigoma. Na wakiiba hatukubali.. Kitanuka. Tunataka kama ni kushindwa tushindwe kihalali.
Dar Mpya TV wamekula bando langu.Ila kwa kweli anajua kujenga hoja.
-Wamepeleleka malalamiko tume tangu 21 Sept lakini hajajibiwa.
-Kuna maadii ya vyama na maadili ya wagombea
-Yupo chini ya ulinzi wa askari kwa maana hiyo yupo jirani mno na serikali na angeweza kuletewa barua na ikamfikia bila kikwazo
-Polisi wametoa wito bila kutaja kosa
Nina wasiwasi ndani ya tume na ndani ya serikali kuna watu hawapo synchronised na matakwa yanayotakiwa.Kwa nini wanampa mwanya hivi??
I wish kama angetii tu na akautumia huo muda kujipanga na kusikiliza mikutano yake ya nyuma.
 
Ameambiwa ana nafsi ya kkukata rufaa,sasa hayo ya kuendelea na kampeni ni kutafuta shida nyingine!!Tunajua ameshapata momentum lakini ni lazima amkumbuke Mungu,Kila jambo lina sababu!!
Atamkumbuka Mungu Mara ngapi? Na wakati Mungu mwenyewe yu pamoja naye kila siku?
 
Umeisoma lakini maelezo yake? Au unaandika tu?
What’s new zaidi ya yale yale Magufuli sijui anafanya mikutano bila ya ratiba, Majaliwa nae anatumia magari ya serikali (waziri mkuu lazima alindwe) mara sijui uwanja wa chato.

Magufuli ni ‘incumbent’ president majukumu yake yataendelea huko USA Trump anapotoa stimulus packages za kupunguza athari za kiuchumi anatoa hongo au anafanya kazi yake tu.

Lissu is full of himself eti yeye kila mtu anamuangalia, off course because you seek that attention for the wrong reasons kwa kuvunja sheria na kuongea maneno ya shari. Lakini sio kwamba tishio kwenye sanduku la kura au sijui maamuzi ya NEC kwa sababu Magufuli anachukua mapumziko.

Nadhani ata yeye mwenyewe Lissu ameshanusa CDM wameanza kumchoka kesho kwenye icho kikao chao wasipomdhibiti adhabu itakayofuata iwe ya CDM yote this guy is a loose canon wakicheka nae ata wa-cost wengi huko CDM.
 
Angesusa si ccm wangeendelea na kujichagua?? Umesahau yaliyojiri wkt wa serikali za mitaa
Kama haiamini tume kwanini ashiriki uchaguzi? Si angeacha? Hiyo ingeleta maana kuwa kuna matatizo kwenye tume. Ni sawa na muumini anayemuomba Mungu bila kujua kuwa Mungu anaweza kufanya hicho anachokiomba. Wote wanaomuomba Mungu wanatumaini kuwa yupo na anaouwezo.

Kubahatisha hakufai
 
Lisu, Kanyaga hapo hapo. Hata China tulikuwa nao sawa kiuchumi hadi miaka ya 1940+, chini ya utawala wa rais Chiang Khai Sheck na serikali ya Kuomintang. Lakini wananchi walipambania Uhuru wa haki na maendeleo hadi kufikia kuiweka madarakani serikali ya Mao Tse Tung, na kufanya maendeleo yakue kwa kasi China.

Now, we need a new government and new strategies of governance.

Why always CCM????

Tubadilike Watanzania, sio kila siku CCM. Unakuta walevi mtaani wamechachamaa CCM mbele kwa mbele huku wakiwa na shida tupu za maisha.

Changes cames by struggle.
 
Mataga mna tabu sana,ukisoma maelezo yake vizuri,huwezi kuandika ujinga Kama huu
Nasema yawezekana si mwenzetu...kama ni mwenzetu tujiulize je familia yake anaijengea mazingira ya kuipenda Tanzania na watanzania? Ama anataka kuitumia Tanzania kwa maslahi yake binafsi? Jiulize kama anatekeleza kwa ufasaha wajibu huo wa kizalendo kuwandaa familia yake kuwa raia wanaoipenda nchi hii liwe jua iwe mvua! Ukifanikawa kupata majibu rudi jukwaani tuendelee na majadala.
Umeandika nini Sasa?
Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
Vua miwani ya mbao na utumie macho yako uliyopewa na Rabuka mwingi wa rehema kusoma nilichoandika. Na hapo swali lako litapata majibu.
 
"...wamenisimamisha kipindi Magufuli akiwa Gereji...." Mh. Tundu Antipasi Lissu.
Hapa ndipo huwa najiuliza akili za huyu mheshimiwa huwa zinakwama wapi, yaani bila "personal attack" hawezi kuelezea jambo na jamii ikaelewa? Tuliosoma NLP (Neuro-linguistic Programming) tunajua kuwa kichwani mwa Lissu kuna shida au ya kuzaliwa au ya kimalezi tu,... macho uona kile mtu anachokiwaza..
 
Lissu ndie mgombea urais kupitia chadema pia ni Kaimu/Mwenyekiti.Hivyo anavyoongea anaongea kama yeye pia kwa niaba ya Chama.
Anapambana na aliyeshika mpini. Busara ilikuwa ni chama chake kitoe tamko siyo yeye binafsi.
 
Nasema yawezekana si mwenzetu...kama ni mwenzetu tujiulize je familia yake anaijengea mazingira ya kuipenda Tanzania na watanzania? Ama anataka kuitumia Tanzania kwa maslahi yake binafsi? Jiulize kama anatekeleza kwa ufasaha wajibu huo wa kizalendo kuwandaa familia yake kuwa raia wanaoipenda nchi hii liwe jua iwe mvua! Ukifanikawa kupata majibu rudi jukwaani tuendelee na majadala.

Vua miwani ya mbao na utumie macho yako uliyopewa na Rabuka mwingi wa rehema kusoma nilichoandika. Na hapo swali lako litapata majibu.
Siyo kosa lako.

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
Changes cames by struggle.
Crazy Benghazi hooligans had the same thinking, when they decided to torpedo the Libyan nation's boat. However, let us all be clear right here that the crazyness of that nature will be nipped at its bud then everything will be uprooted!!
 
Back
Top Bottom